Kwanini wanaume tunafurahi maanguko ya wanaume wenzetu?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Nilikuwa nakula chakula ghafla zikaja kumbukumbu mbaya za vicheko na maneno ya kejeli ya "Hahaha... kanyooshwa", "Kwisha habari yake 'bwege' yule...", "Mshamba tu chezea wanawake wewe", "Usicheze na mwanamke jamaa kashawahishwa (akimalizia na emoj za kucheka)", "Jamaa lina kib... lile (akimalizia na emoj za kumcheka mwanaume mwenzake).

Nikaona nisiendelee kula acha niliseme hili, this should come to an end. Zamani tulisema wanawake hawapendani, siku hizi wanawake wanasema wanaume hatupendani.

Jamani, kwamba meza ndiyo imepinduka kwa dk chache hivyo? Hapana sitaki kuamini.

Zaidi ya nyuzi 100+ tofauti zihusuzo visa vya wanaume kudhulumiwa, kufilisiwa au kufanyiwa uhuni na wanawake humu ndani, zote kuna zaidi ya 98+% wanaume wakishangilia maanguko ya wanaume wenzao.

Achana na nyuzi nyingine za hapa na pale. Hii si sawa.

Unapata faida gani kwa kushangilia mwanaume mwenzio anapodhulumiwa na mwanamke? Unafaidika na mgao?

Wanawake wamekuwa na utu na wanapendana mno kiukweli. Umebaki msemo wa mdomoni tu kuwa hawapendani. Ila kiuhalisia wanajaliana mno.

Leo hii hata mitaani tu, mwanaume akifanyiwa uhuni hata kwa kuonewa, midume na ndevu zao kabisa inakimbilia kucheka na kutangaza aibu za mwanaume mwenzao.

Wanaume ndiyo tumefika hapa?

Nawalenga wanaume wenye tabia hizi ambao wamejaa sana JF na as days go on wanazidi kuongezeka kwa kasi. Kwenye kila post ya mwanaume kudhulumiwa au kufanyiwa uhuni iwe na mke au mwanamke, utakuta zinajichatisha emoj's za kucheka, mpaka unabaki na maswali, why this? Are these really the humans?

Wanazitag wenzao wanasaidiana kucheka kwenye nyuzi za huzuni za wanaume wenzao. Hii ifike mwisho!
 
Nilikuwa nakula chakula ghafla zikaja kumbukumbu mbaya za vicheko na maneno ya kejeli ya "hahaha... kanyooshwa", "kwisha habari yake 'bwege' yule...", "mshamba tu chezea wanawake wewe", "usicheze na mwanamke jamaa kashawahishwa (akimalizia na emoj za kucheka)", "jamaa lina kib... lile (akimalizia na emoj za kumcheka mwanaume mwenzake).

Nikaona nisiendelee kula acha niliseme hili, this should come to an end. Zamani tulisema wanawake hawapendani, siku hizi wanawake wanasema wanaume hatupendani.

Jamani, kwamba meza ndiyo imepinduka kwa dk chache hivyo? Hapana sitaki kuamini.

Zaidi ya nyuzi 100+ tofauti zihusuzo visa vya wanaume kudhulumiwa, kufilisiwa au kufanyiwa uhuni na wanawake humu ndani, zote kuna zaidi ya 98+% wanaume wakishangilia maanguko ya wanaume wenzao.

Achana na nyuzi nyingine za hapa na pale. Hii si sawa.

Unapata faida gani kwa kushangilia mwanaume mwenzio anapodhulumiwa na mwanamke? Unafaidika na mgao?

Wanawake wamekuwa na utu na wanapendana mno kiukweli. Umebaki msemo wa mdomoni tu kuwa hawapendani. Ila kiuhalisia wanajaliana mno.

Leo hii hata mitaani tu, mwanaume akifanyiwa uhuni hata kwa kuonewa, midume na ndevu zao kabisa inakimbilia kucheka na kutangaza aibu za mwanaume mwenzao.

Wanaume ndiyo tumefika hapa?

NB

Nawalenga wanaume wenye tabia hizi ambao wamejaa sana JF na as days go on wanazidi kuongezeka kwa kasi. Kuna ID's sitozitaja, ila zinasikitisha sana...

Kwenye kila post ya mwanaume kudhulumiwa au kufanyiwa uhuni iwe na mke au mwanamke, utakuta zinajichatisha emoj's za kucheka... mpaka unabaki na maswali, why this? Are these really the humans?

Wanazi tag na ID za kike wanasaidiana kucheka kwenye nyuzi za huzuni za wanaume wenzao. Hii ifike mwisho........!!!!!!!!
Lini walikuwa wanasikitika ukifilisika? Ni ndugu zako hao?
 
Ukiwa tajiri ishi vizuri na watu, ukifilisika watakuhurumia, ukiwa mbali na watu, ukifilisika watashangilia. Kuna mmoja aliambiwa"njoo nikupe kazi ya kuchimba choo".
 
Back
Top Bottom