Kwanini wabunge hawagomei vikao?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Unafahamu, huwa najiuliza mbona wabunge hawajawahi kugoma kwenda Dodoma? Ukiongea na waheshimiwa Wabunge, wanalia njaa pamoja na posho za kila siku hiku wakitimiza wajibu wao. Vikao vya Bunge ni sehemu ya wajibu wao lakini wanapokaa pale, fedha haikosekani wala bajeti yao huwa haipungui ili wakopwe muda wao wa kukaa Dodoma.

Sasa kwanini fani zingine kama walimu, madaktari, maafisa kilimo wao wanakopwa na hawatakiwi kugoma? wakitumia njia za kuandika barua kudai haki zao hawajibiwi, Wakigoma.. serikali ikiahidi chochote haitekelezi; wakigoma tena, kiongozi anaulimbokwa!

Nawashauri wabunge kama kweli kitendo cha kutekwa, kuteswa, kupigwa kwa jaribio la kumwua dr. Ulimboka kimewaudhi, nao wagome kuingia bngeni hapo kesho.

Quality
 
Back
Top Bottom