Kwanini wafanyakazi hatuna TIN numbers?

By the way unatumia payroll number ya mwajiri wako... Yeye ndiye anayekusanya kodi yenu na kuipeleka TRA. By the way kama huna TIN number mpaka leo, you are the poorest of the poor! Hivi ina maana hata leseni ya kuendesha gari au boda boda hauna? Maana hiyo tu kuipata lazima uwe na TIN. Jiongeze bhana 2016 usitie aibu!
 
Wafanyakazi wanaruhusiwa kuwa na TIN namba, nenda TRA ukajisajili. Swala la kwamba unalipa kwa kupitia mwajiri au kwa TIN ya mwajiri sio muhimu. kwa mfano ukitaka kuuza/kununua chombo chako cha usafiri unatakiwa kuambatanisha TIN number utafanyaje? Pia kumbuka wafanyakazi hawazuiwi kufanya biashara binafsi. Nimeona pia baadhi ya watumishi wa TRA wakiwa na TIN number.
Mkuu usemacho ni kweli kabisa. Mimi nilikuwa mfanyakazi wa serikali mwaka 2012 na nilibahatika kununua chombo changu cha usafiri kutoka kwa mtu. Wakati nataka kufanya transfer ya umiliki wa hilo chombo hicho, TRA walinipatia TIN namba ambayo waliingiza kwenye kadi yangu mpya. Kwa hiyo TIN ni bure kabisa kama unataka kuwa nayo!
 
Kwanza napinga kabisa PAYE ni kodi kandamizi haina tofauti na kodi ya kichwa na haistahili kuwepo....Kama serikali inahitaji fedha kwa ajili ya maendeleo basi wakishakata PAYE kila ingizo la kodi liwekwe kwenye TIN ya mlipaji na serikali imrejeshee mlipaji wa PAYE fedha yake anapostaafu au kufikia umri wa kustaafu....serikali isipore fedha za wananchi wake.
 
TIN namba anakuwa nayo mwajiri wako ambaye ndiye mwenye jukumu la kupeleka kodi zote za wafanyakazi walioko chini yake

Kwa nn inafanyika hivyo?
Naamini ni kutoa urahisi wa usimamizi na ufuatiliaji wa kodi husika hasa kwa kuzingatia kuwa anaewasilisha kodi ni Mwajiri.

Chukulia mfano una wafanyakazi 200 kila mmoja akiwa na TIN namba yake maana yake italazimika kodi kulipwa kwa namba hizo....inaweza kuwa kwa namna mbili....moja ni wewe mwenyewe kwenda kulipa TRA mwenyewe au mwajiri kuwa na sheet ambayo itakuwa na jina, TIN namba na PAYE ya kila mfanyakazi jambo ambalo ni usumbufu mkubwa na huweka ugumu wa ufuatiliaji

Kwa watu wa TRA ni rahisi kwao kufuatilia kwani wakitaka kujua nidhamu ya uwasilishaji wanaweza kuja kwenye shirika/ofisi na ku-sample baadhi ya salary slip na kuangalia kama kilochowalishwa TRA kwa kila mfanyakazi ni sawa na kilichopo kwenye makato yao ya PAYE kwenye salary slip

Hivyo binafsi naona itakuwa na ugumu wa administration ya PAYE kama kila mfanyakazi atakuwa na TIN yake

Nionavyo mimi lakini and I stand to be corrected

Mbona Contributions za pesnion funds, NSSF,PSPF, LAPF Etc, zinaenda zikiwa na Member identification?? na ndo inakuwa rahis zaid wao kufuatilia

Nadhan suala hapa niku account mtu aliyelipa Kodi, ziyo anaecollect kwa niaba ya TRA. hasa kwa hili la PAYE na hata kwa Withholding taxes. TRA wangeweka mfumo ambayo unamtambua yule aliye lipa na si yule aliye kusanya, Jambo hilimlinawezekana hata kwa VAT ( Kwa msaada wa Vitambulisho vya Taifa) but huko wangesubir kwanza had miaka kadhaa ipite ila huku kwenye PAYE na Withholding taxes za Consultants etc etc, wangeanza tu hata sasa. Sababu kuna waajiri wanakwepa Kodi Kipumbavu kabisa
 
Wafanyakazi wanaruhusiwa kuwa na TIN namba, nenda TRA ukajisajili. Swala la kwamba unalipa kwa kupitia mwajiri au kwa TIN ya mwajiri sio muhimu. kwa mfano ukitaka kuuza/kununua chombo chako cha usafiri unatakiwa kuambatanisha TIN number utafanyaje? Pia kumbuka wafanyakazi hawazuiwi kufanya biashara binafsi. Nimeona pia baadhi ya watumishi wa TRA wakiwa na TIN number.

Kinachoongelewa hapa si kuruhusiwa au kutoruhusiwa! Kila mtu anajua kuwa wafanyakazi wanaruhusiwa na kuwa TIN number ni Bure.

Suala ni kuwa kwa nini TIN number ya mfanyakaz haitakiwi wakati anapolipa PAYE yake?? Leo hii umetoka Kampuni xz ,ukaenda kampuni yz . Je tukikuuliza jumla ya kodi ulizolipa kampuni XZ na YZ utajua ni kiasi gan?? Ishu ni mlipa kodi (Mfanyakzi) Kutambuliwa kodi yake anayolipa yeye kama yeye (PAYE) na Siyo kwa kodi anazolipa kwa occupation nyingine.
 
Labda kama Wafanyakazi wa Sekta binafsi lakini kama wa Umma ninyi hamlipi kodi ila ni balance ya fair in Taxation. Wafanyakazi wa umma hamzalishi bali mnatoa huduma. Fikiria 12% ya kodi yako itakusanya mara ngapi ili iweze hata kukulipa mshahara wa mwezi mmoja? Mfano 12% *500,000=60,000. Ili kodi yako iweze kukulipa mshahara wa mwezi mmoja inatakiwa ikusanywe kwa miezi 8.
Wafanyakazi wa umma msilalamike kwamba nyinyi ndio mnaolipa sana kodi bali imewekwa kubalance tu kwamba kila mtu analipa kodi lakini in reality hakuna chochote sawa sawa na kuwapangia tu kiasi chenu mnacholipwa baada ya kukatwa kodi mkabakia hapo hapo.
 
TIN namba anakuwa nayo mwajiri wako ambaye ndiye mwenye jukumu la kupeleka kodi zote za wafanyakazi walioko chini yake

Kwa nn inafanyika hivyo?
Naamini ni kutoa urahisi wa usimamizi na ufuatiliaji wa kodi husika hasa kwa kuzingatia kuwa anaewasilisha kodi ni Mwajiri.

Chukulia mfano una wafanyakazi 200 kila mmoja akiwa na TIN namba yake maana yake italazimika kodi kulipwa kwa namba hizo....inaweza kuwa kwa namna mbili....moja ni wewe mwenyewe kwenda kulipa TRA mwenyewe au mwajiri kuwa na sheet ambayo itakuwa na jina, TIN namba na PAYE ya kila mfanyakazi jambo ambalo ni usumbufu mkubwa na huweka ugumu wa ufuatiliaji

Kwa watu wa TRA ni rahisi kwao kufuatilia kwani wakitaka kujua nidhamu ya uwasilishaji wanaweza kuja kwenye shirika/ofisi na ku-sample baadhi ya salary slip na kuangalia kama kilochowalishwa TRA kwa kila mfanyakazi ni sawa na kilichopo kwenye makato yao ya PAYE kwenye salary slip

Hivyo binafsi naona itakuwa na ugumu wa administration ya PAYE kama kila mfanyakazi atakuwa na TIN yake

Nionavyo mimi lakini and I stand to be corrected

Hiyo kauli ya watu wazembe wanaopenda shortcuts. Kutumia TIN ya mwajiri kunaweka mianya ya mwajili kukwepa kuwasilisha baadhi ya kodi na ni kumnyima mfanyakazi haki yake ya kutambulika kama mlipa kodi. Mbona nchi nyingine (hata Kenya tu hapa) kila mlipa kodi (including wafanyakazi) anakuwa na namba yake ya kumtambulisha kama mlipa kodi?
 
Hapa suala ni kwamba anayetambulika kama mlipa kodi si mfanyakazi bali mwajiri. Hii ni kutokana na kwamba PAYE inalipwa na mwajiri baada ya kukata kodi kutoka kwa mshahara wa mfanyakazi. Ndiyo sababu endapo kuna default, anayeulizwa ni mwajiri na si mfanyakazi. Lakini hii haimzuii mfanyakazi kuomba TIN kwa madhumuni mengine ambayo hayatokani na mshahara wake.
 
Nashangazwa na hii mamlaka ya mapato TRA.

Wafanyakazi ni walipa kodi wazuri na hawana pa kukwepea lakini maajabu ni kuwa hawana hata namba ya kuwatambua kama wao nao ni walipa kodi yaani TIN namba.

Wazo zuri sana mkuu.naamini kwa staili hii ile mishahara yetu hewa itatoweka
 
Kutumia TIN ya mwajiri kulipia PAYE, kumefanya waajiri wengi kutolipa kodi zao binafsi. Mtu anapeleka PAYE, naye anatamba ni mlipa kodi tena anademand hata kuheshimiwa na kualikwa kwenye seminar. Mlipa kodi Halisi hata system haimtambui na wala seminar haalikwi
 
By the way unatumia payroll number ya mwajiri wako... Yeye ndiye anayekusanya kodi yenu na kuipeleka TRA. By the way kama huna TIN number mpaka leo, you are the poorest of the poor! Hivi ina maana hata leseni ya kuendesha gari au boda boda hauna? Maana hiyo tu kuipata lazima uwe na TIN. Jiongeze bhana 2016 usitie aibu!
nadhani mkuu hujanipata vema,tin namba mimi kama mimi ninayo kwa kuwa nina leseni kama ulivyosema,maana yangu ilikuwa ikiwezekana wale ambao tayari wana tin namba walizopata kwa ajili ya shughuli zao binafsi na wakati huo huo ni wafanyakazi wawasilishe namba zao kwa mwajiri ili zitumike kuingiza kodi wanayokatwa na si kutumia namba ya mwajiri,na yule ambaye bahati mbaya hana basi apewe tin yake ili kodi yake ipitie kwenye namba yake na si namba ya mwajiri ili mwisho wa siku ijulikane mfanyakazi binafsi amechangia kiasi gani kwenye pato la taifa.
 
Mkuu usemacho ni kweli kabisa. Mimi nilikuwa mfanyakazi wa serikali mwaka 2012 na nilibahatika kununua chombo changu cha usafiri kutoka kwa mtu. Wakati nataka kufanya transfer ya umiliki wa hilo chombo hicho, TRA walinipatia TIN namba ambayo waliingiza kwenye kadi yangu mpya. Kwa hiyo TIN ni bure kabisa kama unataka kuwa nayo!
kuwa na tin namba nio jambo moja na kutumika (kujaziwa ni jambo jingine)wengi wanazo zao binafsi ,ilitakiwa ile kodi ninayokatwa kila mwezi ipitie kwenye tin yangu
 
Sikubaliani na wewe, hii inachangia wizi, unapokuwa na wafanyakazi wengi unaweza kupeleka record ya uongo lakini kila mmoja akiwa na tin number yake huwezi kudanganya.

kwa mfumo wa kicompyuta haiwezi kuwa ni usumbufu, kwani tra wanakuwa na majina na tin namba za wafanyakazi wa kampuni fulani ndani ya database moja , na technologia kwa sasa mwajiri anauwezo wa kufanya malipo online bila usumbufu kwa kubofya tu.

Zipo ofisi nyingi najua wanapeleka record za uongo na wafanyakazi hawafuatilii hili kwakuwa haliwahusu wao wanavimba na makato ya mafao yo tu,

Well said Mkuu hii ingesaidia kudhibiti wizi, maana kama mfanya kazi hana TIN number angelalamika TRA na TRA waweke mfumo w akila mtu kuona kuwa amechangi kiais gani kwa mwaka.
 
Mi naona kuna kitu hakipo sawa,kuna haja ya mlipa kodi kutambuliwa ni nani ili kuweka kumbukumbu sawa,kusema ni usumbufu wa waandaaji kuandika namba hili linaweza kuwa usumbufu mwanzo likisha anza litakuwa halina huo usumbufu. Kama walivyosema waliotangulia kusema mifuko ya Jamii LAPF,GEPF,NSSF,PSPF na NHIF pamoja na Benki kila mfanyakazi ana namba yake ya uanachama na namba ya akaunti.
 
TIN NUMBER NI BURE HAIUZWI...jipatie TIN number katika ofisi za karibu za TRA
Swali lake sio kuwa na TIN bure tu. Ni kuwa na TIN ambayo itatumika kukuidentify hata ukihama employers unaendelea kutambulika ni the same person analipa hiyo kodi. Coz majina huwa yanafanana ila TIN ni unique
 
Vipi kuhusu mishahara na michango ya pension, mbona wanaweza kuweka kwenye akaunti ya kila mwajiriwa? Kwa nini kodi ishindikane?
Meonaee. Hii sababu ya kusema kua ukiandka TIN no. ya mfanyakazi m1 m1 ni usumbufu, sasa hapa ndo jipu lnapoanza kukua.
 
Swali lake sio kuwa na TIN bure tu. Ni kuwa na TIN ambayo itatumika kukuidentify hata ukihama employers unaendelea kutambulika ni the same person analipa hiyo kodi. Coz majina huwa yanafanana ila TIN ni unique
Naona process zimeanza kila mfanyakazi kuwa na tin,

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom