Kwanini uteuzi wa Profesa Muhongo kwenye Cabinet unashusha hadhi ya aliyemteua!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Kwa Waziri aliyejiuzulu kwa kashfa ya ESCROW ACCOUNT ambapo mafisadi waligawana mabilioni ya fedha chafu kama njugu na kuzibeba kwenye lumbesa na visalfeti bado tunajiuliza hivi kuna tija ipi uongozi mpya unamwona muasisi huyu wa ufisadi wa kutisha bado ni lulu!

Bungeni wakati wa ESCROW ACCOUNT alitetea sana TANESCO lakini juzijuizi alipomtumbua kibosile wa Tanesco akadai utendaji wa Tanesco ni mbovu. Kauli hizi mgongano zinathibitisha ni tumbo lake tu Mheshimiwa huyu analihudumia.

Ikija masilahi ya wanyonge kwenye uwekezaji wa gesi alituona ni kuwauzia makabaila mbogamboga wala siyo kununua hisa na kunufaika moja kwa moja.

Sasa ana donge na TPDC kisa kampuni aitakayo ya kichina imepigwa stop kumilikishwa vitalu vya uchimbaji wa gesi na anajivika gwanda la mpambanaji wa ufisadi humo hata maisha yake yako hatarini.

Kwanza kabisa tuhuma za rushwa wamiliki wake ni TAKUKURU, lakini Mheshimiwa huyu hajawahi kuwaandikia ili wazifanyie Kazi.

Pili, hakuna sheria ya manunuzi inayompa mamlaka ya kushiriki au kushawishi au kutishia kampuni yoyote ile ipewe kazi serikalini.

Waziri siyo Mtendaji serikalini bali ni msimamizi tu.

TPDC inaona Mheshimiwa anakiuka sheria ya manunuzi lakini aliyemteua Muhongo kapiga ganzi.

Hivi uteuzi wa Muhongo kwenye baraza la mawaziri kunamnufaisha nani? Au ufisadi ndiyo kigezo cha kuwa Waziri? Kama ndicho basi futeni sheria inayounda TAKUKURU na mtangaze ufisadi ndiyo wasifu mpya Wa utaifa wetu.

Vinginevyo futa Kazi Muhongo na kuagiza TAKUKURU watoke kwenye lindo la usingizi mnono na wakchunguze mchakato mzima wa upatikanaji Wa wawekezaji kwenye uchimbaji wa gesi hapa nchini.

*KAMATI YA MAKONTENA YA MCHANGA WA MADINI*

Huu ni muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Mruma hii keo Ikulu!.

1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.

2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.

3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,

4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.

5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.

6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.

MATOKEO YA UCHUNGUZI

1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.

3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.

4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na thamaninya Bilioni 13.

4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.

5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha

6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,

7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka bilioni 261.5

Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.

8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.

9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.

10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.

MAPENDEKEZO YA KAMATI

1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi

2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini

3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.

4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia

5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.

6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.

7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.

8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.
 
Kwa Waziri aliyejiuzuru kwa kashfa ya ESCROW ACCOUNT ambapo mafisadi waligawana mabilioni ya fedha chafu kama njugu na kuzibeba kwenye lumbesa na visalfeti bado tunajiuliza hivi kuna tija ipi uongozi mpya unamwona muasisi huyu wa ufisadi wa kutisha bado ni lulu!

Bungeni wakati Wa ESCROW ACCOUNT alitetea sana TANESCO lakini juzijuizi alipomtumbua kibosile Wa Tanesco akadai utendaji Wa Tanesco ni mbovu. Kauli hizi mgongano zinathibitisha ni tumbo lake tu Mheshimiwa huyu analihudumia.

Ikija masilahi ya wanyonge kwenye uwekezaji wa gesi alituona ni kuwauzia makabaila mbogamboga wala siyo kununua hisa na kunufaika moja kwa moja.

Sasa ana donge na TPDC kisa kampuni aitakayo ya kichina imepigwa stop kumilikishwa vitalu vya uchimbaji wa gesi na anajivika gwanda la mpambanaji wa ufisadi humo hata maisha yake yako hatarini.

