Kwanini vyombo vyetu vya dola vinavunja ibara ya ya 14 na ibara ya 20 ya katiba ya

ALEX PETER

Senior Member
Jan 17, 2012
117
23
ibara ya 14 ya katiba inasema kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria.
Ibara ya 20 ya katiba ya jamhuri ya muungano inasema kila mtu anastahili kuwa huru,bila kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine,kutoa mawazo hadharani.

Kwanini polisi wanaua raia wasiokuwa na hatia eti kisa wanadai haki yao ya msingi kikatiba,kwanini polisi wetu hawachukuliwi hatua kwa vitendo vyao viovu juu ya wananchi?
kwanini vyombo vyetu vya dora vinatumikia upande mmoja wa chama tawala?

mbona uvccm arusha waliandamana bila kuwajulisha polisi lakini hawakuchukuliwa hatua kwanini vikifanya hvo vyama vya upinzani na wananchi inakuwa nongwa?

Kwasababu katiba haijatungwa na watanzania,kama unataka mabadiriko ya ukweli shiriki kikamilifu wewe pamoja na marafiki ndugu zako ktk mchakato wa kupata katiba mpya!
 
Kwasababu katiba haijatungwa na watanzania,kama unataka mabadiriko ya ukweli shiriki kikamilifu wewe pamoja na marafiki ndugu zako ktk mchakato wa kupata katiba mpya!

kwann basi wasiitekeleze hiyo iliyopo maana ndo inayo watambua wao kama vyombo vya ulinzi
 
Tumia kifungu hicho kuwashitaki mahakamani kama unaona wana kosa. Tafsiri za sheria ziko nyingi unaweza kukuta kuna kifungu kingine kinawalinda kwa tukio hilohilo.
 
Tumia kifungu hicho kuwashitaki mahakamani kama unaona wana kosa. Tafsiri za sheria ziko nyingi unaweza kukuta kuna kifungu kingine kinawalinda kwa tukio hilohilo.

Umeona eheh,ndio maana nikamwambia hatujaitunga sisi watanzania.
 
sheria inapiga kotekote na hutafusiriwa mahakamani kuona ni nani anasitahiri kulindwa na sheria. kunyofoa kipengere kimoja tu sivyo ndivyo kwenye sheria.
 
Umeona eheh,ndio maana nikamwambia hatujaitunga sisi watanzania.

Ni katiba zote duniani hatunyofoi kipengere kimoja tu na kumpa adhabu mwingine. Tukio ndio linatoa kinga na adhabu kwa mwingine.

Kuna sehemu nyingine kwenye katiba hiyo hiyo inamlinda askari polisi kulingana na tukio kama ataona maisha yake yako hatarini.
 
Back
Top Bottom