Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,901
- 20,417
Wanabodi, kwa nyakati tofauti tumeshuhudia taarifa mbalimbali za CHADEMA kulalamikia mapingamizi waliyowekewa wagombea wao ambayo yametokana na umbumbumbu wa viongozi wa ngazi ya Mikoa na Wilaya wa chama hicho katika kusimamia zoezi zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hata hivyo, kwa siku za karibuni, kuna kelele nyingi na utapeli uliokuwa unafanywa na CHADEMA kutuaminisha kuwa UKAWA ndo mbadala wa vyama vilivyoungana. Kabla ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, tulikuwa tunashuhudia viongozi wa UKAWA wakikutana na kutoa matamko ya pamoja pale wanapoona mambo hayaendi sawa.
Ila tangu mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ulipoanza, ni CHADEMA pekee wanaojitokeza kulalamika kuwa wagombea wao wameenguliwa kutokana na mapingamizi waliyowekewa na wagombea wa CCM. Binafsi napata shinda sana katika hili na najiuliza maswali yafuatayo
Hakika nina mengi ila naamini wadau mtasaidia kuweka sawa hili.
Nawasilisha

- Kwa nini wanaojitokeza kulalamika kuwa wagombea wao wamewekewa mapingamizi na CCM ni CHADEMA tu?
- Je hakuna wagombea wa vyama vingine washirika wa UKAWA wamewekewa mapingamizi?
- Kama hakuna wagombea wa vyama vingine waliowekewa mapingamizi, je CHADEMA waliteleza wapi na je ni kweli kuwa zoezi hili lilisimamiwa na UKAWA au kila chama kilikuwa na mikakati yake?
- Kwa nini viongozi wakuu wa UKAWA hawakutani na kutoa tamko la pamoja ilhali mambo yanazidi kwenda mrama?
Hakika nina mengi ila naamini wadau mtasaidia kuweka sawa hili.
Nawasilisha