Kwa mtu ambaye hakupata fursa ya kusoma kwa kweli wana wakati mgumu sana. Kwa mtu aliyesoma, Mungu nisamehe tu ila naona ni uzembe.
Yaani vichwa vimijaa kuajiriwa tuuu. Mtu ana degree ya Accounts na yeye anahangaika na kulalamikia ajira. Wakati angeweza kufanya consultation work, kuandika proposals, business plans.
Mtu kasomea sheria, anashindwa hata kuandika mikataba ya kuuziana viwanja, nyumba, magari apate hela. Kama hana muhuri, mtafuti mwenye muhuri ushirikiane naye, unamlipa chochote apige muhuri.
Mtu kasomea kodi, kila siku wana lalamika kodi, uwezi fanya hata consultation kwa wafanya biashara, maduka, makampuni kweli?
Yaani list ni ndefu... Nikasema nitengezene mtandao wa wao kujinadi hizo huduma wanazoweza kutoa, ila waziito. Wanaangalia na kusema watajiunga baadae, mara kesho, mara weekend, siku zina kata tu.
Matokeo yake unamwita interview, unamuuliza miaka miwili yote hii tokea umemaliza chuo ulikuwa unafanya nini? Anakwambia natafuta kazi, umefanya shughuli yoyote inayoendana na taaluma yako au kazi unayoomba, hapana, sikuwa na kazi. Pumbavu kabisa.