Kwanini wamakonde wanadharauliwa?

Kwanini wamakonde wanadharauliwa?

Zenji wanadharauliwa Wamakunduuchi, kwani maustaadh wao wanaranda na ngazi usiku kucha kupiga chabo. kama ni mwalimu skuli au madrassa basi watoto wote wa kiume si riski tena

kumbe wazenj nao mnadharauliana!!?? na hao maustadhi kwanini wanatabia hio!!??
 
kaka tembea mtu akijatambulisha mmakonde hata kama ni dar ambapo ni saa 6 au 7 wao wanaamin anatoka mbali huko na wanaamin n mshamba kwa kila ktu je huo ni utani wa kikabila?

Weweeee.....!! Mimi ni Mmakonde pure, nimeishi Moshi, Morogoro, Tanga, Dar, Iringa na sasa Mbeya!! Na kwote ninakopita nafahamika sana sababu ya Umakonde, hiyo ni inferiority yako tu. Majina yaote unayojua nimeitwa sana chamaki nchanga, nchumali, mmachinga, chinga na sasa mzee wa gesi upooo???

Kuna ndugu yangu nilinchukua Mtwara yeye alikuwa anapigana mara kwa mara huko Iringa sababu ya inferiority akitaniwa kidogo tu anahisi kadharauliwa, na kama ujuavyo Makonde hakubali kudharauliwa hata kidogo ila sasa nashukuru amechange na anafanya maisha kama kawa. Hali hiyo ndiyo uliyonayo wewe, hizo ni hisia tu na narudia tena kuwa mi nataka uthibitisho 'AINA YA DHARAU' unayoona wanapewa kila siku. Achana na hizo hisia za kuonekana mshamba na nini sijui lete evidence mezani tuichambue bana
 
Na kuna dhana ilikuwepo kuwa wamakonde wanakula nyama za watu.
 
Wanajishuku tu, hakuna anayewadharau, mbona wasukuma wanasakamwa sana? Mara wanapenda msosi, mara washamba huwa wanauziwa bahari na lile daraj la Manzese, mara wao ni kama mbwa mbele ya chatu kwa wanawake weupe. Hawawahi chukulia kama dharau.
 
vipi lile kabila la kukandamiza kutoka kanda ya ziwa, maana sijaona watu washamba kama wale

Acha dharau wewe kanda ya ziwa inaingiaje kwenye topic hii? kwa mtu asie na exposure ya kutembea mikoa mingi Tanzania ndo hufikiria humiliation kwa makabila mengine.
Hata hivyo wasukuma ndio kabila linaloongoza kwa ukarimu ktk nchi hii! wazee wa maguzu masese!
 
Nchi yetu ina makabila mengi sana na kwa uwingi huo unafanya nchi yetu kuvutia.Na inavutia zaidi hasa pale utakapowakuta watu kutoka maeneo mbalimbali wakizungumza kiswahili kwa lafudhi zao.

Lakini kabila la wamakonde wamekuwa wakidharauliwa kila wafikapo maeneo mengine.

Sijajua kwa lipi hasa lafudhi,makosa yao ya kisarufi,hulka zao au nini.Kama lafudhi binafs ya kiluguru,kinyakyusa hata kikurya zinachekesha zipo nyingne.Kama makosa yao ya kisarufi wapemba nao hawana m mimi binafsi kabila langu halina l pia wachaga hawana z,kama ni hulka zinafanana na upwani za umwinyi makabila meng kama wazaramo wanazo hizo.

Kwa sasa mkoa wao unaendelea kwa kasi asilimia 90 ya vitu vnavyohtajika vipo vyuo vya juu,vya kati,mahotel,mkoa wao upo vizur kimpangilio,fukwe ya kuvutia na hata barabara ya kwenda dar haiwetenganish mbal na dar masaa kama 6 au 7 tena kuna root za saa 2,4 na kuendelea.Wazawa wanasoma kwa uchungu.Kwa kweli nilipoenda kwa kazi zangu binafsi nimeshangazwa juu ya stori za uongo juu ya kabila na mkoa wao.
nani anawadharau na kivipi? wacha kuchokonoa mioyo ya watu wewe! shemeji yenu mmakonde ,wale mademu wako juu kule kunako na zile figure zao! shauri zenu niacheni nijilie samaki mchanga ukweni!
 
