Kwanini wake na waume wa Marais wapewe ulinzi?

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,688
2,000
Mimi sina uzoefu wa uongozi wa kiserikali lakini nikiwa mume mwenye wake wanne nina uzoefu sana na mambo yanavyokwenda majumbani mwetu.

Raisi au mfalme ni mtu mkubwa katika taifa lolote lakini anapoingia chumbani kwake kulala na kujipumzisha na mwenzake anakuwa binadamu wa kawaida sana. Ana mambo mengi sana ya siri yanayompitikia ambayo hayatakiwi kujulikana na mtu yoyote mwengine pamoja na hata wapambe na walinzi wake.

Pamoja na hivyo mume au mke huwa ana nafasi ya kubwa ya kuyajua kwa kuyaona na kuyasikia. Anaweza akayajua kupitia mwenzake anapojifaragua katika baadhi ya mambo kama ilivyo kibinadamu Lakini hata akiwa mtunza siri hodari, bado mwenzake akaweza kuyadukua kwa njia nyingi ikiwemo mawasiliano yake ya kikazi ambayo mwenza huyo atakuwa karibu nayo kuyashuhudia.

Katika hali kama hizo mke au mume wa Rais haifai kumuacha akachanganyika kwenye vijiwe vya kahawa kama ni mume au kwa wasusi wa nywele kama ni mke kwani na yeye lazima baadhi ya vitu vya siri za kiserikali atazibwaga pasipo husika.

Kwa upande mwengine kuachwa mke au mume wa Rais bila ulinzi anaweza akadhuriwa kwa namna fulani kwa makusudi ili wale wanaomchukia raisi wamuumize na ashindwe kutenda kazi za kiserikali kwa umakini.

Wale waliopitia nyanja hizo wanaweza wakachangia pakubwa.
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,410
2,000
Wewe wee weee thubutu yaan mke au mume wa Rais asilindwe???

Mmhhh nakuambia ivi itakua ni patashika nguo kuchanika

Hapatashikika wala kukalika

Unaambiwa Dunia nzima itashangaa sanaaa

Nchi itasimamaaa kwa ujumla


Unaambiwa hata CDF anaweza kupigwa chini


Kwa sababu Mke au Mume wa Rais asipolindwa, Atachepuka sana yaan..nasema uongo ndugu zangu
 

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
31,922
2,000
Wewe wee weee thubutu yaan mke au mume wa Rais asilindwe???

Mmhhh nakuambia ivi itakua ni patashika nguo kuchanika

Hapatashikika wala kukalika

Unaambiwa Dunia nzima itashangaa sanaaa

Nchi itasimamaaa kwa ujumla


Unaambiwa hata CDF anaweza kupigwa chini


Kwa sababu Mke au Mume wa Rais asipolindwa, Atachepuka sana yaan..nasema uongo ndugu zangu
Hapo mwisho umeharibu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom