Mimi ninaona kama Taifa na bara kwa ujumla bado tunasafari ndefu sana katika swala zima la kupiga hatua kutoka hapa tulipo kuingia japo hata kwenye njia ya kwenda kule tunapopatazamia ,,
Tofauti na hilo wanaloliongelea kuna mambo mengi sana ambayo yangefanyika na kuokoa baadhi ya gharama na pengine kuleta pesa nyingi kwa muda Fulani kama ifuatavyo :
1. Katika kipindi nilichotembea baadhi ya mikoa hapa Tanzania kwa mihangaiko ya maisha , nimekuta mabango ya kutoa heko kwa raisi juu ya ufanyaji kazi , mabango ambayo kwanza yatatengenzwa kwa gharama kubwa na pia yasingekuwepo ingeleta fursa ya mengine ya kibiashara kuwekwa na watu binafsi na kuleta ushuru.. RAISI KAMA KALETA MAJI MIMI NITAJUA ,KAMA KALETA UMEME NITAONA TU , SASA NINAUMIA SANA NINAPOONA MARKETING STRATEGIES ZINATUMIKA KWENYE SIASA TENA YA URAIS.
2. Sijui kama nakosea lakini , binafsi naona kama taifa tunatumia gharama kubwa sana zisizo za msingi kwa viongozi, ambayo yamkini ikawa sawa lakini haiendani na Pato letu , haiwezekani sisi na baadhi ya mataifa yaliyoendelea tuwe tofauti afu eti viongozi wetu waishi kama kule hatuwezi endelea hata kidogo , Kuna waziri mmoja aliyetenguliwa alisema hawezi kutembelea gari ya kawaida kwenye ziara ataumiza mgongo na kiuno , huku soko la mabibo jijini dar es salaam Kuna watu kutwa kuchwa wanabeba magunia na bado maisha yanaenda,, sijamaanisha kumlazimisha waziri aishi kwa kujibana kwa sababu ya nchi lakini mantinki yangu ni kwamba kama hawezi kufanya kazi kwa maslahi madogo yanayoendana na uwezo wa nchi aache watu wapo watafanya kazi bila lawama na mambo yataenda ,, HIVYO MASLAHI TUNAYOTOA KWA VIONGOZI YAPUNGUZWE YAPELEKWE KWENYE MAMBO YA MSINGI.
3. Wananchi tumekuwa vipofu pia katika kukemea uovu wa viongozi, na hata wanaoona wameshakata tamaa wakidai kuwa watafanya nini sasa ,
Kwa mantinki hiyo viongozi hawatoacha kutujeruhi sisi na pia kutengeneza hatari kwa Tanzania ya baadae.. Watanzania wenzangu, tuamke tufuatilie mwenendo wa nchi , kwa umoja wetu tukemee maovu ya viongozi, lakini tusiweke uadui na tutumie hekima kana kwamba kiongozi akifanya vizuri tuone na vibaya pia tuone pia , sio Ile mwana CCM haoni mabaya na mpinzani kamwe haoni mazuri kitu hii pia inatuumiza sana japo siwezi elezea hapa ..
Ningependa kuandika mengi sana lakini naomba niishie hapa ,,ISHI SANA TANZANIA, ISHI SANA AFRIKA.πͺπͺπͺ