Sababu 31 kwanini Magufuli hawezi kuwa rais wa Tanzania

Fandre

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
320
225
SABABU 31 KWANINI MAGUFULI HAWEZI KUWA RAIS WA TANZANIA WALA CCM KUENDELEA KUIONGOZA TANZANIA.
By Fandre

Suala la Uchaguzi Mkuu katika Taifa lolote lile huwa ni suala kubwa na lenye kubeba maslahi mapana kwaa Taifa husika kutokana na kuwa ndio njia pekee HALALI ya kupata kiongozi Mkuu wa Nchi pamoja na viongozi wengine watakaounda serikali.

Suala hili linakuwa kubwa na la kuvuta hisia na umakini wa watu wengi zaidi hasa linapofanyika katika nchi zenye mfumo wa Demokrasia ya Uwasilishaji yaani Representative Democracy kama Tanzania ambapo kiongozi hupatikana kwa kupigiwa kura kwa njia ya masanduku ya kura(Ballot Box) ambayo ni siri na humfanya mpiga kura kuwa huru zaidi kumchagua mgombea yule anayeona anaweza kumletea MABADILIKO anayohitaji kulingana na vipaumbele vya mahitaji yake huku akioanisha na Ilani, Umakini wa mgombea na uwezo binafsi wa mgombea kama anaweza kuyatimiza yale anayoyaongea ama kuyaahidi.

Kwa sababu hizo za msingi hapo juu, name nimeshika kalamu kuandika sababu zangu 31 TU za kwanini Watanzania TUSIMCHAGUE MAGUFULI KABISA KUWA RAIS wetu kutokana na ukubwa wa nafasi hii na kule tunakotaka Taifa hili kwenda baada ya CCM na uongozi wake kutufikisha hapa tulipofika leo hii.


Naam, sasa naanza kuzitaja sababu zangu 31 za kumkataa Magufuli na CCM yake:


1. MAONO (VISION)

Uongozi wowote ule ni maono na kwa nafasi kubwa kama ya urais ni mtu mwenye maono tu ndio anayestahili kuwa kinara na mwenye nia thabiti ya kushika hatamu katika eneno hilo. Magufuli hana na hajawahi kuwa na Maono na nafasi ya Urais anayogombea leo, kwahiyo hajawahi kujiandaa hata mara moja wala hakuwahi kuwaza kama atakuja kuwa kiongozi mkuu wan chi hii. Miaka yote amekua akilia kuendelea kubakishwa katika Wizara ya Ujenzi na Miundombinu.

2. HANA UELEWA WA SIASA ZA KITAIFA WALA KIMATAIFA

Jambo hili liko wazi, Magufuli ana uelewa mdogo sana wa siasa za Kitaifa na Kimataifa. Tangu ameanza kampeni kila mtu ameshuhudia jambo hili lisilohitaji ubishani. Siasa za Kitaifa zimekuwa kubwa sana kwa Magufuli na mzigo.

3. ANA MAAMUZI MABAYA NA YA HARAKA(MKURUPUKAJI)
Magufuli ni mtu ambaye hupenda sana kuonekana amefanya jambo hata kama ni baya ila aonekana amefanya. Kuna tofauti kubwa kati ya maamuzi magumu na maamuzi ya haraka na mabaya

4. MAGUFULI SIO CHAGUO LA CHAMA CHAKE

Magufuli hakuwahi kuwa chaguo la chama chake hivyo yeye kupata nafasi ya kuwania urais ni matokeo ya visasi, chuki, mpasuko na vita vya ndani ya chama cha CCM. Jambo hili limeshuhudiwa wazi kabisa pale mjini Dodoma katika Ukumbi Mpya wa Chama cha Mapinduzi siku ambayo majina matano yalipotangazwa kwani wajumbe kwa wingi wao walianza kuimba jina la bwana Lowassa kuashiria kuwa wao ndio mtu waliyekuwa wamemuandaa na kumuamini kumpa ridhaa ya kuwa mgombea kupitia chama chao.

5. MGOMBEA ASIYE NA MVUTO
Kiongozi mzuri huwa na tabia ya Kupendwa na watu yaani Charisma lakini kwa Magufuli ni tofauti ndio mana CCM inatumia gharama kubwa kumnadi Magufuli kuliko ghrama ilioztumia katika chaguzi zozote zile. Magufuli anakosa mvuto kutokana na kuwa na visasi vingi na wananchi huko nyuma hasa kutokana na maamuzi mengi ya kukurupuka yaliyoigharimu serikali na wananchi kwa ujumla. Kadharika kutokuandaliwa kwake kunamfanya akose mvuto zaidi kwani wananchi hawakuwahi kumuwaza kma atakuja kuwa mgombea kupitia chama cha mapinduzi.


6. ANAGOMBEA WAKATI CHAMA CHAKE HAKINA UMOJA

Hii inatupa picha ya kwamba akiwa Rais atatumia muda mwingi kujenga chama kwa gharama kubwa kuliko kujenga nchi, pia inaashiria ya kuwa atakandamiza sana demokrasia ili kuinua upya misingi ya chama chake iliyokwishapotea. Viongozi wengi wa CCM wamesusa kushiriki katika kampeni za Uchaguzi baada ya kupigwa chini katika kura za maoni na wengine kutoswa urais.

7.
HAUNGWI MKONO NA WATANZANIA WALIO WENGI
Sensa ya mwaka 2012 ilionyesha dhahiri ya kuwa Vijana ndio kundi kubwa katika jamii ya Kitanzania yenye zaidi ya asilimia 68 na kundi hili ndio linalohitaji MABADILIKO NJE YA MFUMO WA CCM. Kwahiyo tayari magufuli ameshindwa kabla ya uchaguzi, kumchagua Magufuli ni kupoteza kura yako.


8. CCM IMEISHIWA MBINU ZA KUSHINDA

Kwa miongo mingi CCM imekuwa na mbinu nyingi za wizi wa kura lakini mfumo uliowekwa mwaka huu tayari umeshawanyima raha CCM na kuonyesha wazi kuwa hawataweza kuiba hata kura moja kwani kura zote zitahesabiwa kituoni na masanduku ya kura hayataruhusiwa kusafirishwa. Ndio maana CCM baada ya kujua hili wameanza kulalamika.


9. LOWASSA NI BORA ZAIDI KATI YA WAGOMBEA WOTE

Ubora wa Lowassa unatokana na kuwa na Maono (Vision) kwa muda mrefu hivyo kujipanga vyema na Imani waliyonayo watanzania juu ya uwezo wake wa kuondoa kero zao ndio kunakomfanya kuwa mgombea anyependwa zaidi.

10. USALITI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Miaka ya hivi karibuni CCM imekumbwa na usaliti pamoja na mambo kadha wa kadha ambayo yalikuwepo kwa mud amrefu lakini alikosekana wa kuyakemea kutokana na kuwa hakuna aliye msafi ndani ya CCM mwishowe leo wanatafutana mchawi wakiwa wameshachelewa.

11. VYOMBO VYA HABARI
Magufuli hajawahi kuwa rafiki wa vyombo vya habari kama ilivyokuwa kwa mgombea wa UKAWA Mh. Lowassa, hivyo waandishi wengi wanaoandika habari za Lowassa huandika wakijihisi na wao ni sehemu ya MABADILIKO ila wale wanaoandika habari za Magufuli huandika kwakua wanalipwa fedha nzuri isingekuwa hivyo wasingeandika kabisa au wangempuuza ama wangeandika kwa sababu wanatakiwa kuandika habari.


12. RUSHWA, WIZI, UHARAMIA NA UKANDAMIZAJI
Kwa miaka mingi imekuwa ni jambo la kawaida sana unapotaja tu jina CCM basi watu huelewa unamaanisha rushwa, wizi, uonevu, ukandamizaji na usafirishwaji wa wanyama wetu nje ya nchi. Kwa lugha ya kiingereza wanasema maneno haya ni Synonyms of CCM. Kwahiyo mambo haya yamewafanya watu wengi kuchoka kabisa na kuamini siasa za CCM.


13. LUGHA ZA KEBEHI NA MAUDHI ALIZONAZO MAGUFULI
Magufuli hakuwahi kuwaza kuwa rais hicyo alikuwa akiongea kila kilichokuwa kinakuja mdomoni mwake na kuwajenga wananchi wengi kumchukia na kumuona kama kiongozi asiye na huruma na shida au taabu ambazo wao wanazipitia. Wananchi wengiwameamua kumlipiza kwa kumaungusha katika uchaguzi. Mf: Majibu ya kuwa asiye na 200 apige mbizi kwenda kigamboni; Majibu juu ya bomoa bomoa alizokuwa akiziendesha na kuzisimamia.


14. UZOEFU WA LOWASSA
Hii ndio homa walionayo CCM juu ya Lowassa kwani jambo hili limemfanya Lowassa kuwa na uwezo wa kujua kila aina ya mipango wanayoifanya CCM muda mfupi mara baada ya kupanga labda ndio maana makampuni huitaji mtu mzoefu kwenye kazi kama kigezo cha kupata kazi. Lowassa anajua kila aina ya njia ambayo CCM hutumia kuiba kura na kujitangaza washindi.


15. WATANZANIA WANAHITAJI MABADILIKO
Kwa Zaidi ya miaka 54, CCM imekuwa ikiongoza taifa hili lakini sasa kinachoonekana wazi ni kuwa watanzania wamechoka na wanahitaji mabadiliko sio tu ya kiongozi bali ya kimfumo na muundo na njia pekee wameamua kuitoa CCM madarakni ikajipange upya.


16. MAGUFULI AMEKUWA MGOMBEA WAKATI CCM INACHUKIWA SANA
Siku za hivi karibuni tumeshuhudia makundi mbalimbali ya watanzania wa kada za aina zote wakijitokeza pasipo hofu na kueleza kuwa wamechoshwa na CCM hivyo kwa tafsiri sahihi ya jambo hili ni kuwa wananchi walio wengi hawamuungi mkono Magufuli kwakua wanaichukia CCM na utawala wake usiojali wananchi.


17. CCM HAINA WAFUASI WENGI KAMA INAVYODANGANYA UMMA
Watanzania wote tumeshuhudia jambo hili kwa wazi kabisa kuwa CCM haina kabisa wafuasi au mashabiki wengi ila imekuwa ikiwasafirisha wafuasi wake wa jimbo moja nakuwapeleka jimbo jingine kwa kutumia malori na magari madogo ili tu kuwadanganya watanzania kuwa wao bado wana watu wengi kitu ambacho sio kweli kabisa. Wanachofanya ni sawa na kutoa pesa mfuko wa kushoto na kuweka mfuko wa kulia.


18. UONGOZI MBOVU WA CHAMA CHA MAPINDUZI
Mpaka kufikia leo hii hadi watoto wadogo wanafahamu fika ya kuwa CCM ina uongozi mbaya ambao ndio umekifikisha chama hapa kilipo leo na hivyo jambo hili litaendelea kukitafuna chama hiki kwa muda mrefu mpaka pale watakapokua wapo tayari kuunda upya mfumo wao wa uongozi ndani ya chama.


19. SUALA LA MAADILI, UWAJIBIKAJI NA UWAZI
Ni jambo lililowazi kuwa kumekuwa na mbinu nyingi sana za waovu na wezi wa mali za umma kulindwa na chama cha mapinduzi badala ya kuwajibishwa na kuvuliwa uanachama kutokana ka kurudia makosa yaleyale. Kupotea kabisa kwa maadili kwa viongozi na makada wa chama hiki kumefanya watanzania wengi kukichukia chama hiki.Mfano: Wezi wa Escrow, EPA, RICHMOND, RADA, MEREMETA n.k ni watu walewale


20. CCM SI TEGEMEO LA VIONGOZI BORA TENA
Kwa miaka mingi ya nyuma watanzania walikuwa wakiamini ya kuwa viongozi bora wa nafasi ya Urais watapatikana toka CCM lakini kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kukua kwa upinzani na ongezeko la maarifa na habari miongoni mwa wananchi wengi wamegundua ukweli ya kuwa CCM ya leo si ile ya Mwl Nyerere na ni kichaka cha kunufaisha matajiri wachache na kuwafukarisha watanzania walio wengi.

21. MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA YA CCM KATIKA UCHAGUZI
Kutokana na Magufuli kuonekana kuwa hana mvuto na ni ngumu kumnadi kama ambavyo wajumbe wengi wa kamati kuu ya chama cha mapinduxi waliwahi kuzungumza kwa nyakati tofauti tofauti jambo hili limekifanya chama chake kutumia gharama kubwa katika kumnadi, kuwahonga watu, kuwanunua wapinzani haas wale watu ambao walikuwa mstari wa mbele katika mapambano ya kupigania Uhuru wa Pili wa Taifa hili toka mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi.

Wananchi wengi wamechukizwa na namna ambavyo Chama hiki kinatumia gharama nyingi katika kusaka urais kuliko kuleta maendeleo wakati walipokuwa na muda wa kufanya hivyo zaidi ya miaka 54 iliyopita.
NB: Gharama ambazo CCM inatumia katika Uchaguzi inadhihirisha tosha kabisa kuwa hawako tayari kuja kuleta maendeleo katika Taifa hili hata kama watakuja kupata ridhaa ya kuongoza.

22. UONGOZI MBOVU WA RAIS ANAYETOKA MADARAKANI
Rais anayetoka madarakani alionekana kuwa tumaini la watanzania wakati anaingia madarakani mwaka 2005 kwa awamu ya kwanza lakini aliwakatisha watanzania Tamaa na baada ya kuvurunda zaidi ameondoa imani ya watanzania kwa Chama cha Mapinduzi hivyo kumfanya mgombea ajaye kupitia chama chake yaani Magufuli kuwa na wakati mgumu zaidi katika ushindani wa Medani za siasa za kweli katika taifa hili.

23. TUME YA UCHAGUZI CHINI YA JAJI RUBUVA
Siku za hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa mwiba mkali kwa Chama cha Mapinduzi baada ya kuonekana kuwa iko imara na haitakuw atayari kupendelea upande wowote, tunaimani Jaji Rubuva ni mtu mweledi na mchapakazi pamoaja na uzoefu wake katika kazi utamfanya kuifanya tume hii kuwa Tume ya kihistoria katika kutenda haki na kuleta mabadiliko katika tiafa na hii ndio hofu kubwa iliyoitawla CCM kwakua miaka yote hutegemea mbinu ya wizi wa kura kama njia ya kuchukua dola pamoja na kushinda chaguzi nyingine ndogondogo nyingi.

24. UMASIKINI WA WATANZANIA

Kutokana na ongezeko la umasikini wa taifa hili unaochangiwa na ugumu wa maisha ambayo yote haya ni matokeo ya utawala mbovu, sera mbovu, serikali kushindwa kusimamia vyema rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla; jambo hili limekuwa ni shubiri katika mioyo ya watanzania na hivyo wamenuia kwa pamoja sasa kuiangusha serikali ya CCM na kuamua kuanza uoya na kuunda mfumo upya ukiwa chini ya chama kingine huku wakiamini UKAWA ambako Lowassa ndiye mgombea wake kinafaa kuwa mrithi sahihi wa CCM.

25. ONGEZEKO LA WASOMI NA MATOKEO YA SHULE ZA KATA
Kwa sasa taifa hili lina idadi kubwa nguvukazi yenye ujuzi ambayo bado haijapata kazi za kufanya na hivyo watu hawa wenye ujuzi hasa wasomi wa vyuo vikuu, vyuo vya kati na elimu ya sekondari wamekuwa watu wa mbele kabisa katika kutangaza, kuyadai na kuyaimba mabadiliko huku wakionanisha mabadiliko ya kiunogozi yaliyofanyika katika nchi mbalimbali barani Afrika kuwa sasa ni zamu ya Tanzania.

Kwa upande mwingine, wimbi la wanafunzi waliosoma shule za kata ambao leo hii zaidi ya asilimia 99 tangu shule hizi zilipoanza walikwisha timiza miaka 18 na kujiandikisha kupiga kura wote wanamuunga mkono Mh. Lowassa huku wakimuona kama mkombozi wao katika kupata elimu ya sekondari.

26. NAFASI YA MITANDAO YA KIJAMII NA SIMU ZA AINA YA SMARTPHONE
Mapinduzi makubwa yaliyofanywa katika ulimwengu wa Mawasiliano hasa baada ya ugunduzi ya mitandao ya kijamii pamoja na simu za viganjani ambazo zina uwezo mkubwa wa kupokea taarifa zinasemekana kuwa ni jambo kubwa sana lenye kuleta mageuzi makubwa katika siasa za Ulimwengu mzima. Mfano mwepesi ni majirani zetu Kenya ambapo wanazuoni wa elimu ya siasa wanasema mitandao ya kijamii ndio iliyochehchea ushindi wa Bwana Uhuru Kenyata.

Kadharika ndivyo hali ilivyo hata hapa nchini Tanzania ambapo inaonekana mitandao ya kijamii kujadili sana madhaifu makubwa ya Chama cha Mapinduzi na wagombea wake hivyo kusafiri kwa taarifa hizi kwa kasi kunawafanya watanzania wengi pia kuwa na uelewa mpana juu ya suala la uchaguzi na wagombea pamoja na vyama vyao. Hii ni silaha kubwa sana ambayo imekuwa ni sumu kwa chama tawala.

Taarifa zilizopo zinasema ya kuwa tayari serikali kupitia TCRA imekusudia kuzima DATA ambayo kimsingi ndio njia ya usafirishaji wa taarifa kwa watumiaji wa simu za smartphone hivyo kuingilia kati na kufanya wananchi wasipeane taarifa za uchaguzi na kujua nini kinaendelea.

27. NAFASI YA VYOMBO VYA DOLA
Wahenga waliwahi kusema..."Siku ya kifo cha nyani basi miti yote huteleza" ndivyo meli ya Chama cha Mapinduzi inavyoendelea kuzama zaidi baada ya vyombo vya dola haa vya Usalama kuweka maamuzi yake wazi kabisa kwa taifa kwa ujumla juuya kutokujihusisha kwa namna yeyote ile na kuingilia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Tarehe 25 Oct kama ambavyo imepangwa. Jeshi la Wananchi chini ya Mkuu wake wa Majeshi Mwamunyange tayari wameshatoa tamko, lakini hali pia si shwari kwa jeshi la polisi ambalo mpasuko ni mkubwa kwani wapo askri ambao wanaonekana wazi maka sasa kuwa wanatekeleza maazimio ya chama Dola huku wengine wakiwa hawataki kabisa na kuwa hawana upande wowote na kuwaacha wanasiasa wenyewe waendelee na shughuli za ushindani katika siasa zao.

Tunaimani muda utakapowadia pia Jeshi la Polisi nalo litatoa tamko kutokuingilia uchaguzi kwa namna yeyote ile, Mkuu wa Jeshi la Polisi Ernest Magu ni mtu mweledi na mpenda haki tunaimani mwaka huu jeshi hili ambalo hupokea lawama sana toka kwa wananchi litakaa kando na mbali pasipo kuingilia uchaguzi kwa nmna yeyote ile ya kupendelea.

28. NAFASI YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI
Vyama vya wafanyakazi nchini kwa mudamrefu wamekuwa na umoja ambao umetishia sana kuleta mapinduzi kwa kuiangusha serikali ya chama cha mapinduzi, na yawezekana mwaka huu ukawa ndio mwaka wao wa kuamua kufanya hivyo na yote haya nikutokana na kukosa stahiki zao za msingi na za lazima kwa muda mrefu huku maisha yao yakiendelea kuwa magumu na madeni ya malimbukizi yao ya mishahara ikiongezeka kwa kasi kubwa sana. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa chama cha WALIMU TANZANIA kinaidai sana serikali malimbukizo makubwa ya mishahafa ya wanachama wake(walimu) mbali na hayo pia mazingira mabaya ya kazi na malalamiko mengi mengi ndio yanayopelekea chama hicho kuhitaji mabadiliko makubwa ambayo wameshidwa kuyapata ndani ya serikali ya CCM.

Vyama vingine kama TUICO, Wafanyakazi wa Reli, Wastaafu wa EAC na kadhalika navyo vimekuwa na uchungu na hasira za muda mrefu na chama cha mapinduzi huku wakikumbuka namna ambavyo wazee wa Afrika Mashariki walivyopigwa mabomu na kumwagiwa maji ya kuwasha wakati wakidai haki zao.

29. WATANZANIA WALIOKO NJE YA TANZANIA(DIASPORA) HAWAITAKI CCM TENA
Mgombea Urais kupitia UKAWA, Mh. Edward Lowassa ameonekana kuungwa sana mkono na watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi huku wakilinganisha muda amabo CCM imkeaa madarakani na maendeleo kiduchu yaliyoko nchini hivyo watu hawa ambao kwa muda tofauti tofauti wamekuwa wakitumia mitandao kuikejelei serikali ya CCM pamoja namgombea wake wameonekana kuwa wanahitaji sana mabadiliko na wamekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wenzio walioko nchini Tanzania kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuiondoa CCM madarakani huku wengi wamekuwa wakisema ya kuwa ukitaka kujua umasikini na uozo wa uongozi wa Tanzania basi nenda ng'ambo ukaone.

30. HALI YA KISIASA ZANZIBAR
Kutokana na maoni yao yaliyokuwemo katika katiba mpya kupingwa na kupindishwa kabisa na serikali ya chama cha mapinduzi, wananchi wengi wa Zanzibar wamekuwa na shauku kubwa ya kuichagua UKAWA kwa mgombea yeyote yule ili tu kutimiza azma yao ya kuwa na serikali tatu huku Zanziabar nayo ikiwa huru. Jambi hili limekuwa kubwa sana kwa Zanziabar ndio jambo kubwalitakaoamua mshindi wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu huko visiwani Zanzibar hivyo, Magufuli hana nafasi ya kupata kura za kutosha kutoka visiwani humo kwani wananchi walio wengi wameamua kuipinga CCM.

31. JUMUIYA ZA KIMATAIFA
CCM imekuwa ikifahamika kwa muda mrefu kwa kutumia mabavu katika kutangaza matokeo hasa kwakua mra nyingi kama sio mara zote kwa sababu ya tabia ya wizi wa kura walionayo. Lakini mwaka huu hali ni tofauti kwani Jumuiya za Kimataifa ikiwemo ICC, UN(UNDP), EU, AU, SADC pamoja na nchi kubwa duniani hasa wahisani wakubwa kupitia balozi zake tayari wameshasema wanahitaji kuona haki ikitendeka na watashiriki kama wasimamizi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Kadharika nchi jirani kama vile Rwanda tayari Rais wake Mzee Paul Kagame ameshasema anategemea Kikwete kuonyesha ukomavu wa hali ya juu katika kuhakikisha hakuna uvunjifu wa demokrasia ambayo yeye amekuwa akiihubiri katika Ukanda huu wa Maziwa Makuu yote haya ikiwa ni baada ya kuona kuwa tayari chama Tawala yaani CCM imekumbana na upinzani hatari unaopelekea kukiondoa chama hicho madarakani.

Kwa hoja hii tayari CCM haina tena nafasi nyepesi ya kufanya ule wizi wa wazi wa kuiba kura na kuanzisha vurugu za makusudi kisha kuwapiga wananchi na kusingizia vyama vya upinzani ndio waanzilishi wa uvunjifu wa amani.

MWISHO.
Watanzania wenzangu, ni aibu, dharau sana na kufanywa wajinga na wapumbavu kama ambavyo Marais waliopita walivyoweza kutuita kuona ni miaka 54 ya Uhuru mpaka sasa tukiwa chini ya Chama Cha Mapinduzi, chama ambacho kimeshindwa kabisa kuletea maendeleo yanayoshabihiana na rasilimali zilzipo nchini lakini kikiendekeza watu wachache wezi. Ni aibu mpaka leo watanzania wanaambiwa kuwa wanatakiwa kuchangia ujenzi wa maabara na wanafurahia, ni aibu sana mpaka leo watanzania wanaambiwa wachangie ujenzi wa hospitali na zahanati za afya na wanafurahia, ni aibu sana mpaka leo hii barabara inakuwa ni sehemu ya ilani ya uchaguzi ya chama kilichoongoza kwa zaidi ya miaka 54 kwa mfululizo.


Taifa limekosa viongozi bora wenye kuumizwa na maisha magumu ya watanzania, wenye kuona hali ngumu za maisha ya watanzania basi ni maisha yao pia, taifa limekosa viongozi wenye maono na wenye kusimamia vizuri rasilimali tele zilizopo ili kuwaletea maendeleo watanzania ambao ndio wamiliki wa rasilimali za nchi hii.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu wabariki Watanzania wote wanaotaka Mabadiliko.
 
ye anajua tu kuongelea masuala ya barabara mambo mengine kama siasa za kimataifa atakuambia 'me am biziii'... muulize sadam rais wa kuwait
 
Khaa!! Pitia na hii kidogo :glasses-nerdy:

Askofu kilaini atoa sifa nane (8) za rais chaguo la mungu 2015-2020!
watanzania habari za jioni,
siku ya trh 26-09-2015 askofu wa kanisa katoliki ndg kilani atoa sifa nane za mtu ambaye atakua rais wa tanzania awamu ya tano chaguo la mungu.
Akiyasema hayo gazeti la nipashe na vyombo mbalimbali vilinukuu maneno yake. Hivyo hapa nawaletea maono ya askofu kilaini;
zifuatazo ni sifa nane kwa mujibu wa askofu kilaini;

1. Mwadilifu
amesema nchi yetu ilipofika inahitaji mtu/rais ambaye anao uadilifu wa kweli na wa hali ya juu ili kuleta uongozi uliojaa uadilifu na nidhamu katika kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika na kufurahia nchi yao na mambo yake yote.

2. Uchapa kazi kwa vitendo
nchi hii inayo rasilimali za kutosha ambapo zikitumika vyema watanzania watanufaika na maisha yao yatakuwa pazuri sana zaidi ya sasa hivi. Ili kuhakikisha hayo ni lazima tupate kiongozi mchapa kazikwa vitendo na hata tukimuuliza umefanya nini anao uwezo wa kutuambia nimefanya hili na lile.

3. Mtekeleza majukumu yake ipasavyo
kiongozi ambaye atakua amiri jeshi mkuu wa tanzania anapaswa kuwa ni mtekeleza majukumu anayopewa na yanayomhusu ipasanyo, kama umekabidhiwa jambo unalifanya kwa ukamilifu wake. Hivyo tanzania ya sasa haihitaji tena wajanjajanja ambao wanachekea watu huku hakuna utekelezaji wa majukumu yao ipasavyo.

4. Mzalendo
hakuna maendeleo tuyatakayo hapa nchini kwasababu viongozi wetu wengi sio wazalendo wa kweli, wanayoyasema hawayaishi, wanayoyahidi hawayatekelezi kisawasawa. Hivyo basi 2015-2020 inahitaji kzalendo wa kweli na naamini mpaka sasa tumeona nani mzalendo anayezungumza kwa ukali na umakini kuwa atawasaidia watanzania na atapambana na ufusadi, wezi na kushughulika na wabadhilifu wa mali na uchumu wa nchi.

5.mcha mungu
katika utumishi uliotukuka na katika utumishi uliojaa haki na utawala makini na bora ni lazima tupate rais ambaye anyo hofu ya mungu na nimcha munngu kabisa, tumepata kuwa na viongozi ambao hawana utii kwa mungu na wakaharibu utumishi. Mwaka huu watu wanaoigiza kuwa niwacha mungu wanapaswa kukataliwa kaibisa na kuwaa kura watu wanaoonekana kuwa na hofu ya mungu.

