Kwanini viongozi wa Kanda CHADEMA wengi ni wabunge?

Kwanini viongozi wa Kanda CHADEMA wengi ni wabunge?

viking

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
2,289
Reaction score
1,426
Najaribu kujiuliza huwa sipati majibu. Kwa nini viongozi wengi wa kanda wa chadema ni wabunge.

Hivi hakuna watu wengine kwenye kanda wakagombea hizi nafasi ili baadae waje kugombea nafasi za kitaifa au ubunge?

Kumpa nafasi ya kiongozi wa kanda mbunge fulani kusema kweli ni kumtwisha zigo lingine la madaraka ambalo linahitaji muda mwingi.

Fikiria ameenda bungeni kwa miezi 3, je shughuli za kikanda zitafanyika kweli achilia mbali shughuli za jimboni kwake?

Hamuwezi kujua mna viongozi wengi wazuri wazuri pasipo ku wa groom wengine. Hii tabia ya power monopoly sio nzuri katika ujengaji wa chama.
 

Attachments

  • 2261267_tapatalk_1571851230700.jpeg
    2261267_tapatalk_1571851230700.jpeg
    9.2 KB · Views: 13
Wewe nyege-nyero hebu wataje tuone kama kweli ni wengi! CCM yalishakosa hoja yamebakiza viroja!
 
Nijuavyo mimi wengi wao ni wenyeviti. Na kazi za kikanda huwa zinafanywa na makatibu.

By the way, katiba ya taasisi au chama ndio inatoa muongozo kwa mapana yake. Kama katiba yao inaruhusu mbunge kugombea nafasi ya kuwa kiongozi wa kanda, mimi sioni haja ya kuhoji kwa nini wengi wao ni wabunge. Huenda ndio waliojitokeza na wamenadi sera nzuri kwa wapiga kura wao.
 
Hao wanalao jambo , hawafanyi kwa bahati mbaya ,ni mkakati wa kisiasa ,wengi wanajua hawarudi bungeni kipindi kijacho ,hivyo wametafuta eneo la kujifichia kukwepa aibu ya kupotea kwenye siasa hapa nchini,hivyo kupitia nafasi hizo hawatapotea na itawapa nafasi ya kujipanga 2025viking,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu utetezi wa katiba yao inaruhusu ni wa kijinga sana, hivi Katiba ni Quran au Biblia, wengine watapata vipi nafasi kama nafasi zote zinashikiliwa na watu hao hao?
 
Huu utetezi wa katiba yao inaruhusu ni wa kijinga sana, hivi Katiba ni Quran au Biblia, wengine watapata vipi nafasi kama nafasi zote zinashikiliwa na watu hao hao?
Kwanini mawaziri ni wabunge?Usilete utetezi wa katiba maana ni wa kijinga sana!
 
Back
Top Bottom