Kwanini vyombo vya habari vilimuandama sana Trump kwa kutoripoti mazuri ya uongozi wake lakini vinakaa kimya kwa madhaifu mengi ya Biden?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Pamoja na madhaifu ya Trump yaliyokuwa yakishindiliwa na hata kuongeza chumvi lakini vyombo vya habari vilikuwa havitipoti mazuri aliyokuwa akiyafanya, hii ilifanya watu wengi sana hasa walio nje ya marekani wanaotegemea kupata habari za marekani kupitia cnn kumuona Trump mbaya.

Kuishinikiza nchi za ulaya za Nato kuchangia fair share lasivyo kuondoloewa NATO.

-Kuimarisha uchumi wa marekani, hakupewa credit yoyote na kwa uchumi alioukuta hata Obama alisema ni muujiza pekee ndio utafufua uchumi.

-Kuwaonya Ujerumani wasiingie mkataba na russia kwa bomba la gesi litalotengeneza utegemezi wa nishati,
-kwenda korea kuimarisha diplomasia, n.k.

-Kulitengea jeshi bajet nene bila kkuathiri uchumi

-Kuwapa mikono na saluti graduates zaidi ya elf 1 wa air force
-n.k.

Kwa biden hali ni tofauti, madhaifu yake hasa kwa ugonjwa wake wa akili hayavumi na nina uhakika ingekuwa trump kafanya hata theluthi tu basi vyombo vya habari ingekuwa ni trending news.

-Mbwa wa Biden alimshambulia mfanyakazi wa ikulu, Kimya,

-Biden kujikwaa wakati anapanda ngazi za ndege ni kawaida, aliwahi jikwaa mara tatu lakini stori ilibinywa.

- Kukosea maneno kwake kawaida sana, akiwa bunge la Canda aliwashukuru china badala ya Canada, akiwa illinois anaweza kusema yupo chicago, n.k.

- Biden hafanyi press na waandishi, anasaidiwa karibu asilimia 98 na secretary wake.

- Kesi ya mtoto wake kuhusu madawa ya kulevya wala haikuwa habari,

Mifumo ya vyombo vya habari vya kimagharibi ni wa kinafiki sana.

Mtu yoyote alie kinyume na unafiki kwao hivyo vyombo ni adui mkubwa, watamtengenezea kila aina ya propaganda mbaya aonekane mbaya dunia nzima lakini kumbe ni kinyume chake.
 
Trump alikuwa moja ya majembe lakini media ilichomfanyia sio kabisa, walikaa kimya sana kwa megi aliyoifanyia marekani, Trump alimarisha sana uchumi lakini media ilipiga kimya wapo bize kumchafua
 
Kuna jamaaa yupo insta ni mkenya comedian ana suti Moja halafu mda wote anakula mirungi anasemaga AKILI MTU WANGU AKILI??????
 
Pamoja na madhaifu ya Trump yaliyokuwa yakishindiliwa na hata kuongeza chumvi lakini vyombo vya habari vilikuwa havitipoti mazuri aliyokuwa akiyafanya, hii ilifanya watu wengi sana hasa walio nje ya marekani wanaotegemea kupata habari za marekani kupitia cnn kumuona Trump mbaya.
Mtoa mada unakaa nchi gani na unafuatilia vyombo gani vya habari?
 
Pamoja na Fox News na Newsmax??
Mifumo ya vyombo vya habari vya kimagharibi ni wa kinafiki sana.

Mtu yoyote alie kinyume na unafiki kwao hivyo vyombo ni adui mkubwa, watamtengenezea kila aina ya propaganda mbaya aonekane mbaya dunia nzima lakini kumbe ni kinyume chake.
 
Trump ndio Rais wa kwanza wa Marekani kujaribu kugeuza matokeo ya uchaguzi na kufanya mapinduzi ya serikali
 
Trump alikuwa moja ya majembe lakini media ilichomfanyia sio kabisa, walikaa kimya sana kwa megi aliyoifanyia marekani, Trump alimarisha sana uchumi lakini media ilipiga kimya wapo bize kumchafua
Hakika mkuu, yule mtu nadhani kwa zama zetu hizi hajawahi kutokea rais wa Marekani aliye kichwa kama Trump
Kwa upande wangu mimi hili ni tukio bora kabisa kuwahi kufanywa na rais wa Marekani kwa nyakati zote.
48162702412_53b8899c9c_k.jpg
trumpkimjong.jpg
 
Mifumo ya vyombo vya habari vya kimagharibi ni wa kinafiki sana.

Mtu yoyote alie kinyume na unafiki kwao hivyo vyombo ni adui mkubwa, watamtengenezea kila aina ya propaganda mbaya aonekane mbaya dunia nzima lakini kumbe ni kinyume chake.
Mifumo mizuri ni ipi ya kidikteta?
 
Back
Top Bottom