Thubutu, hilo ni eneo ambalo Wabunge wote bila kujali vyama vyao huwa wanaungana, Hoja ya vipato vya wabunge huwa inanifanya niyasahau mapungufu yote ya Zitto Kabwe, maake aliwahi kushauri kuna baadhi ya posho zitolewe, Posho tu za mbunge zinafikia 40m kwa mwaka, hapo bila mshahara huwa nasikia mbunge unapokea wastani wa 7m hadi 11m kwa Mwezi hapo ni mshahara, marupurupu, anafanya kazi miaka 5 akistaafu anapewa kiinua Mgongo 230m.
Mwalimu analipwa 900k, anafanya kazi miaka 35 anapata pensheni Mil 100 - 150, Siasa ni uwekezaji unaolipa sana Tanzania, hapo mtu akiwa Waziri ana mshahara wa Mbunge na Waziri, hanunui umeme, halipi maji, halipi nauli, chakula hajui bei yake