6.mpenda watu
kupendwa na watu pia ni sifa muhimu sana, ila uwe unapendwa sio kwasababu unawapa rushwa, sio kwasababu uliwaandaa muda mrefu wakupende, sio wakupende kwasababu umewafanya watamani kumkomesha mtu au chama fulani. Iwe wanakupenda kwasababu ni mtendaji wa kazi, kwasababu unachukiwa wezi mafisadi, uwe wanakupenda kwasababu hupendi mchezo ktk kazi, iwe wanakupenda kwasababu ya uzalendo wako. Nawe pia uwe unawapenda kwasababu unayapenda maelendeleo yao na uwe unawapenda kwa kuwatendea kazi ipasavyo na sio kuwaibia mali zao.

7. Asiwe boss kwa wananchi
rais ajaye hapaswi kuwa boss/ meneja wa wananchi wake. Hii ni tabia chafu kwa rais kuwa au kujifanya boss au meneja wa taifa zima. Bali rais anapaswa awe mtumishi wa watu, achukue muda wake mwingi kuwazungukia wananchi katika maeneo yao kukagua shughuli za maendeleo na kushiriki pia, hivyo lazima uwe mkakamavu wa mwili na akili.

8.ujasiri wa kuwakemea wasio waadilifu
rais wa tanzania 2015-2020 anapaswa kwa nguvu zote awe mjsiri wa kukemea na kuwaonya hata kuwachukulia hatua viongozi na watanzania wasio waadilifu. Ni lazma afanye hivyo kwa lengo la kujenga nchi yetu katika hali ya uadilifu ili kuimarisha umoja,mshikamano,na ushirikiano hata usawa na haki.na tayari mmeshaona kiongozi mwenye ujasiri wa kufanya hivyo, na hata anayekerwa na wasio waadilifu.
Kwa kuzingatia hayo tutakuwa tumepata kiongozi chaguo la mungu 2015-2020, na lazma tutampata.

Hayo ndio maono na maoni ya askofu kilaini
 
Umenena mkuu na umemaliza kabisa na huo ndiyo ukweli!!

Kwa gharama tu mimi naamini CCM tayari wameshatumia zaidi ya 300bn na hizi ni fedha za hazina yetu kuu wala wasitudanganye!!

Na hili CCM wanatuudhi kwa sbb ktk ofisi za serikali kwa sasa hali ni ngumu, mambo hayaendi kwa sbb hakuna fedha kwa kuwa zote wamezichukua na kujigawia ktk kampeni zao!!
 
Mimi sababu za kushindwa kwa Lowassa walinipa hao hao wanaomnadi leo na ni nyingiiiiiii!
 
Ongeza zifike Mia.
Utake uctake magufuli ndio rais wa tano wa jamuhuri ya muungano wa tanzania.

Hizi Kauli zenu zitawarudisha wafu Nyumbani... Unaposema Utake Usitake Maana Yake Nn ..

Kura Zikiamua Zimeamua . hiyo Utake Usitake Utasababisha Amani Isiwepo....
 
Umesahau No 32. Madhehebu yote ya waumini wa kilokole awaitaki kabisa ccm. Ref jinsi walivyo toswa bunge la katiba na mkwere
 
ImageUploadedByJamiiForums1443810287.388910.jpg
 
Ongeza zifike Mia.
Utake uctake magufuli ndio rais wa tano wa jamuhuri ya muungano wa tanzania.
Kwangu naongezea na hii iwe sababu ya 32 ya kuitosa CCM, kiburi. Mwalimu Nyerere alituasa kuhusu mtu ama chama kukaa madarakani kwa muda mrefu, kwamba hujemga kiburi. Kauli ya utake usitake ni kauli ya kifedhuli na kishenzi isiyo na nafasi katika karne hii na moja kwa moja sitakosea nikiihusisha kauli hii na hulka ya Magufuli ya kukurupuka. Kiburi cha CCM kwa kutegemea nguvu za dola kuzima sauti ya UMMA lazima ilaaniwe na kila mpenda demokrasia popote alipo. Naviasa vyombo vyetu vya dola na hasa vya usalama na polisi vizingatie jukumu lao la kwanza kikatiba nalo ni kuwalinda raia wa nchi hii pamoja na mali zao bila kujali itikadi zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom