Kwanini vijana wengi wa kitanzania wanalalamika maisha magumu!

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,258
2,000
Wakuu
husikeni na kichwa tajwa hapo juu hii hali inanishangaza
je wanashindwa kujiajiri au shida ni nini?
kwa ujumla tutoe mawazo ili baadae yatusaidie kupata solution ya hili tatizo because mimi naamini ukiamua kujiajiri hata bila mtaji wa kuanzia unaweza kwa kufanya huduma au vibarua then ukapata pesa ya kuanzia maisha so huwa nashindwa kuelewa ni kwanini vijana wengi wanalalamika sana
Hivi unadhani kujiajiri ni rahisi ?, kumbuka hapo ulipo unauza nyanya au genge sababu tu corporations na big business hazijaja zikija na wewe na kibiashara chako vyote vitaenda na maji..

Kuona fursa ni talent sio kila binadamu anaweza, kwahio inabidi wachache waona fursa ndio waweze kuweka vitu vya kuweza kuwakomboa wengine (big, businesses, corporations etc).., kwahio mkuu huku kujidanganya kwamba kila mtu asome alafu aende kivyake kutafuta fursa ni ndoto za mchana.., when push comes to shove na competition becomes the norm only the strongest and few survive, ukizingatia soko ni moja na unaoshindana nao ni people with high buying power..
 
D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
2,871

Sikupingi lakini zikija nadhani mimi pia nitakuwa either nimebadilisha upepo kwenye biashara nyingine au hiyo big company nachuana nayo..
Usisahau pia npo na part time job japo hainilipi sana
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,258
2,000
Sikupingi lakini zikija nadhani mimi pia nitakuwa either nimebadilisha upepo kwenye biashara nyingine au hiyo big company nachuana nayo..
Usisahau pia npo na part time job japo hainilipi sana
Wewe unaweza ukawa ni among minority mwenye business skills na right attitude ambayo ni wachache wanayo majority hawana thus dependent on being employees..,

when corporations come into your target customers you can not compete unless uje na new innovation uiwekee patents za kutosha na kama ni kubwa sana na haujajiandaa watakwenda mahakamani na kesi utashindwa... uki-survive ni among the few ambapo wengi kama wewe wangefanya wengeshindwa
 
D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
2,871
2,000
Wewe unaweza ukawa ni among minority mwenye business skills na right attitude ambayo ni wachache wanayo majority hawana thus dependent on being employees..,
when corporations come into your target customers you can not compete unless uje na new innovation uiwekee patents za kutosha na kama ni kubwa sana na haujajiandaa watakwenda mahakamani na kesi utashindwa... uki-survive ni among the few ambapo wengi kama wewe wangefanya wengeshindwa
nakuelewa mkuu wewe ni mmoja kati ya watu wanaoonekana wana hoja,je wewe unawashaurije vijana wanaozidi kulalamikia hili suala la ajir.
Je waendelee kulalamika na kuvumilia mpaka wapate ajira hizo ambazo hazijulikani ni lini watapata?
Au wabadilishe mindset zao kwenda kwenye fursa zingine
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,258
2,000
nakuelewa mkuu wewe ni mmoja kati ya watu wanaoonekana wana hoja,je wewe unawashaurije vijana wanaozidi kulalamikia hili suala la ajir.
Je waendelee kulalamika na kuvumilia mpaka wapate ajira hizo ambazo hazijulikani ni lini watapata?
Au wabadilishe mindset zao kwenda kwenye fursa zingine
Kosa sio vijana tu.., sababu wale wanaokula kodi zetu hawafanyi kazi zao kutengeneza mitandao vijana wapate ajira.., na so called educated hawaji na mikakati long term ya kuzuia hili balaa.., matokeo yake wanaleta majibu ya holela na shortcuts kwamba kila mtu ajitafutie fursa wakati wenyewe fursa wanayoiona ni kula mishahara minono kwa mgongo wa kodi zetu na wanalolifanya halionekani (thus ndio maana siasa imekuwa fursa ya kujilimbikizia mali)

Pia kuwaambia watu fursa kumekuwa fursa ya kuwatumia watu kuwauzia theoretical information; yaani biashara kubwa Tanzania ni fursa ya kuwaambia watu jinsi ya kutafuta fursa ili wapate fursa (not implementing the fursa but talking about it and spreading the word)
 
ForeverMore

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
655
1,000
Kwa mtu ambaye hakupata fursa ya kusoma kwa kweli wana wakati mgumu sana. Kwa mtu aliyesoma, Mungu nisamehe tu ila naona ni uzembe.

Yaani vichwa vimijaa kuajiriwa tuuu. Mtu ana degree ya Accounts na yeye anahangaika na kulalamikia ajira. Wakati angeweza kufanya consultation work, kuandika proposals, business plans.

Mtu kasomea sheria, anashindwa hata kuandika mikataba ya kuuziana viwanja, nyumba, magari apate hela. Kama hana muhuri, mtafuti mwenye muhuri ushirikiane naye, unamlipa chochote apige muhuri.

Mtu kasomea kodi, kila siku wana lalamika kodi, uwezi fanya hata consultation kwa wafanya biashara, maduka, makampuni kweli?

Yaani list ni ndefu... Nikasema nitengezene mtandao wa wao kujinadi hizo huduma wanazoweza kutoa, ila waziito. Wanaangalia na kusema watajiunga baadae, mara kesho, mara weekend, siku zina kata tu.

Matokeo yake unamwita interview, unamuuliza miaka miwili yote hii tokea umemaliza chuo ulikuwa unafanya nini? Anakwambia natafuta kazi, umefanya shughuli yoyote inayoendana na taaluma yako au kazi unayoomba, hapana, sikuwa na kazi. Pumbavu kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom