Kwanini wanaotoa matamko ya kulaani, laana haziwapati wanaolaaniwa?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Mara nyingi, tumekuwa tukisikia taasisi za kijamii, wanaharakati, wananchi nk wakiilaani nchi fulani au viongozi wa kisiasa kwa madai kwamba wamekosea au kutenda jambo linalowaletea maumivu.

Wakati mwingine watu wenye dini nao husikika wakitamka maneno ya laana dhidi ya wale wanaoona wamekosea. Na wengine huwaombea wakosaji wapatwe na mabaya kama kifo, magonjwa au ajali. Kwanini mara nyingi, laana hizo hazitimii au haziwapati wanaolaaniwa?

Sababu kubwa ni kwamba Mungu hapendi tuwalaani wenzetu. Maandiko yanasema hivi katika Warumi 12:14
"Wabarikini wale wanaowaudhi, barikini wala msilaani..” Tafsiri nyingine ya andiko hilo inasema: "Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani."

Maneno ya laana yanajenga mazingira ya kisasi, chuki, na kutotubu. Lakini baraka—hata kwa maadui—hufungua mlango wa neema, uponyaji, na mageuzi ya kweli. Mungu hajihusishi na laana zinazotokana na hasira za kibinadamu.

Laana inayotoka kwa mtu asiyeongozwa na Roho wa Mungu, haipati kibali kwa Mungu, ndio sababu laana nyingi za watu haziwapati wanaolaaniwa.

Kama kuna nchi inayolaaniwa sana ni Israeli. Lakini badala ya kulaanika, tunaona ikiendelea kustawi. Na wanaoilaani wenyewe ndio wanapatwa na mabaya!
 
Maandiko ya kutafakari zaidi:

1 Petro 3:9
"Msiwalipe watu ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; bali watakieni baraka, maana nyinyi mliitwa na Mungu mpate kupokea baraka."

Mathayo 5:44
“Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.”

Warumi 12:21
"Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema..”
 
Mara nyingi, tumekuwa tukisikia taasisi za kijamii, wanaharakati, wananchi nk wakiilaani nchi fulani au viongozi wa kisiasa kwa madai kwamba wamekosea au kutenda jambo linalowaletea maumivu.

Wakati mwingine watu wenye dini nao husikika wakitamka maneno ya laana dhidi ya wale wanaoona wamekosea. Na wengine huwaombea wakosaji wapatwe na mabaya kama kifo, magonjwa au ajali. Kwanini mara nyingi, laana hizo hazitimii au haziwapati wanaolaaniwa?

Sababu kubwa ni kwamba Mungu hapendi tuwalaani wenzetu. Maandiko yanasema hivi katika Warumi 12:14
"Wabarikini wale wanaowaudhi, barikini wala msilaani..” Tafsiri nyingine ya andiko hilo inasema: "Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani."

Maneno ya laana yanajenga mazingira ya kisasi, chuki, na kutotubu. Lakini baraka—hata kwa maadui—hufungua mlango wa neema, uponyaji, na mageuzi ya kweli. Mungu hajihusishi na laana zinazotokana na hasira za kibinadamu.

Laana inayotoka kwa mtu asiyeongozwa na Roho wa Mungu, haipati kibali kwa Mungu, ndio sababu laana nyingi za watu haziwapati wanaolaaniwa.

Kama kuna nchi inayolaaniwa sana ni Israeli. Lakini badala ya kulaanika, tunaona ikiendelea kustawi. Na wanaoilaani wenyewe ndio wanapatwa na mabaya!
ni kwa sababu laana donot exist, it is just kutishana
 
Laana zipo ndugu yangu Retired .
Hii hapa ni baadhi ya mifano ya laana zenye msingi wa Mungu, yaani, laana ambazo Mungu mwenyewe alizitamka au alizidhihirisha kupitia manabii wake, na zikawapata waliohusika kwa sababu ya uasi, dhambi, au ukaidi. Tofauti na laana za kibinadamu, hizi zilikuwa na mamlaka halali na matokeo ya kweli.