Dada zetu wamakonde ni wakarimu sana sio vizuri kuwadharau eti kwa sababu wanakula Panya.
 
kihistoria wamakonde wanaonekana ni watu kutoka msumbiji na hata mkoa wa mtwara na lindi yote ilikua sehemu ya msumbiji, huenda hilo inaweza kuwa sababu ya kuadharau wamakonde.
LINDI na MTWARA eeeh,haya elimu haina mwisho.
 
wewe mtoa post una chuki binafsi na wamakonde.....naomba mtuachiee ntwaraa yetuuu ges
 
watu wengi walikuwa hawajawahi kufika mikoa ya kusini kutokana na tatizo la miundombinu lilosababishwa na serikali ya awamu ya kwanza kuitelekeza mikoa hiyo, hivyo walidhani watu wa huko ni waajabu saana. kwa sasa kusini kumefunguka, watu wanaoenda huko ndio wanashangaa kuona kumbe mazingira ni ya kawaida tu kama sehemu nyingine, tena kwa upande wa vijiji, mikoa ya kusini kuna vijiji vinavyoeleweka kuliko sehemu nyingi tu za nchi hii.
 
Kwa sababu wanajidharau we mtu hutaki kusema unatokea Ntwala unategemea nn siku wakikujua ni wa huko, lazima wakudharau na kuona kwenu si lolote kama mwenyeji unakumbia.
 
watoto hupenda sana kuweka 'cha' kwenye 'sa'.., imagine mtu anasema "chamaki" instead of "samaki", au anasema "nchale" instead of "mshale".., yaani unaanza kuhisi kama unaongea na mtoto mdogo anaeanza kujifunza kuongea.., kwa hiyo wanakuwa kama vikatuni fulani hivi.., tatizo ni lafudhi yao imefanana na ya watoto wadogo wasiojua kuongea bado.

Poor u.. Uwezo wako wa fikra uko chin ya wa kondoo.
 
kuna dharau fulani inaambatana na hiyo.......ngoja nikupe mfano
uko mahali unatoa huduma fulani sema Dar
kuna profesa muhaya zaidi ya english kiswahili kigumu sana, mfanyabiashara msukuma anayejulikana au milionea, mfanyabiashara wa madini masai toka mererani na machinga anayeuza bidhaa bila hata frame. Unafikiri ni nani kati ya hawa atahudumiwa, ni kujikomboa ndio kutakupa heshima ktk jamii. Wanaamka kweli soon watakuwa watu na wao.

Wewe raia kwel wa hii nchi au mhamiaji haramu wewe.. Lakin nisikulaum sana mana hapo ndipo ubongo wako ulipokoma kufikiri.
 
Nchi yetu ina makabila mengi sana na kwa uwingi huo unafanya nchi yetu kuvutia.Na inavutia zaidi hasa pale utakapowakuta watu kutoka maeneo mbalimbali wakizungumza kiswahili kwa lafudhi zao.

Lakini kabila la wamakonde wamekuwa wakidharauliwa kila wafikapo maeneo mengine.

Sijajua kwa lipi hasa lafudhi,makosa yao ya kisarufi,hulka zao au nini.Kama lafudhi binafs ya kiluguru,kinyakyusa hata kikurya zinachekesha zipo nyingne.Kama makosa yao ya kisarufi wapemba nao hawana m mimi binafsi kabila langu halina l pia wachaga hawana z,kama ni hulka zinafanana na upwani za umwinyi makabila meng kama wazaramo wanazo hizo.

Kwa sasa mkoa wao unaendelea kwa kasi asilimia 90 ya vitu vnavyohtajika vipo vyuo vya juu,vya kati,mahotel,mkoa wao upo vizur kimpangilio,fukwe ya kuvutia na hata barabara ya kwenda dar haiwetenganish mbal na dar masaa kama 6 au 7 tena kuna root za saa 2,4 na kuendelea.Wazawa wanasoma kwa uchungu.Kwa kweli nilipoenda kwa kazi zangu binafsi nimeshangazwa juu ya stori za uongo juu ya kabila na mkoa wao.

Wamakonde watudharauliwi bali tunataniana na makabila mengi sana hii ni kutokana haiba,historia na mengine mengi tu..Pia suala la kuwa nyuma kimaendeleo hili ni la kihistoria zaid ambapo wakoloni waliyafanya maeneo ya kusini ni kuwa maalumu kwa kuchukua vijana ambao ndo nguvu kazi na kuwapeleka katika mashamba yao huko Arusha,Kilimanjaro,Tanga Morogoro na kadhalika..hakukujengwa miundo mbinu na huduma za jamii. Hivyo kutokana kutaniwa sana na watu wengine we unahisi kuwa ni dharau kitu ambacho si kwel, hii inamaanisha kuwa tuna amani na kila mtu wa kabila lolote.
 
Mbona mi naona kama wamasai ndo wamedharauliwa sana!
Mara utasikia disko kaingia masai!
Mara kasimamisha basi la abiria kuulizia mda!
Wamekufa masai wawili na mtu mmoja!

Hivi Tanzania hii kuna watu wanadharauliwa,kupigwa madongo na kutaniwa kama wamasai???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom