Kwanini wake zetu hawatuamkii asubuhi?

Kwanini wake zetu hawatuamkii asubuhi?

Tanzania kumpa MTU salama ya shikamoo ni heshima kubwa sana
Hata watoto wadogo wanafundishwa kutoa salamu ya shikamoo kwa wakubwa..

Jambo la kushangaza sana ni pale hawa wake zetu ambao wengi tumewazidi umri.,na walikuwa wanatoa salamu za kuamkia b4 kuanza mahusiano.

Ila shikamoo uisha faster mkianza kudate,wapo wanaoendeleza ila wachache sana.

Hapa kwangu nimeuliza kwann haunipi salamu yangu jibu nililopewa ci mchezo..
Ananiambia ukitaka nikuamkie acha kunivua........

Wanamama embu tuambieni kwann lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli yaani unile halafu nikusalimie hapo sasa nikazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu ya Shikamoo ilishapitwa na wakati tangu enzi za utumwa zilipoisha!
Shikamoo maana yake “ niko chini ya miguu yako”
Baada ya utumwa kuisha hiyo salamu haina maana tena,
Lakini sasa jamii imekariri , mtu asipofanya hivyo ataonekana hana adabu!
Salamu zinazokubalika ni zile za kiimani matharan;
1. Asalam alyekum
2. Bwana asifiwe
n.k

Salamu nyingine ni za kawaida kutokana na majina
Mfano asubuhi ;
Umeamkaje? Umeshindaje n.k


Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja
 
Kawaida mwanamume anahitaji utii au heshima kutoka kwa mwanamke. Na mwanamke anahitaji upendo kutoka kwa mwanamume. Hivyo mpe heshima yake mumeo.
Ndiyo maana Neno la Mungu linasema katika Wakolosai 3:18 Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. 19 Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini mkuu kwani kumuamkiaa ndio kumtiii[emoji3][emoji3][emoji3]kwakweli mm shikamoo hapana kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi yameisha, naona unatafuta sababu taratibu
 
Lakini mkuu kwani kumuamkiaa ndio kumtiii[emoji3][emoji3][emoji3]kwakweli mm shikamoo hapana kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuamkia sio kutii bali ni ishara ya kutii au kuheshimu. Na kama vile kununulia zawadi mtu sio kupenda bali ni ishara ya kupenda. Kwani ukimpa shikamoo mumeo utapungukiwa kitu gani? Inahitaji shilingi ngapi? Utachubuka? Majibu yote ni hapana. Lakini naona kuna kitu kilicho ndani yako kinakuzuia, ungekuwa mkristo ningekuambia ujifunze kwa Sara alivyomtii mumewe Ibrahim.
Mpe haki yake mumeo, naye utaona atakavyokupenda zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
amaniii hivi mi nilishagajua haya mambo Tz yameisha kumbe kuna watu bado wanasimamia kwny misingi hii ya kikoloni.

Hivi mke wangu nidai aniamkie kweli.....huyo hatajuwa mke hata sielewi nitakuwa naishi na nani..... kapuya mwenyewe hana mpango kudai shikamoo kwa yule binti sasa wewe kijana mdogo kujitia uzee maana yake nn.

Tuacheni tamaduni za kale
 
Back
Top Bottom