Kwanini wahitimu wa vyuo Tanzania ambao hawana ajira wanaona kama walipoteza muda wao kusoma?

Kijana Wa Makamo

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
212
116
Salam wanajamvi. Moja kwa moja kwenye mada, kwa sababu kuna hili jambo ambalo linazidi sana kukithiri nchini Tanzania hasa kwa wahitimu wa shahada ya kwanza. Wahitimu ambao wamepata shahada kwa asilimia kubwa hawana ajira na hii ni kutokana na ukweli kwamba swala la ajira katika nchi zinazo endelea ni changamoto.

Hivyo basi kumekuwa na tabia ya wahitimu wengi kukaa vijiweni au la kugeuka kuwa watu wa kushinda katika vijiwe vya kidigitali (social medias). Je, kuna haja ya kuangalia upya elimu yetu ya juu kwa mapana yake yote?. Hata humu JF kuna wahitimu wanadiriki sema wanajuta muda waliopoteza vyuoni.

Swali, Je! Elimu yetu imeshindwa kuwasaidia hawa wahitimu au ni ignorance yao tu?.

Nawasilisha.
 
Asilimia 99% ya wanachuo wanawaza kusoma ili kuja kuajiriwa, sasa wakimaliza na wakachelewa kupata ajira wanaishia kujikatia tamaa. Kiujumla msomi wa kitanzania ni mjinga wa kawaida sana ambaye alipelekwa shule kujengewa uoga wa maisha.

Elimu yetu ni ya kwenda kulipwa pesa tu, haina mchango wowote katika maisha yetu ya kila siku. Ndio maana tuna watu kama wakina Profesa Lipumba nk.
 
Nimekuelewa vyema sana, nadhani kuna ulazima wa ku refine elimu yetu.
 
Sawa mkuu wamesoma theory, ila mtu anaitwa msomi baada ya kupata shahada ya kwanza. Sasa kama umekuwa msomi na katka jambo la kutumia usomi wako ili kujikwamua inakuwa shida, watu ambao si wasomi wafanyaje?
Tena wasomi SAA hiz ndo bure kabisa MTU kaja ofsini kuomba kazi tunamwambia atuandalie wasifu binafsi anakuna kichwa

acha uongo
 
Asilimia 99% ya wanachuo wanawaza kusoma ili kuja kuajiriwa, sasa wakimaliza na wakachelewa kupata ajira wanaishia kujikatia tamaa. Kiujumla msomi wa kitanzania ni mjinga wa kawaida sana ambaye alipelekwa shule kujengewa uoga wa maisha.

Elimu yetu ni ya kwenda kulipwa pesa tu, haina mchango wowote katika maisha yetu ya kila siku. Ndio maana tuna watu kama wakina Profesa Lipumba nk.
Kama kusoma kungekuwa hakuna impact yeyote katika maisha ya baadae ya mwanafunzi basi hakuna ambae angejishughulisha na shule amini hivyo.
 
60% tumejiajiri kwenye betting..hauhitaji mtaji mkubwa wala mkopo bank..ni kuchambua odds vizuri na kufatilia betting experts wazuri..Tutafanyaje sasa wakati tuna bachelor of procurement and supply implication yake kwenye maisha ya kitaa haina nafasi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahah mkuu nipe tips basi, nataka nijiajiri katika hio sector mkuu
 
Maisha ya sasa jinsi yaliyo unapofikia na kama ikitokezea nafasi ya ajira ikamate kwanza, then utaendelea kusoma ukiwa na ajira yako. Wengi wa wanaosoma huwa hawataki kuacha gape kwenye kusoma kwao kiasi ambacho mtu huwa anapenda asome moja kwa moja kwa lengo kuwa akimaliza ataajiriwa na kupata maendeleo ya haraka haraka. Sasa mabadiliko ya zama nayo pia ni kikwazo.

Jamii Forums mobile app
 
Km waziri anaogopa kuachishwa kazi sababu familia yake itakosa matunzo je mhitimu aliemaliza chuo sasa hv hatawezaje kujiajiri? Hawa viongozi wetu wana miaka mingi serikalini lkn wenyewe hata ujasiliamali mdogo hawawezi itakuwa mhitimu ametoka chuo na deni LA mkopo wa 8m.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfano mtu umesomea uhasibu. Yani kutunza kumbukumbu za mahesabu za mashirika makubwa, unaanzaje kujiajiri? Ni lazima uajiriwe na mashirika makubwa ili uwatunzie kumbukumbu za mahesabu.

Mfano mtu umesomea kutibu watu kwa kutumia vifaa vya kisasa, unawezaje kujiajiri? Ni lazima uajiriwe na hospitali kubwa kubwa yenye vifa tiba ili uweze kutumia ujuzi wako.
Mfano umesomea mambo ya uaskari/ uanajeshi alafu usiajiriwe, hivi ukijiajiri nini kitatokea? Si utaishia kuwa jambazi sugu?

Elimu inayotolewa ni ya kukuwezeka 'ku function well in an organization/ institution and not as an indivitual...
 
Back
Top Bottom