Kwa bahati mbaya, Rais akivunja kipengele cha katiba, kama ilivyo hivi sasa, hawezi kushitakiwa mahakamani. huwezi kumshitaki Rais aliye madarakani na hata akitoka madarakani. hiyo ni kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa. kuna njia nyingi za kukabiliana na changamoto, au kutatua tatizo. kuna njia za kisheria, kuna njia za kisiasa, kuna njia za mabavu - nguvu za dola. Tatizo kubwa ni kwamba hapa Tanzania inaonekana njia za kutumia mabavu ndio zinapendwa zaidi. matatizo mengine yanahitaji "political solution" tu.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, na Sheria ya Vyama vya Siasa, Viongozi wa vyama vya siasa wanawajibika kueleza sera zao kwa wananchi, kutoa mawazo mbadala, na kukosoa mwenendo wa serikali iliyoko madarakani. Katiba inaruhusu hayo kufanyika kupitia vyombo vya habari, au kuongea na vikundi au katika mikutano ya hadhara. kwa hakika, wananchi wote wana uhuru wa kupokea na kutoa habari, kwa mujibu wa katiba. hao uliowataja wanalazimika kuongea kupitia vyombo vya habari, kwa sababu mikutano imepigwa marufuku. Rais hana mamlaka ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa wala maandamano yao. sheria inamruhusu OCD kuzuia mkutano, na kuupangia siku nyingine. hiyo ni kwa ajili ya kulinda usalama tu. unataka tuamini kwamba Tanzania si salama mpaka 2020? Lakini Rais hana mamlaka ya kisheria. na kwa kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, anavunja katiba na sheria. kumshitaki mahakamani haiwezekani. kinachowezekana ni kusisitiza kwamba ni haki ya kikatiba na kisheria kufanya mikutano ya siasa. ndio lengo la UKUTA
nadhani ni kweli hasikulizi ushauri wa washauri wake. kama angefanya hivyo, asingekuwa anafanya baadhi ya mambo, au kutoa baadhi ya kauli: Polisi kuiba matairi ya magari yaliyokamatwa, ili wafanye biashara ya matairi; Polisi kupokea hongo ya elfu tano; kufyatua watoto ili wasome bure, nk. pia hatua alizochukua kwenye ishu ya sukari, wananchi wakapata usumbufu mkubwa; kukataa kuondoa VAT kwenye utalii, nk. Lakini wapinzani awaache waongee kwenye mikutano, atasikia vizuri zaidi. na aache bunge lioneshwe live, atapewa na kupata majina zaidi ya kutumbua, na sifa itakwenda kwake. tatizo liko wapi?