Kwanini WANASIASA hudanganya wakati wa Kampeni? Sababu kuu JAMII hupenda KUDANGANYWA

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,598
3,644
Jamii au wananchi asilimia kubwa huamini uongo kuliko ukweli. Hivyo basi Wanasiasa hutumia nafasi hiyo ya kudanganya kwa sababu jamii hupenda kudanganywa.

Haijalishi ni Afrika au Ulaya au Amerika, siku zote mwanasiasa mkweli ni mara chache sana kupata ushindi kwa kuongea ukweli.

Watu hupenda kusikia vile vitu wanavyopenda kuvisikia na si vinginevyo. Ikitokea kuna wagombea wawili wanaochuana vikali kuwania Urais au Ubunge; mmoja wapo AONGEE UKWELI na mwingine AONGEE KILE AMBACHO JAMII INAPENDA KUKISIKIA, basi kitakachotokea ni kwamba yule aliyezungumza yale ambayo jamii inapenda kuyasikia lazima atashinda huo UCHAGUZI na yule mzungumza UKWELI atashindwa.

Kwahiyo mara nyingi kama mgombea unataka kushinda uchaguzi inabidi uanze kampeni za KUDANGANYA ili yule MSEMA UKWELI atakapo kuja akose nafasi ya kuwashawishi wapiga kura.


HALI ILIVYO HAPA TANZANIA:
Kati ya Magufuli na Lowasa mmoja wapo lazima awe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukifuatilia Kampeni zao kuna mmoja anaoongea UKWELI na kuna mwingine anaongea UONGO {anaongea yale ambayo jamii inataka kusikia}.

liberals-lies-politics-1343567933.jpg


1397741061b0c8ee_l.jpg


Kwa wale MATOMASO pitieni LINK HIZI:
1.
https://www.google.com/url?sa=t&rct=...VRFtkCCVkPal2g


2.
https://www.google.com/url?sa=t&rct=...zorOo94nXWIT0A

 
Iyo ni kawaida mkuu, tuliambiwa tuchague mtu sio chama, badae tumeona ikiwa ni chama au ni mtu
 
Back
Top Bottom