Adamu na Hawa baada ya kuasi kwa kula tunda walilokatazwa, walilaaniwa (Mwanzo 3:16–19). Mwanamke alilaaniwa kuwa atakuwa akizaa kwa uchungu, jambo linaloendelea hadi leo. Na mwanaume alilaaniwa kuwa atakuwa akila kwa jasho tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Isitoshe ardhi yenyewe ililaaniwa. Ikaanza kuzaa miiba na wadudu wabaya wanaoshambulia mazao wakaanza uharibifu.

Nchi ya Misri ililaaniwa kwa kupata mapigo kumi (Kutoka 7–12). Farao alikataa kuwaachilia Waisraeli licha ya onyo la Mungu kupitia kwa Musa. Mungu akawaletea laana ya kiuchumi (kuharibiwa kwa mazao, mifugo, maji) na hatimaye kifo cha wazaliwa wa kwanza. Hiyo ilikuwa laana ya kitaifa, ya wazi kabisa kutoka kwa Mungu.
 
Mara nyingi, tumekuwa tukisikia taasisi za kijamii, wanaharakati, wananchi nk wakiilaani nchi fulani au viongozi wa kisiasa kwa madai kwamba wamekosea au kutenda jambo linalowaletea maumivu.

Wakati mwingine watu wenye dini nao husikika wakitamka maneno ya laana dhidi ya wale wanaoona wamekosea. Na wengine huwaombea wakosaji wapatwe na mabaya kama kifo, magonjwa au ajali. Kwanini mara nyingi, laana hizo hazitimii au haziwapati wanaolaaniwa?

Sababu kubwa ni kwamba Mungu hapendi tuwalaani wenzetu. Maandiko yanasema hivi katika Warumi 12:14
"Wabarikini wale wanaowaudhi, barikini wala msilaani..” Tafsiri nyingine ya andiko hilo inasema: "Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani."

Maneno ya laana yanajenga mazingira ya kisasi, chuki, na kutotubu. Lakini baraka—hata kwa maadui—hufungua mlango wa neema, uponyaji, na mageuzi ya kweli. Mungu hajihusishi na laana zinazotokana na hasira za kibinadamu.

Laana inayotoka kwa mtu asiyeongozwa na Roho wa Mungu, haipati kibali kwa Mungu, ndio sababu laana nyingi za watu haziwapati wanaolaaniwa.

Kama kuna nchi inayolaaniwa sana ni Israeli. Lakini badala ya kulaanika, tunaona ikiendelea kustawi. Na wanaoilaani wenyewe ndio wanapatwa na mabaya!
Labda tatizo lako ni kutokujua maana ya laana ....siku moja nilishuhudia mmama akichwapwa makofi na mtoto wake ...kisha yule mmama alikuwa ana lalamika kuwa huyo mtoto kamlaani lakini wapi!!!....hapo nikajua huyo mmama ni mpumbavu .
 
Laana isiyo na sababu(yaani isiyokubalika mbele za Mungu) haiwezi kumpata mtu. Ila huyo mtoto kumpiga mama yake sio mapenzi ya Mungu. Laana inaweza kumpata. Na sio lazima matokeo ya laana yaonekane saa hiyohiyo.
 
Kwa sababu hizo laana haziwapati
Wewe umesema una cheo cha kukusanya sadaka kanisani. Inakuwaje unatamani watu walaaniwe? Au unakusanya sadaka kwa manabii wa mchongo?
 
Laana isiyo na sababu(yaani isiyokubalika mbele za Mungu) haiwezi kumpata mtu. Ila huyo mtoto kumpiga mama yake sio mapenzi ya Mungu. Laana inaweza kumpata. Na sio lazima matokeo ya laana yaonekane saa hiyohiyo.
Kitu kilicho laaniwa maana yake kime fungiwa kutenda mema ...hivyo mtu muovu akilaaniwa maana yake atazidi kuwa muovu na kutenda ushenzi zaidi ndiyo maana ya laana..mfano ni kama samia bushiri
 
Wewe umesema una cheo cha kukusanya sadaka kanisani. Inakuwaje unatamani watu walaaniwe? Au unakusanya sadaka kwa manabii wa mchongo?
C ht Mungu nae alishawahi kutoa laana, hvy Siwez kumpinga sir God
 
Back
Top Bottom