Kwanini vyama vyingi vinataka chadema ife?
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kila chama kina haki ya kushiriki uchaguzi
Kila chama kina haki ya kusimamisha wagombea
Swali,ni je, kwanini vyama vyingi badala ya kutaka ccm iondoke madarakani vinataka chadema ndio ife?
Ukifanya utafiti usio rasmi utagundua cuf,nccr tlp na baadhi ya vyama viko tayari ccm iendelee kubaki madarani kuliko chadema kupata wabunge wengi au kushika dola,je vyama vyingine vya upinzani kutaka chadema ife lkn ccm ibaki madarakani viko sahihi?na kwanini unafikiri vinatamani chadema ife?
Anayeiua Chadema ni Mbowe. Huyu kiumbe mkabila na mfanyabiashara wa kisiasa anaonekana wazi amepewa au ameahidiwa mpunga mrefu sana ili kuhakikisha Tanzania haipati Chama chenye Demokrasia na kushika Dola.
Tukiacha ushabiki tukamtafakari Mbowe vizuri na wenyeviti wenzake tutapata jibu na ama kuwatimua kwa marungu na mawe toka kwenye Ofisi za vyama vya watanzania na kuweka katiba bora zinazojenga vyama kitaasisi sio vyama vya mtu binafsi.
Nimemsikiliza vizuri Kibajaji Bungeni nikagundua kuwa yule jamaa anaipenda sana Chadema na anaumia sana anavyoona jinsi Mbowe anavyoiua kwa manufaa yake.
Serikali nzima ya Awamu ya Tano iliingia ikiwa na imani ya kupata sapoti kubwa kutoka Chadema kuliko kutoka CCM kwani wengi walikua ni wale walikua wanachukizwa na ufisadi,uzembe, ubabaishaji,wizi,rushwa umangi meza na kila aina ya uhalifu uliokuwa unafanywa na watawala.
Cha ajabu Mbowe alibadili gia angani na kupinga kila kitu mpaka ushauri mzuri wa kujenga makao makuu ya Chadema Dodoma aliokuwa amepewa na Mh . Rais siku ya kuzindua Bunge . Hapo ndipo nilipoanza kumtoa Mbowe kwenye thamani kabisa. Nikamfutilia Mbali kabisa kwenye orodha ya wanasiasa wenye nia nzuri na nchi yetu alipochukua tena form na kugombea Uenyekiti kwa awamu ya nne.
Mbowe anazeeka huku Chama chake kikiwa kinakufa kwa kasi ya ajabu.
Sijui angeacha Demokrasia ikashamiri ndani ya Chadema angepata hasara gani! Bora Mbowe angeachia mwingine Chama kisimfie mikononi mwake. Hakika Mbowe atafuta historia yake nzuri kwa uroho wa madaraka.
Wachawi wa vyama vya upinzani ni wenyeviti wao na sio CCM. CCM ya sasa ni Chadema asilia kwa hiyo kama Mbowe angecheza karata yake vizuri angekijenga Chama chake vizuri sana na kumwachia mwingine kiti kidemokrasia kabisa.
Ukiua Demokrasia kama Mbowe inabidi utumie nguvu kubwa kulinda kiti chako.
ACT Wazalendo kitakua Chama kikuu cha upinzani mana kinaongozwa na mtu aliyekua na maono ya kuujenga upinzani , ubinafsi wa Mbowe akamfukuza. Chama kitakachofuatia kwa kuwa na wabunge wengi kitakuwa ni NCCR kikifuatiwa na Chadema