Kwanini Waajiri wengi huogopa kuajiri Watu ambao huhisi ni Knowledgeable na Intelligent kuliko wao?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Je ni Kosa la Jinai, Kiueledi na la Kitaaluma kwa Waajiri kuwaajiri Watu ambao labda wanawahisi ni Knowledgeable na Intelligent pengine kuliko wao au labda kwa kusikia tu sifa zao kutoka kwa Waajiri wao wa mwanzo?

Nini kinapelekea Watu walio knowledgeable na Intelligent kuogopeka mno na Waajiri / Wamiliki wa Makampuni au Mabosi?

Nawasilisha.
 
I think they are scared of the costs of paying these people, and that they can not last longer in the organisation if you are paying them little. Every organisation will prefer cheap intelligent people.
 
Hii itakuwa Afrika lakini kwa nchi za ulaya ni tofauti sana.Sababu ili kampuni ikuwe inahitaji talent and skills. Ila sijajua unaongelea kampuni za wapi??
 
Wanaogopa kwa sababu ya hofu na IQ zao zitafunikwa but kwa malegend km cc tunaajiri wenye knowledge (ht km ni ya mtaa) cz tuko vixur and proud kuongoza vichwa....
Knowledge inakaa kichwani cjui km ww maybe unawaongelea [HASHTAG]#Mabashite[/HASHTAG] wenye elimu ya vyeti......
 
Kwanini hao intelligent beings wanaenda ajiriwa na watu ambao hawana intelligence sawa na wao
 
Je ni Kosa la Jinai, Kiueledi na la Kitaaluma kwa Waajiri kuwaajiri Watu ambao labda wanawahisi ni Knowledgeable na Intelligent pengine kuliko wao au labda kwa kusikia tu sifa zao kutoka kwa Waajiri wao wa mwanzo?

Nini kinapelekea Watu walio knowledgeable na Intelligent kuogopeka mno na Waajiri / Wamiliki wa Makampuni au Mabosi?

Nawasilisha.
hapana hapo sikubaliani na wewe, waajiri wanataka mtu mwenye ueledi na taaluma, tatizo ni wale wanaozunguka mabosi ndio shida, wakishaona cv za jamaa ni hatari, yaani wanampiga juu juu wakijua kwamba akija jamaa pale wao lazima washushwe vyeo na jamaa atakuwa juu yao, mifano hai ninayo
 
Ni kwasababu zifuatazo :
1. Mtu mwenye CV nzito na experience ya kutosha automatically lazima atadai mshahara mkubwa na posho nyingi.
2. Ni ngumu sana kumwelekeza kazi mtu ambae ana uwezo pengine kukuzidi hata wewe bosi wa kitengo.
3. Watu wenye uwezo mkubwa mara nyingi huwa hawatulii sehemu moja kwa muda mrefu. They always prefer to seek greener and greener pastures.
4. Mabosi wengi huwa hawapendi dharau kutoka kwa watu walio chini yao kicheo.
5. Kuna raha na ufahari fulani bosi anapata ikiwa anaombwaombwa maelekezo na wafanyakazi wake. Haitakuwa hivyo kama akiajiri vichwa much knows.
5. Hofu ya kupokwa au kushushwa cheo kutokana na kuzidiwa sifa na uzoefu na hao wafanyakazi wapya.

Ila hayo mambo yalikuwepo sana zamani. Siku hizi makampuni mengi yanaajiri wafanyakazi mahiri tu ili kuongeza ufanisi na ushindani katika soko la biashara.
 
Ni kweli wenye akili wanaogopwa. Mabashite ndiyo yanang'ang'aniwa hata kama ni zero form IV, maana ni kama mbwa tu. Ukimwambia "kamata yule" anakimbia kama mwehu hata kama anamkamata mama mkwe wake!
 
Ni kitu cha kawaida kibinadamu mkuu! Wanalinda nafasi zao... Wakiajili mtu knowledgeable sana wanaweza wapindua katika ofisi.

Ni rahisi kumcontrol mtu inferior kwako...
"Don't hire a person you can't fire"
 
Back
Top Bottom