Kwanini vyombo vya habari haviendi Kibiti?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,753
34,854
Sehemu nyingi duniani kunapotekea mauaji ya watu iwe kwa ajali, vita, ama majanga ya kiasili, vyombo vya habari huwa ni watu wanaokwenda maeneo hayo kwa ajili ya kuhabarisha umma ni nini kinaendelea.

Tangu mauji ya Kibiti na maeneo yanayozunguka huko yaanze, kama taifa hakujakuwa na chombo chochote cha habari ambacho kimezitafuta habari za mauaji ama chanzo chake kwa kina na kuzileta kwetu wananchi.

Habari za Al Qaeda, Al shabab, vita vya Iraq, mambo ya IRA huko Ireland Kaskazini yote hayo dunia huyajua kupitia vyombo vya habari. Ni kwa nini vyombo vyetu vya habari mpaka sasa havijafanya juhudi za kutuletea habari za kina za kiuchunguzi kuhusu nini hasa kinachoendelea Kibiti?
 
Wamekatazwa kwenda wameambiwa wakienda na wao wanahesabiwa kama wauaji
 
Hakuna anayependa kuulizwa maswali baada ya kutoa taarifa hiyo ya uchunguzi.
Kwa kifupi, tunawanganga njaa tu na siyo vyombo vya habari.
 
Ata wewe unaweza kwenda kama muandishi wa kujitegemea tu kama pascal mayalla na ukaja na data zako nenda tu
 
Vyombo vya habari vya hapa nchini vinaweza kuripoti umbea, na kutotoa habari za Bashite. Ukija upande wa utoaji habari zenye mashiko na msaada kwa wengine wasiojua..upande huo ni zero. Kwa ufupi wanaganga njaa tu!
 
CHA AJABU JANA LOWASSA KAITWA KUHOJIWA WAKAJAZANA KAMA WAMEALIKWA....
Hawa daima wanapenda mteremko na hawajui umuhimu wa habari kama ya kibiti.Unaweza kuwa shujaa katika tasnia yako kwa kufuatilia suala kama la kibiti.
 
Sehemu nyingi duniani kunapotekea mauaji ya watu iwe kwa ajali, vita, ama majanga ya kiasili, vyombo vya habari huwa ni watu wanaokwenda maeneo hayo kwa ajili ya kuhabarisha umma ni nini kinaendelea.

Tangu mauji ya Kibiti na maeneo yanayozunguka huko yaanze, kama taifa hakujakuwa na chombo chochote cha habari ambacho kimezitafuta habari za mauaji ama chanzo chake kwa kina na kuzileta kwetu wananchi.

Habari za Al Qaeda, Al shabab, vita vya Iraq, mambo ya IRA huko Ireland Kaskazini yote hayo dunia huyajua kupitia vyombo vya habari. Ni kwa nini vyombo vyetu vya habari mpaka sasa havijafanya juhudi za kutuletea habari za kina za kiuchunguzi kuhusu nini hasa kinachoendelea Kibiti?
Mbona gazeti la mwananchi walienda na wakaleta walichokisikia huko
 
Kila siku wao ni kuandika habari za "kusikia" toka kwa wengine ni kwa nini hawaendi huko wenyewe na kufukunyua ili sisi watanzania kama taifa tujue nini kinaendelea huko?
Wanabana matu.imzi
Sehemu nyingi duniani kunapotekea mauaji ya watu iwe kwa ajali, vita, ama majanga ya kiasili, vyombo vya habari huwa ni watu wanaokwenda maeneo hayo kwa ajili ya kuhabarisha umma ni nini kinaendelea.

Tangu mauji ya Kibiti na maeneo yanayozunguka huko yaanze, kama taifa hakujakuwa na chombo chochote cha habari ambacho kimezitafuta habari za mauaji ama chanzo chake kwa kina na kuzileta kwetu wananchi.

Habari za Al Qaeda, Al shabab, vita vya Iraq, mambo ya IRA huko Ireland Kaskazini yote hayo dunia huyajua kupitia vyombo vya habari. Ni kwa nini vyombo vyetu vya habari mpaka sasa havijafanya juhudi za kutuletea habari za kina za kiuchunguzi kuhusu nini hasa kinachoendelea Kibiti?
 
hizo habari za mauaji wewe umezipata wapi??
hata wakienda kutakuwa na athari gani??
pia kama wataenda mauji yataisha??
 
Back
Top Bottom