Kwanza kabisa tuhuma za rushwa wamiliki wake ni TAKUKURU, lakini Mheshimiwa huyu hajawahi kuwaandikia ili wazifanyie Kazi.

Pili, hakuna sheria ya manunuzi inayompa mamlaka ya kushiriki au kushawishi au kutishia kampuni yoyote ile ipewe kazi serikalini.

Waziri siyo Mtendaji serikalini bali ni msimamizi tu.

TPDC inaona Mheshimiwa anakiuka sheria ya manunuzi lakini aliyemteua Muhongo kapiga ganzi.

Hivi uteuzi wa Muhongo kwenye baraza la mawaziri kuna mnufaisha nani? Au ufisadi ndiyo kigezo cha kuwa Waziri? Kama ndicho basi futeni sheria inayounda TAKUKURU na mtangaze ufisadi ndiyo wasifu mpya Wa utaifa wetu.

Vinginevyo futa Kazi Muhongo na aagiza TAKUKURU watoke kwenye lindo la usingizi mnono na wakchunguze mchakato mzima wa upatikanaji Wa wawekezaji kwenye uchimbaji wa gesi hapa nchini.

Hata sijakuelewa Mkuu labda wenzangu.. Unajua tujifunzeni kuanzisha majungu ili iwe ni vigumu kutofautisha kati ya ukweli na uongo.
vinginevyo urudi shuleni tena ukajifunze jinsi ya kuwa mnafiki... Kwa taarifa yako muhongo ni kila kitu na tunamhitaji zaidi ya unavyofikiria.umeme Rea kila kona, Watoto wanakwenda kusomea menejimenti na Usimamizi kwa ujumla wa gesi, makaa ya mawe na madini ya jasi yananufaisha wachimbaji wadogo,

Hakuna kukatika katika umeme hovyo, wala Mgao... Na mengine rundo.. Sasa mzee utabakia humu JF tu na baadhi ya wafia dini wa Ufipa.. Ila wazee na vijana vijijini wanamwona kama mungu wao..
 
Hata sijakuelewa Mkuu labda wenzangu.. Unajua tujifunzeni kuanzisha majungu ili iwe ni vigumu kutofautisha kati ya ukweli na uongo.vinginevyo urudi shuleni tena ukajifunze jinsi ya kuwa mnafiki... Kwa taarifa yako muhongo ni kila kitu na tunamhitaji zaidi ya unavyofikiria.umeme Rea kila kona, Watoto wanakwenda kusomea menejimenti na Usimamizi kwa ujumla wa gesi, makaa ya mawe na madini ya jasi yananufaisha wachimbaji wadogo, Hakuna kukatika katika umeme hovyo, wala Mgao... Na mengine rundo.. Sasa mzee utabakia humu JF tu na baadhi ya wafia dini wa Ufipa.. Ila wazee na vijana vijijini wanamwona kama mungu wao..
Hujaelewa au umeelewa na hukubaliani na hoja. Mnafiki ni yule anadai hajaelewa kumbe ni povu tu linamtiririka baada ya kuelewa
 
Hata sijakuelewa Mkuu labda wenzangu.. Unajua tujifunzeni kuanzisha majungu ili iwe ni vigumu kutofautisha kati ya ukweli na uongo.vinginevyo urudi shuleni tena ukajifunze jinsi ya kuwa mnafiki... Kwa taarifa yako muhongo ni kila kitu na tunamhitaji zaidi ya unavyofikiria.umeme Rea kila kona, Watoto wanakwenda kusomea menejimenti na Usimamizi kwa ujumla wa gesi, makaa ya mawe na madini ya jasi yananufaisha wachimbaji wadogo, Hakuna kukatika katika umeme hovyo, wala Mgao... Na mengine rundo.. Sasa mzee utabakia humu JF tu na baadhi ya wafia dini wa Ufipa.. Ila wazee na vijana vijijini wanamwona kama mungu wao..

vipi bado una jeuri ya mkutetea Prof. Muhongo??
 
Rais wa Nchi hii Dr John Magufuli anapokea ripoti ya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini ambao husafirishwa nje ya nchi makontena kwa makontena. Ripoti hii itatoa dira na mwelekeo wa miongozo inayotakiwa kufuatwa na kufanyika kunusuru rasilimali zetu kwa maslahi ya watz.

FUATILIA UZI HUU KWA LIVE UPDATES PIA FUATILIA KUPITIA TBC1
------------

--Updates..

3: 30 Asubuhi: Shughuli imeanza kwa wasanii kutumbuiza wimbo wa uzalendo.

Sasa Katibu Mkuu Ikulu, Mheshimiwa Balozi Kijazi anazungumza kwa utangulizi huku akibainisha kuwa ripoti inayosomwa leo ni ya Kamati ya Kwanza iliyoundwa na Rais na kueleza kuwa ripoti ya 2 itafuata siku zijazo.

Baada ya utangulizi, anamkaribisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof Mruma ili asome ripoti kabla ya kuikabidhi kwa Rais Magufuli.

Prof Mruma: Kamati hii baada ya kuteuliwa, tulianza kwa kuandaa mpangokazi, kupitia mafaili yote ya usafirishaji, kutembelea maeneo yote yenye makontena ili kuyachunguza na kuweza kuchukua sampuli. Katika kuchukua sampuli tulifuata taratibu za kisayansi ili kufanya sampling na kufanya uchunguzi wa materials zote.

Matokeo ya Uchunguzi

- Jumla ya makontena 277 yalifanyiwa uchunguzi.

- Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya madini ya dhahabu, copper, chuma na mengine ndani ya makenikia(mchanga) yaliyobebwa kwenye makontena.

Taarifa kutoka kwa wazalishaji na wakala wa serikali (TMAA);

Dhahabu tani 1.2 = Bilioni 7.5bilioni
Silver gramu 202.7 - 351/tani (iliripotiwa nusu tu ya gramu zilizomo kwenye kila kontena)
Sulphur 16.7 - 50.8/tani (kwa tani zilizopatikana 2161 kwa makontena 277)= Bilioni1.4
Chuma 13.6 - 30.6/tani (kwa kontena 277) = Bilioni 2.3
Copper 17.6 - 23.3/tani (kwa kontena 277) = Bilioni 13.6

(Reserved space for more data)

THAMANI YA JUMLA

(reserved space for data)

- Kamati imebaini kuna upotevu mkubwa wa mapato ya serikali ktk ukokotoaji wa mirabaha.

- Bahati mbaya madini haya (sulphur na chuma) hayahusishwi ktk kukokotoa mirabaha. Ni Silver, Shaba na dhahabu pekee ndio yanayoripotiwa.

- Kuna madini mkakati(strategic metals) ambayo yanalingana na dhahabu, hayakuhusishwa pia japo yanahitajika sana duniani kwa sasa na yana thamani kubwa.

Yote yalikuwa na thamani ya bilioni 129.5=261.5

(Reserved space for more data)

Mhe Rais, hivyo ndivyo viwango na mapato tuliyopoteza.

Pamoja na kuchunguza makenikia, kamati ilichunguza pia shehena ya mbale za shaba (38.9g kiwango cha dhahabu)

Katika kufuatilia utendaji wa TMAA, Kamati ilibaini kuwa;

- Haifungi utepe wa kudhibiti makontena (ufungaji unafanywa wakati kusafirisha tu). Hii inatoa fursa ya watu kuchezea viwango. Tunapendekeza wakala wafunge utepe mwanz

- Uwezo wa scanner inayoangalia yaliyomo kwenye makenikia ndaniya kontena ni hafifu. Mfano tulijaribu kuficha vipande vya chuma, scanner haikuona. Hivyo mtu akiamua kuficha vitu kwenye makenikia haviwezi kubainika.

Mapendekezo ya Kamati

1. Isitishe usafirishaji wa mchanga mpaka mrabaha stahiki utakapolipwa serikali kwa kuzingatia thamani halisi ya makenikia.

2. Ujenzi wa *** unafanyika haraka ili makenikia hayo yasafirishwe ndani ya nchi ili madini yote yaweze kufahamika na kutozwa mrabaha sahihi.

3. Tepe za udhibiti zifungwe mara moja ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanyika wakati wa kuchukua sampuli.

4. TMAA ipime metali zote zilizomo kwenye makenikia ili kupata thamani halisi ya metali hizo (mrabaha).

5. Kutokana na kuwepo madini mbalimbali kwenye Mbale. TMAA ipime viwango vya metali zote muhimu ktk mbale zinazosafirishwa bila kujali kilichoandikwa kwa msafirishaji.

6.

7. Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wale wa wizara inayohusika.

8. Pamoja na vyombo vya uhakiki, serikali iweke mfumo wa kushtukiza ili kuepuka watendaji kufanya kazi kwa mazoea.

9. Serikali itumie wataalamu wa mionzi ili kufunga scanner zenye uwezo sahihi (kwa ajili ya makenikia na mizigo mingine).

Mhe Rais, nichukue fursa hii kukushukuru kwa kuwa na imani na sisi na kututeua kutekeleza jukumu hili muhimu ili kuepusha nchi kupata hasara. Ni imani yetu kuwa matokeo ya uchunguzi hii yatatoa msaada mkubwa kwa serikali.

Shukrani kwa vyombo vya ulinzi na usalama, Wakala wa Jeolojia (Maabara mkemia mkuu), TPA, TRA, TMAA, Vyuo vya UDSM na MUM(kwa kutoa wataalamu).

Kamati hii iko tayari kutoa ufafanuzi pale utakapohitajika. Asante.
----------------

Prof. Mruma amemaliza kusoma ripoti hiyo na sasa zoezi la kumkabidhi Rais linaendelea.

========
Magufuli: (Anatambulisha wote waliohudhuria kulingana na itifaki), Tulitumia vifaa vyote katika ulinzi lakini wapo waliojitokeza kutaka kuingilia uchunguzi huu na bahati nzuri majina yote tunayo, wapo wengine mnawajua wenyewe wakibwatuka wengine kwenye mitandao, wamepewa fedha.

Ndugu zangu tuko kwenye vita na vita ya uchumi ni mbaya sana, mabilioni ya fedha haya ambayo nchi yetu imepoteza, dhahabu tani tani 7.8 hadi 13.16 kwa kontena 277. Tani 15.5 ni malori mawili na land rover moja. Malori mawili ya tani 7 yanaleta tani 14, labda na pick up zote umezipaki pale na hio ni kwa makontena 277.

Kuna tume inayotaka kujua ni makontenayanasafirishwa mangapi, haraka haraka ni makontena 250 na 300 kwa mwezi, kwa mwaka zaidi ya makontena 3600.

Ni kitu cha kuumiza mno na kwa hili watanzania wote tushikamane, hospitali watu wanakosa madawa, mashuka, shule watu wanakosa madawati, hela za treni mpaka tukope kumbe kuna hela zinamwagika hapa.

Nilimfukuza katibu mkuu wa nishati na madini alipoulizwa na kamati ya wabunge kiasi cha dhahabu kilichopo, ni aibu kwa mtu aliesomeshwa na watanzania.

Bilioni 676 hadi trilioni 1.5 tunzazipoteza watanzania, madini mengine hawakujali hata kuyarekodi(Nipe ile document). Tunaweza tukaona kwa miaka kwa 17, tulipaswa kuwa donor country kwa vitu tulivyopewa na Mungu.

Hauwezi ukashangaa katika wizara hizi ndio nilichagua watu waziri wa kuziendesha, kuna tume iliundwa miaka ya nyuma, walidanganya kuna smelter ziko nchi fulani, walipoenda wakaishia hotelini. Smelter sio tatizo kwenye ripoti, inaonyesha kampuni nyingi zinazoweza kuuza smelter, viongozi hawakuchukua juhudi za kununua smelter.

Sera ya taifa ya madini ya mwaka 2009 inasema haja ya kununua smelter, viongozi wa hizo wizara hawakufanya juhudi, kwanini TMAA wapime kidogo halafu wanakuja kuweka tu seal wakati hujui kilichowekwa ndani, kwanini?

Kwanini wasimamizi wasimamizi wa TMAA ambao ni wizara hawakushtukia? Kwanini bodi ya TMAA haiwakushtukia? Inawezekana nikajiuliza maswali mengi majibu yasipatikane. Inawezekana yakaletwa na tume nyingine, nilienda na wenzangu kuteta kidogo, Haiwezi kupita hivi hivi.

Ripoti hii ikipita hivi hivi tutakuwa watu wa ajabu sana, tutafanya kitu, tunasubiri ile ripoti nyingoine.

  1. Mapendekezo yote ya tume nimeyakubali
  2. Bodi ya TMAA nimeivunja Rasmi
  3. Namsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TMAA na wafanyakazi waanze kuchunguzwa na vyombo vya dola
  4. Shughuli zote zinazohusu madini, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vianze kutumika sawasawa.
Wizara wameshindwa kusimamia TMAA, ujenzi wa Smelter pia imeshindwa kuweka utaratibu wa kufatili haya makenikia, mbona huwa wanaenda Ulaya? Kamishna madini anafanya nini? Waziri anafanya nini?

Vyombo viwachunguze watendaji wa wizara ya madini wanaoshughulia

Nampenda sana Prof Mhongo lakini pia ni rafiki yangu, lakini kwenye hili, ajifikirie, ajitathmini na bila kuchelewa nilitaka aachie madaraka.
 
Aliwafanyia roho mbaya wenzake toka Tpdc, tanesco kina mramba nk akasahau kua karma has no menu, you are served what you deserve.

Hii iwe red flag kwa DAB kua pamoja na Magu kumpenda sana Muhongo pamoja na kushiriki wizi wa pesa za umma za escrow mwisho wa siku numbers dont lie.
 
Hata sijakuelewa Mkuu labda wenzangu.. Unajua tujifunzeni kuanzisha majungu ili iwe ni vigumu kutofautisha kati ya ukweli na uongo.vinginevyo urudi shuleni tena ukajifunze jinsi ya kuwa mnafiki... Kwa taarifa yako muhongo ni kila kitu na tunamhitaji zaidi ya unavyofikiria.umeme Rea kila kona, Watoto wanakwenda kusomea menejimenti na Usimamizi kwa ujumla wa gesi, makaa ya mawe na madini ya jasi yananufaisha wachimbaji wadogo, Hakuna kukatika katika umeme hovyo, wala Mgao... Na mengine rundo.. Sasa mzee utabakia humu JF tu na baadhi ya wafia dini wa Ufipa.. Ila wazee na vijana vijijini wanamwona kama mungu wao..
Mkuu njoo huku tafadhali sana
 
We jamaa uliyeanzisha huu uzi nakupa pongezi zangu.
Mungu akubariki uendelee hivi japo kuna watu walikudharau kwa maoni yako halafu Leo yamekuwa kweli.
Huyo KANYAMA anatakiwa aje kuomba radhi hapa
 
Hapa ndipo unapata kujua kuwa 'it's a home of great thinkers' ...ningekuwa mamlaka iliyompeleka mwanzilishi wake Mahakani ningefuta kesi!
 
Hata sijakuelewa Mkuu labda wenzangu.. Unajua tujifunzeni kuanzisha majungu ili iwe ni vigumu kutofautisha kati ya ukweli na uongo.vinginevyo urudi shuleni tena ukajifunze jinsi ya kuwa mnafiki... Kwa taarifa yako muhongo ni kila kitu na tunamhitaji zaidi ya unavyofikiria.umeme Rea kila kona, Watoto wanakwenda kusomea menejimenti na Usimamizi kwa ujumla wa gesi, makaa ya mawe na madini ya jasi yananufaisha wachimbaji wadogo, Hakuna kukatika katika umeme hovyo, wala Mgao... Na mengine rundo.. Sasa mzee utabakia humu JF tu na baadhi ya wafia dini wa Ufipa.. Ila wazee na vijana vijijini wanamwona kama mungu wao..
KANYAMA are still there? If so, Hebu fanya uungwana kwa kumuomba radhi ndugu Rutashubanyuma kupitia uzi huu huu!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom