Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Kwa Waziri aliyejiuzulu kwa kashfa ya ESCROW ACCOUNT ambapo mafisadi waligawana mabilioni ya fedha chafu kama njugu na kuzibeba kwenye lumbesa na visalfeti bado tunajiuliza hivi kuna tija ipi uongozi mpya unamwona muasisi huyu wa ufisadi wa kutisha bado ni lulu!
Bungeni wakati wa ESCROW ACCOUNT alitetea sana TANESCO lakini juzijuizi alipomtumbua kibosile wa Tanesco akadai utendaji wa Tanesco ni mbovu. Kauli hizi mgongano zinathibitisha ni tumbo lake tu Mheshimiwa huyu analihudumia.
Ikija masilahi ya wanyonge kwenye uwekezaji wa gesi alituona ni kuwauzia makabaila mbogamboga wala siyo kununua hisa na kunufaika moja kwa moja.
Sasa ana donge na TPDC kisa kampuni aitakayo ya kichina imepigwa stop kumilikishwa vitalu vya uchimbaji wa gesi na anajivika gwanda la mpambanaji wa ufisadi humo hata maisha yake yako hatarini.
Kwanza kabisa tuhuma za rushwa wamiliki wake ni TAKUKURU, lakini Mheshimiwa huyu hajawahi kuwaandikia ili wazifanyie Kazi.
Pili, hakuna sheria ya manunuzi inayompa mamlaka ya kushiriki au kushawishi au kutishia kampuni yoyote ile ipewe kazi serikalini.
Waziri siyo Mtendaji serikalini bali ni msimamizi tu.
TPDC inaona Mheshimiwa anakiuka sheria ya manunuzi lakini aliyemteua Muhongo kapiga ganzi.
Hivi uteuzi wa Muhongo kwenye baraza la mawaziri kunamnufaisha nani? Au ufisadi ndiyo kigezo cha kuwa Waziri? Kama ndicho basi futeni sheria inayounda TAKUKURU na mtangaze ufisadi ndiyo wasifu mpya Wa utaifa wetu.
Vinginevyo futa Kazi Muhongo na kuagiza TAKUKURU watoke kwenye lindo la usingizi mnono na wakchunguze mchakato mzima wa upatikanaji Wa wawekezaji kwenye uchimbaji wa gesi hapa nchini.

*KAMATI YA MAKONTENA YA MCHANGA WA MADINI*
Huu ni muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Mruma hii keo Ikulu!.
1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.
2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.
3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,
4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.
5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.
6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.
MATOKEO YA UCHUNGUZI
1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.
3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.
4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na thamaninya Bilioni 13.
4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.
5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha
6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,
7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka bilioni 261.5
Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.
8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.
9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.
10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.
MAPENDEKEZO YA KAMATI
1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi
2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini
3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.
4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia
5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.
6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.
7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.
8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.