Sio wote wanavaa
Nilihudhuria harusi moja ya wanajeshi tena hawa na wote(Bw.harusi na Bi.harusi) walikuwa wanajeshi lakini walivalia mavazi ya kawaida tu
Mi nadhani wanakwepa gharama ya kununua Suti ya harusi, sio lazima utinge mavazi ya kazini kila sehemu.
Kingine ni sifa kwenye taaluma yao kwan wanawekaga na mbwembwe za saluti kibao na vichekesho ili kuburudisha na kusherehesha waalikwa.
Mwanajeshi anaweza kufunga ndoa ya kijeshi ama ya kawaida, jeshini huwa kuna utaratibu wa kufunga ndoa ya kijeshi na hiyo inautaratibu wake kijeshi, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa gwaride maalum la ndoa, ambalo hufanywa na wanajeshi wenye cheo sawa na muoaji na wote huvaa mavazi ya kijeshi, lakini baadae hubadilisha.... Angalizo kama Raia mwanamume ndo anamuoa mwanajeshi wa kike hakuna utaratibu huo wa ndoa ya kijeshi..
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.