Kwanini wanajeshi wafungapo ndoa huvaa nguo za kijeshi(military uniform) ?

nadhani ni kwasababu shughuli pia huendeshwa na husimamiwa na JESHI hivo ni lazima avae mavazi ya kikazi ili asitofautiane na wenzake
 
Sio wote wanavaa
Nilihudhuria harusi moja ya wanajeshi tena hawa na wote(Bw.harusi na Bi.harusi) walikuwa wanajeshi lakini walivalia mavazi ya kawaida tu
 
Mi nadhani wanakwepa gharama ya kununua Suti ya harusi, sio lazima utinge mavazi ya kazini kila sehemu.
Kingine ni sifa kwenye taaluma yao kwan wanawekaga na mbwembwe za saluti kibao na vichekesho ili kuburudisha na kusherehesha waalikwa.
 
Mwanajeshi anaweza kufunga ndoa ya kijeshi ama ya kawaida, jeshini huwa kuna utaratibu wa kufunga ndoa ya kijeshi na hiyo inautaratibu wake kijeshi, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa gwaride maalum la ndoa, ambalo hufanywa na wanajeshi wenye cheo sawa na muoaji na wote huvaa mavazi ya kijeshi, lakini baadae hubadilisha.... Angalizo kama Raia mwanamume ndo anamuoa mwanajeshi wa kike hakuna utaratibu huo wa ndoa ya kijeshi..
 
Back
Top Bottom