Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,525
- 22,019
Wanadanganya watu kwa kweliNi kwa sababu moyo wao uko kwenye pesa. Kuna mama mmoja nilikuwa nimepanga naye ndani ya ukuta mmoja (wao - yeye na mumewe - wakiwa na nyumba na mimi na mke wangu nyumba ingine). Baadaye walifarakana, lakini waliendelea kuishi nyumba moja. Maisha yalipoanza kuwa magumu zaidi, huyo mama alitembelewa na ndugu au rafiki yake mwenye pesa na wakaanza mpango wa kuanzisha kanisa. Kama maandalizi walikuwa wakiwaalika watu kuja kuombewa kwenye hiyo nyumba yao, ila mumewe alikuwa akisema waziwazi kuwa "ni utapeli mtupu".
Hata mimi nilijua yule mama ni tapeli kwa sababu hakuwa na maadili ya dini hata kidogo. Ila walioweza kudanganywa naye walikuwa wakifika kwa ajili ya kuombewa! Mradi huu uliposhindikana, alijiunga na NGO fulani ambayo ilikuwa interested mashoga. Hivyo, kazi yake ilikuwa kuwakusanya vijana wenye mwelekeo huo na kuongea nao (sijui alikuwa akiwaambia nini), ila siku moja nilimsikia akimwambia rafiki yake naye afike kwenye mkutano wao aone mikakati yao, akidai ile NGO yao "ina hela chafu" kwa maana kwamba ziko njenje.
Wakati huo ndio tulikuwa kwenye mchakato wa maoni ya Katiba Mpya 2013 na hilo kundi lao nao walikuwa wakipigania haki za mashoga. Baada ya kuhama hapo tulipokuwa tukikaa (maana mwenye nyumba aliiuza) sijui alienda wapi na anafanya nini muda huu. Kwa hiyo, hawa watu wanaoweka pesa mbele ina maana wameanzisha kanisa kwa ajili hiyo na wanafaulu sana kuwadanganya watu wanaojiunga nao. Shame upon them!
Na usipotoa sadaka hata kuombewa huombewiWanahubiri kile unachopenda kukisikia ili utoe sadaka nyingi ambapo ndo ada yako pale kansan
Pesa huvunja mabonde na milima, lkn ni kweli ukiwa nayo hata mapepo hayakugusi?Mhubiri 10:19 NEN
Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, nao mvinyo hufurahisha maisha, lakini fedha ni jawabu la mambo yote.
3 Yoh 1:2 SUV
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Wenye kupenda pesa, wasio tii wazazi wao, hii namba imeongezeka maana wanachinja wazazi wao kama kukuDalili mojawapo ya siku za mwisho, yesu alishasema yote
Ndio ivyo mkuu, huwezi kuta mtu anapesa.. alafu awe na mapepo haipogo hiyoo πππPesa huvunja mabonde na milima, lkn ni kweli ukiwa nayo hata mapepo hayakugusi?
Kuanzisha kanisa ni fursa ya kupata hela πKuwa fursa upate fursa π
Kuanzisha kanisa ni fursa ya kupata hela π
Unataka kusema wenye mapepo wote hawana hela?Ndio ivyo mkuu, huwezi kuta mtu anapesa.. alafu awe na mapepo haipogo hiyoo πππ
wana hela za kula mkuu, kuwa na gari moja au tatu, na nyumba.. nazunguzmzia serious money.. alafu hata ukiwa na pesa standard pepo anatoka kimya kimyaaa bwanasheeee.. hatoki kwa mafujooo πππUnataka kusema wenye mapepo wote hawana hela?
Shetani anakuona bwanashee
Hatari sanaKwasababu dini ni utawala na utawala wa Kwanza unaanzia kwenye njaa ya akili yako!
Njaa ya akili zipo nyingi aidha ni ujinga ama ni matamanio yako, baadae inakupeleka katika utumwa.
Social engineering.
Halafu wenye hela wote wanapenda sana kula kitimoto, Yesu aliyaamuru mapepo yaingie kwa wale nguruwe wala hakujishughulisha kuyatoa kwa hao nguruwe, hivyo ukila kitimoto mapepo yanakuhusu.wana hela za kula mkuu, kuwa na gari moja au tatu, na nyumba.. nazunguzmzia serious money.. alafu hata ukiwa na pesa standard pepo anatoka kimya kimyaaa bwanasheeee.. hatoki kwa mafujooo πππ
Huyu ni mchungaji??? labda wa mbuziShalom wapendwa, nataka kujua kuhusu hawa Wachungaji wa michongo inakuwaje wajikite kuhubiri mafanikio ya pesa na mali na sio mafanikio ya kiroho.
Leo hii vijana wengi wamekimbilia kuanzisha makanisa huku wakijiita mitume, manabii, maaskofu nk lakini nimejaribu kusikiliza mafundisho yao yapo kinyume na ukweli wa kibiblia yaani hawajui kuichambua Biblia kama neno la Mungu lisilo na ubaguzi ktk kumhudumia muhitaji.
kuna baadhi ya makanisa haya ya Wachungaji wa michongo ni wabaguzi wakubwa wanaotenga hadi viti maalum kwa watu maalum (VIP)
Hapo tusemeje kuhusu Mungu maana Mungu sio wa kubagua bali huwahudumia wote wenye mali na wasio na mali.
Kwanini Wachungaji wa michongo huhubiri pesa zaidi kuliko mafanikio ya kiroho?
View attachment 2079225