Kumekuwa na nadharia tangu enzi za Nyerere mpaka sasa kwamba ajira ni utumishi wa umma tu, kisa kikubwa eti kuna security.
Lakini ukiangalia wengi wa hao watumishi, ni watu wanaostruggle sana, angalia walimu, madaktari,wauguzi, nk. Asilimia 95 yao ni watu wanaoteseka na maisha.
Mshahara wa kawaida sana, wamejaa madeni , benki mpaka vikoba, hawana la maana. Lakini wanag'ang'ana tu. Mtu anasubiri kustaafu, ndio apate kihela labda cha kupumulia maana lazima atakuwa na madeni ya kutosha. Na atakufa siku si nyingi maana jua linakuwa lishazama.
Baadhi ya watumishi kwenye strategic positions ndio utawaona wananufaika na utumishi wa umma, mfano wale wa bungeni, baadhi ya wizara, mashirika na taasisi za umma. Na hao si wengi kama hawa wa kawaida.
Je, 2025 bado kuna watu wanaamini kuwa maisha ni kufanya kazi serikalini? Huu uoga utaisha lini?
Ukiangalia kwa jicho lingine utakuwa ni incompetence inawasukuma huko maana asilimia kubwa ya graduates hawana skills za kuajirika sehemu za maana. Wataharibu tu. International job market ipo kubwa sana lakini hutoona wanahangaika nayo kama ilivyo wenzetu wa Kenya au Wanigeria.
Je mpaka 2025 hii mentality ya kitumwa na ya ki coward inafaa?