Kumteua Omary Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ni kinyume na Ibara 74(14) na (15)(c) ya Katiba ya Tanzania

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Jana tarehe 29/06/2023 Rais Samia amemteua Balozi Omary Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa NEC wakati kiongozi huyo alishawahi kushika nafasi ya Katibu Uenezi ndani ya CCM. Nimepita mtandaoni nikaona malalamiko ya wadau kuwa katiba imevunjwa. Hivyo katika uzi huu nimeona nilete hivyo vifungu tuvisome pamoja.

Ibara ndogo ya (14),
Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Ibara ndogo ya (15),

Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya zote na Majimbo ya Uchaguzi
 
Binafsi kama ungeweka kadi yake ya uanachama ambao ni hai mpaka sasa, ningekuelewa.

Kusema kuwa aliwahi kushika nafafasi ya katibu uenezi ndani ya CCM, hakutoshi kuonyesha kuwa katiba imevunjwa.

Unajuwaje kama kwa sasa siyo mwanachama wa chama chochote?

Katiba haikatazi mtu aliyewahi kuwa mwanachama lakini kwa sasa siyo mwanachama kushika nafasi hiyo.
 
Tuliambiwa lini kwamba Mapuri amejitoa uwanachama wa CCM. Kama alikua katibu wa CCM ni sahihi kasa kusema huyu ni mwanachama wa chama hicho.

Kimsingi uchaguzi Tanzania ni kama maigizo. Rasi watanzania anamalaka kubwa sana.

Sijui kwanini Nyerere alituachia katiba kama hii ambayo ifaa kipindi chake lakini baada ya kuondoka angehakikisha Tanzania inapata katiba mpya.

Nchii hii sio mali ya kikundi kidogo cha CCM ni mali ya kila Mtazania.

Raisi anteua watu hata hawajui.

Nadhani Tanzania tunahitaji Mfumo mpya wa uongozi na utawala. Kuongozwa na mtu mmoja (Rais) bila check and balance ni hatari sana kwa ustawi wa taifa letu.

Raisi wetu ni Mungu Mtu hakuna anae kohoa mbele yake. Sio bunge (sispika) wala Mahakama inaweza sema kitu. huu uraisi wa kifalme umepitwa na wakati. Raisi akiwa mjinga nauza nchi wote tunaingia chaka. Enough is enough .
 
Jana tarehe 29/06/2023 Rais Samia amemteua Balozi Omary Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa NEC wakati kiongozi huyo alishawahi kushika nafasi ya Katibu Uenezi ndani ya CCM. Nimepita mtandaoni nikaona malalamiko ya wadau kuwa katiba imevunjwa. Hivyo katika uzi huu nimeona nilete hivyo vifungu tuvisome pamoja.

Ibara ndogo ya (14),
Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Ibara ndogo ya (15),

Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya zote na Majimbo ya Uchaguzi
Mbona haueleweki.
 
Binafsi kama ungeweka kadi yake ya uanachama ambao ni hai mpaka sasa, ningekuelewa..!! Kusema kuwa aliwahi kushika nafafasi ya katibu uenezi ndani ya CCM, hakutoshi kuonyesha kuwa katiba imevunjwa. Unajuwaje kama kwa sasa siyo mwanachama wa chama chochote..??? Katiba haikatazi mtu aliyewahi kuwa mwanachama lakini kwa sasa siyo mwanachama kushika nafasi hiyo..!!
Hakuna mwana CCM anayeachana na hicho chama, hata kama atakosa teuzi. Sababu anaamini ipo siku ulaji utamrudia. Mapuri ni mfano, wapo wengi waliokaa benchi kitambo lakini baadae wakarudi, tena kwa kasi kubwa.
 
Watanzania Kwa kulalamika hatujambo wengi wetu wanafiki tu Wacha tuliwe Ili tupate akili.
Mwaka 2020 mahakama rufaa ilisema wakurugenzi wakati wa uchaguzi Huwa wamekula viapo vya kutokuwa na chama hivo wangelistahili kusimamia uchaguzi mkuu.
Ni ubabaishaji mkubwa Kwa hili na ndo maana tunataka katiba mpya
 
Jana tarehe 29/06/2023 Rais Samia amemteua Balozi Omary Ramadhani Mapuri kuwa Mjumbe wa NEC wakati kiongozi huyo alishawahi kushika nafasi ya Katibu Uenezi ndani ya CCM. Nimepita mtandaoni nikaona malalamiko ya wadau kuwa katiba imevunjwa. Hivyo katika uzi huu nimeona nilete hivyo vifungu tuvisome pamoja.

Ibara ndogo ya (14),
Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Ibara ndogo ya (15),

Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya zote na Majimbo ya Uchaguzi
Tuwekee uthibitisho hapa kama huna basi hizi nazo ni propaganda tu
 
Hoja yako haina mashiko bro sababu huyo Kmary Mapuri alishahudumu kwenye nafasi hiyo na Rais amepewa mamlaka kisheria kuwa anaweza akamteuwa tena mjumbe kwa hawamu ingine akiona inafaa mjumbe huyo kuendelea kwenye nafasi hiyo, sasa wewe kazi kuchonga ngenga tu ukiambiwa uonyeshe hiyo kadi yake CCM utaanza apechealolo kama hayawani so achana na propaganda za maji taka tafuta hoja zenye mashiko na evidence juu ndiyo waelevu watakuelewa bila hivyo nenda Instagram na Facebook ukapost picha za show off.
 
Mtu alishakuwa katibu mwenezi WA CCM halafu watu wanaulizia Kadi yake, hi7 inaonyesha elimu yetu Ina mapungufu makubwa na imefanywa makusudi ili ccm iendelee kutawala,.
Hapa kinachotakiwa ni kufungua kesi na kupinga uteuzi wake kwani umevunja&óii
 
Binafsi sina sijui kama ni mwanachama au siyo mwanachama. Sasa mtoa hoja, kwa vile amejikita kwenye kusema kuwa katiba imevunjwa, angeweka tu kadi ya uanachama wa mteuliwa. Tukiishia kudhani tu tutakuwa hatutendi sawa
Acha ubishi kihinja. Wewe mjenga hoja za uelewa Muda wote, lkn Leo wataka Tu kubishana. Huijui kama huyu alikuwa kiongozi WA chama, tena mkubwa Tu. Lini imetangazwa aliiacha CCM?

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom