Sababu zako ni nyepesi Sana,kikubwa ni Afrika inazalisha isivyotumia na inatumia isivyozalisha haiwezi kuendelea.
Kuhusu hicho kisa cha mtu kutoka hapa na kwenda sehemu nyingine kupata huduma,hii sio kwa waafrika peke yao.
Hata wazungu.
Kule Zenj mahotel Mengi ya kitalii yanamirikiwa na wazungu,wazungu Hawa wakitaka huduma kama za matengenezo madogo ya ujenzi, umeme, thamani, hawazitafuti kutoka kwa waafrika wa Zenj, watatafuta mzungu mwenzao awape hiyo huduma ata kama yupo nje ya nchi.
Kingine mtoto wa Kiafrika anazaliwa kwenye mazingira yasio na fulsa,Wanaijeria wanaenda South Afrika,wakifika wanaanzisha biashara na wanafanikiwa sana.
Sababu za kutokufanikiwa Afrika ni nyingi na zinarofautiana kila sehemu.
Rushwa, Siasa mbovu, Nigeria inazalisha mafuta lakini ndani ya nchi mafuta ni gharama kubwa!!!mafuta ya Rwanda yanapita Bandari ya Dar, lakini bei ya mafuta Rwanda ni ndogo ukilinganisha na Kule Dar.