Kwanini Vijana wanasubiri wafike 30+ndio waoe/kuolewa, wanaogopa nini kuingia kwenye ndoa mapema?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari,

Jamani ndoa nyingi mbona ni za people aged from 30+ kuna siri gani hapa. Watu wazima ndo wanaoana alafu eti Youths wao hawataki kuoa/kuolewa.

Nimeshuhudia ndoa nyingi Ila asilimia kubwa unakuta wanandoa ni watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 30+ kwani vijana wao wana nini mpaka wasioe/kuolewa.

Alafu ukitaka kuoa mapema ili ui enjoy maisha utasikia maneno eti "hujakua maisha ya ndoa huyawezi".Hii ndio inapelekea vijana wanakua playboys hata wakiingia kwenye ndoa wanachepuka kwasababu washazoea loose life wakiwa wadogo so hata wakikua inaendelea tabia ile ile.

Au labda tuseme vijana wanasubiri wale maisha kwanza alafu wajihisi wametosheka ndo wanatafuta wenza wa kuspend nao the rest of their life.

Kuna wakati ukioa/kuolewa mapema ndoa inanoga sasa ukisubiri mpaka uzeeke ndo uoe/uolewe no enjoyment kwenye marriage .

Yaani ukisikia wanandoa nowdays utakuta na mijibaba na wanawake wenye umri mkubwa. Vijana wanaogopa nini kuingia kwenye ndoa mapema.
 
Points ni zile zile

1.Kukwepa/kuogopa majukumu ya kifamilia
2.Umalaya
3.Kuogopana/kutokuaminiana,siku hizi kumekuwa na tabia ya kutupiana sana lawama....baadhi ya wanawake wanadai wanaume hawaeleweki,na wanaume hawaamini kabisa wanawake
4.Kujirahisisha,kuna wale wanasema eti sijui kama unapata maziwa unapata kwa wakati eti haipo sababu ya kununua ng'ombe mzima...unakuta mtu hamjaoana lakini unaenda kwake unafua,unadeki,unapikia mwanaume akimaliza na yeye analiwa

Mungu asaidie niolewe kabla ya 30,kuna muda nahisi kuolewa ni raha
 
Duh!hadi umetamani kuoelewa maskini

Sema zamani ndoa ilikuwa simple mnakubaliana mna oana

Ila ikafika time wanaume wakawa wanatamani ndoa Ila wanawake hawataki

Nowdays wanawake wanatamani ndoa ila wanaume hawako ready
 
Nilivokuwa na miaka 18 nilitaka kuoa nikawashirikisha na familia walinipinga sana wakisema balehe inanisumbua na bado sijakomaa kuweza kumiliki mke , mpaka leo nina miaka 41 sijaoa natamaa nimekata
Wakati huo unakuta wazazi wao wali ingia ndoani wakiwa wadogo
 
Tuanze na wewe kwanza mleta mada....umeoa?? Maana kwa wingi wa thread unazoleta humu jukwaani inaonesha kabisa you're below 30 yrs of age boy!
Kama bado hujaoa basi kinachokufanya usioe mpaka Sasa ndo hicho hicho kinacho wasibu vijana wenzako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh!hadi umetamani kuoelewa maskini
Sema zamani ndoa ilikuwa simple mnakubaliana mna oana

Ila ikafika time wanaume wakawa wanatamani ndoa Ila wanawake hawataki

Nowdays wanawake wanatamani ndoa ila wanaume hawako ready

Kiuhalisia sidhani kama kuna mwanamke ambaye hajawahi kuolewa hatamani kuolewa

Labda wale waliowahi kuolewa wakakutwa na ya kuwakuta wakaichukia ndoa
 
Kipimo cha akili timamu kwa kijana wa kiume ni kuoa na kijana wa kike ni kuolewa.

Kama hujaoa au kuolewa inabidi ujitathmini aisee. Hapa siwaongelei wale walio fiwa na wake zao au waume zao, bali wale mabazazi na wazandiki.
 
hata mimi nilioa rasmi nilipofikisha miaka 32 ingawa huyomchumba nilipata tangu nikiwa na miaka 22. habari ya kuanza kulea familia na kuitwa baba siyo lelemama.
 
Kiuhalisia sidhani kama kuna mwanamke ambaye hajawahi kuolewa hatamani kuolewa

Labda wale waliowahi kuolewa wakakutwa na ya kuwakuta wakaichukia ndoa
Sasa Joanah mbona kazi rahisi hata wanaume wanatamani kuoa mbona wengi Ila shida ipo kwenu ladies
Unakuta mwanaume yupo ready kuoa Ila ladies mnasema its not the right time
 
Kama n swala la kijipanga kimaisha n kheri kijana angoje

Ila ukiona umeanza nyatia watoto wa watu ww oa tuu huo ndo wakati sahihi hakuna wakati mwengine zaidi ya huo zaidi ya hapo n kujichelewesha tuu
 
Back
Top Bottom