Kwanini Wanaume nao wasiwe 'wanafundwa' kabla ya kufunga ndoa?

Kuna baadhi ya familia kwenye maeneo mwanamke akiwa anaenda kuishi na mume anapewa ABCD.. za namna ya kujenga na kudumisha ndoa na familia bora, pengine yatakua yanasaidia kwa kiasi chake
Zamani walikuwa wakifundishwa pia wanaume

Ila siku hizi nashangaa kwa nini wanawake tu ndio huwa wanapewa haya mafundisho? maana matatizo ya wanaondoa na familia hayasababishwi na mwanamke peke yake, mwanaume anaweza akawa ndio tatizo la familia kuparanganyika au familia kuishi kwa shida

Familia nyingi zinakumbwa na matatizo ya baba kuwa mlevi, mgomvi, anayetumia fedha hovyo, mvivu, ufuska, negligent n.k ambayo yanakwamisha familia nyingi na nyingine kuvunjika.
Pengine hawa vijana wanoingia kwenye ndoa wangekuwa 'mentored' namna ya kwenda kujenga familia bora.

Naona kama kuna attitude iliyojengeka ya kuwa ndoa ikivunjika ni kosa la mwanamke, na akirudi kwao kisa kashindwana na mume basi huyo ni mzembe ndio maana pengine hili halipo
tufundwe kwaajili ya nn ,(wanawake ni wasaidizi wetu ndo maana wanafundwa)
 
Utasubiri sana wanaume wafundwe. Ndoa imebase upande mmoja. Mke awe mtakatifu.. mume afanye atakavyo. Matatizo mengi ya ndoa mke ndo atalaumiwa hata kama tatizo ni la mume.
 
Hapana sio mfumo ila tunaamini mwanamke akikosa maadili athari yake ni kubwa sana kuliko mwanamme coz yeye anahusika moja kwa na malez ya mtoto japo na mume anahusika ila tunaangalia kwa % hapo mara nyingi majukumi ya mume
Hapo ndio mnapokosea. Mke peke yake awe na maadili. Huoni kama unampa mzigo mke kuishi na mume asiye na maadili? Au ni kazi ya mke kumrekebisha mume?
 
Kuna baadhi ya familia kwenye maeneo mwanamke akiwa anaenda kuishi na mume anapewa ABCD.. za namna ya kujenga na kudumisha ndoa na familia bora, pengine yatakua yanasaidia kwa kiasi chake
Zamani walikuwa wakifundishwa pia wanaume

Ila siku hizi nashangaa kwa nini wanawake tu ndio huwa wanapewa haya mafundisho? maana matatizo ya wanaondoa na familia hayasababishwi na mwanamke peke yake, mwanaume anaweza akawa ndio tatizo la familia kuparanganyika au familia kuishi kwa shida

Familia nyingi zinakumbwa na matatizo ya baba kuwa mlevi, mgomvi, anayetumia fedha hovyo, mvivu, ufuska, negligent n.k ambayo yanakwamisha familia nyingi na nyingine kuvunjika.
Pengine hawa vijana wanoingia kwenye ndoa wangekuwa 'mentored' namna ya kwenda kujenga familia bora.

Naona kama kuna attitude iliyojengeka ya kuwa ndoa ikivunjika ni kosa la mwanamke, na akirudi kwao kisa kashindwana na mume basi huyo ni mzembe ndio maana pengine hili halipo
Huyo mwanamke hakutakiwa kurudi kwao kule alishaondoka. Wanaume nao wapewe homeparty.
 
Hapo ndio mnapokosea. Mke peke yake awe na maadili. Huoni kama unampa mzigo mke kuishi na mume asiye na maadili? Au ni kazi ya mke kumrekebisha mume?
Wanaume wengi siku hizi wasumbufu sana kwenye ndoa japo wanawake wanalaumiwa walio wengi hawajui wajibu wao kama baba au mme bali ni ubabe mke anakuwa kama chombo tu ule udhamani ni kidogo yaani na wao wanatakiwa kupewa somo jinsi ya kuishi na mkewe, wake wana vumilia sana ubabe mwingi sana mke akiongea ataambiwa ana mdomo sana lakini kama anaongea sana embu fanyia kazi hayo anayolalamikia au kaa chini muulize mke nini tatizo hapo mambo yatàkaa vizuri lakini duu vyumba vinaficha mengi sana
 
Kuishi na mwanaume ni rahisi sana maana maisha yetu huwa simple ndio maana wanawake mnaweza kuambiwa vitu vya kufanya ili mambo yaende sawa.

Ila kwa upande wenu wanawake maisha yenu ni complicated na hakuna formula maalum ambayo wanaume tunaweza kupeana/kufundishana ili kuwamudu ndio maana kila mwanaume anatumia akili za kuzaliwa nazo tu.
 
Hapana mkuu wanaume wengi wabinafsi sana na matatizo mengi yanaanzia kwenye mgegedo hiyo souce kubwa sana ktk ndoa japo halisemwi sana wanawake wengi hawalizishwi ndiyo maana wengi wao stress nyingi wanaume wengi mkanda juu lakini huko ni sifa tu bilabila halafu hao kwa wivu ni balaa mke asitoke kidogo wapi unaenda anajua yeye hakuna kitu
 
mbona kuna bag party za wanaume ambao wanaingia kwenye ndoa kuna baadhi ya familia wanawafanyia watto wao wa kiume siku chache kabla ya kuingia kwenye ndoa
kama kitchen party tu upande wa mwanamke
 
Huyo kiumbe mwanamke kwa kua alishikiliwa akili na sheitwan lazma apigwe msasa kabla ya ndoa!
Na Mama, Dada yako na Binti yako nao wameshikwa akili na shetani? Ina maana umzaliwa na mtu asiye na akili zake Bali za shetani? Wewe ni zao shetani simply put
 
Back
Top Bottom