Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 88,420
- 154,843
Neema na karaha yote maisha tu. Bora anafanya kazi halali hajaiba kwa mtu wala kufanya jambo la fedheha au jinai. Amekubali kituo alichofikishwa na basi la maisha, na anajitumikisha kufanya maisha yake yawe bora zaidi.
Huyu amejua utubora mara nyingi zaidi ya wauza madawa ya kulevya wanaotembelea mabenzi makubwa.
Anayeweza mtihani wa kutopata alichotaka au kupata asichotaka, na kuishi bila kuhamanika na kuingia kwenye vishawishi vinavyozaa fedheha, ameweza kushinda mtihani mkubwa sana wa maisha.
Mbaraka Mwinshehe aliimba shida haiishi mpaka siku ya mwisho. Unaweza kuwafurahia wenye kuonekana na neema, kumbe wana madeni na kesi zimewabana mpaka shingoni hawana amani.