Kwanini Vatican haitambuliki na UN?

Kwanini Vatican haitambuliki na UN?

Hivi ni sababu gani inafanya nchi ya Vatican isitambulike kama nchi na Umoja wa Mataifa? Kuna nini hapo kimejificha?
Vatican ni mji Mtakatifu wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki , wenye hadhi ya nchi kimataifa na Balozi nchi zote duniani, hivyo ni dola isiyo na jeshi, polisi, sarafu, uhamiaji, mipaka wala passport!. Inatambuliwa kama nchi ndani ya nchi, yenye dola inayotambuliwa ni Italy. Vatican ni mji mtakatifu.

Kule UN utambuzi ni wa dola za Political tuu, Vatican sio nchi ya Political, ni mji mtakatifu, ndio maana hata Zanzibar haitambuliwi kimataifa!.

P
 
Vatikanil City ni taifa huru na pekee duniani ambalo limeamua kutokuomba uanachama UN. (Kumbuka kuwa mwanachama UN sio lazima).

Vatican City, pamoja na nchi nyingine ndogo za Ulaya kama Monaco, Andora, Liechtenstein na Malta ni nchi huru kabisa (sovereign states). Sema kutokana na udogo wao na maeneo yao kijiografia baadhi zina mikataba ya ushirikiano ya karibu sana na majirani zake kiasi kwamba watu hudhani ni nchi moja.

Mfano Vatican na Italy, Monaco na France, Liechtenstein na Switzerland n.k.

Vi nchi hivi vidogo vinashirikiana na hayo mataifa makubwa kwenye maeneo ya ulinzi, fedha, uhamiaji n.k.

Kwahiyo kwa kumalizia, Vatican City ni sovereign state, wao wenyewe ndio wameamua kutokuwa wanachama wa kudumu wa UN japo ni moja ya nchi waangalizi UN (observer state).

Maelezo zaidi soma the Lateran Treaty.
 
Vatican sio nchi ni mji Mtakatifu, wenye hadji ya nchi kimataifa na Balozi nchi zote duniani ila sio dola; hauna polisi, jeshi, sarafu, nchi yenye dola inayotambuliwa ni Italy. Vatican ni mji mtakatifu.

Kule UN utambuzi ni wa dola tuu, ndio maana hata Zanzibar haitambuliwi kimstaifa.

P
Sio kweli, sovereign state sio lazima uwe na jeshi na hivyo vingine.

Monaco hawana jeshi (wana mikataba ya ulinzi na Ufaransa) na ni nchi huru, mwanachama kamili ya UN tangu 1993!

Vatican City ni sovereign state according to international law. Ni wao wenyewe wameamua tena kwa hiyari yao kutokuwa wanachama wa kudumu wa UN.
 
Sio sahihi kuilinganisha status ya Zanzibar na Vatican City.

Zanzibar ni kama Wales, Scotland, Greenland n.k They are not sovereign states.
Kwa sheria za kimataifa, moja ya sifa za sovereign states ni kuweza kuingia mikataba na mataifa mengine huru (other sovereign states), Zanzibar kama ilivyo Scotland, Greenland n.k hawana mamlaka hayo. Mamlaka hayo yapo kwenye serikali za JMT, UK na Denmark respectively.
 
Vatican sio nchi ni mji Mtakatifu, wenye hadji ya nchi kimataifa na Balozi nchi zote duniani ila sio dola; hauna polisi, jeshi, sarafu, nchi yenye dola inayotambuliwa ni Italy. Vatican ni mji mtakatifu.

Kule UN utambuzi ni wa dola tuu, ndio maana hata Zanzibar haitambuliwi kimstaifa.

P
Mkuu vatcan Haina jeshi? Haina usalama wa taifa?
 
Back
Top Bottom