Kwanini waislamu wote wanawaita waKristo makafiri??

Kwanini waislamu wote wanawaita waKristo makafiri??

Swali hili linakuja baada ya kugundua kuwa asilimia 100% ya waislamu husema kuwa wanamwamini YESU KRISTO ambaye wao wanasema ni Issa bin Maryam lakini wanawaita waKristo makafiri wakati hao waKristo(sisi) msingi wa Imani yao ni YESU KRISTO. Kwa maana hiyo waislamu hudai waKristo(sisi) Wana Imani moja na wao.

Naomba majibu tujifunze
kuna tofauti

Quran imegawa watu makundi matatu kwa kadiri wanavoamuamini Muumba

1.Waumini wanamuamini Muumba na mitume wake .Ambapo wamegawika kwa watu wa kitabu yaani mayahudi na wakristo( manaswara)
kuhusu wakristo Quran 5:82 inasema : Na utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi na waumini ni wale waliosema sisi ni wanaswara

2. Kundi la pili ni wanaopinga uwepo wa Muumba na mitume wake ,hawa huitwa makafiri kwa lugha ya kiarabu,kwa kiswahili wapingaji. Quran 2;6 -7

3.Kundi la tatu hitwa wanafiki. Yaani nje au hadharani wanatangaza wanamuamini Muumba na mitume, Lakini nyuma ya pazia , hawako tayari kutekeleza la Muumba wala maelekezo ya mitume (Aswali,afungi , atoi sadaka n.k kwa makusudi na siyo kwa uvivu au kujsahau) Quran 2: 8-16
 
Back
Top Bottom