habari ya hapa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 12,788
- 8,755
- Thread starter
- #21
Mkuu bibilia si neno LA MunguNimekuuliza swali, Je, unaamini kuwa Biblia ni neno la Mungu?? Hukujibu ila umenijia na mengine. Sawa tu usijali. Kama nimekuelewa swali lako; Nimefanya nini mpaka niokoke? Dah! Utamuokoaje mtu ambaye hajui hatari inayommeza? Dhambi ni mauti na nadhani hakuna anayeyapenda mauti. Kama umetenda dhambi, tiyari wewe unatembea na mauti. Hivyo unahitaji Mkombozi akuokoe.
Usemi wako ati; Biblia haijawahi kuwa Mungu wala Mungu hajawahi kuwa Biblia. Ni usemi wa hikima kweli kweli. Ila nauliza, Ukisoma noti ya shs 500 (Jero) imeandikwa, FEDHA HALALI KWA MALIPO YA SHS 500. Hivi kile kikaratasi ndio Mahindi sado moja?? Thamani ya kale kakaratasi ni yale maneno yalio andikwa pale. Biblia si Mungu wala haitakaa iwe Mungu ila yale maneno yaliyoandikwa mle ni ya Mungu mwenyewe hivyo ni yeye Mungu anasema nasi. Neno la mtu ndiye mtu mwenyewe. Cheki tupu haina thamani hadi iandikwe neno na sahihi ya mwenye akaunti.
Hayo yalikuwa ni mawazo ya Yohana juu ya Mungu,
Hata Yesu mwenyewe alisema; niaminini Mimi yaani Yesu, mwaminini na Mungu, km haitoshi kuwamini yy basi tuamini kazi alizozifanya
Hakuna pahala kasema tuiamini bibilia km neno LA Mungu