Funa the Great
Senior Member
- Aug 1, 2022
- 159
- 271
Unapopanga mipango yako ya safari basi mkoa wa Tanga usiache kuuweka kwenye orodha yako. Mkoa wa Tanga umejaaliwa kuwa na mandhari mazuri na yenye kuvutia watembezi wengi wanaotembelea eneo hilo. Kuna vivutio mbalimbali vya utalii vyenye kukufanya usijutie maamuzi yako ya kuvitembelea vivutio hivyo.
1. Hifadhi ya taifa SAADAN.
Hii ni hifadhi ya Taifa ambayo ina sifa za kipekee. Ni hifadhi inayotambulika kwa kuwa na mandhari ya majini na nchi kavu (Hifadhi iliyoungana na Bahari). Shughuli unazoweza kuzifanya, kuona wanyama, Kuogelea, Kupanda boat, camping, uvuvi na shughuli nyinginezo.
2. Msitu wa Magoroto (Magoroto forest).
Huu ni msitu unaopatikana mkoani Tanga. Ni miongoni mwa msitu uliobarikiwa kuwa na mandhari adhimu ya kuvutia kiasi kwamba wageni wengi hupendelea zaidi kutembelea eneo hilo. Huko utakutana na maporomoko ya maji, eneo lililozungukwa na maji na kuunda bwawa ambalo ni kivutio kwa watalii wengi sana. Shughuli unazoweza kuzifanya, Kuogelea, kupanda mlima, camping, uvuvi, kupanda boat, utalii wa kuendesha baiskeli/Pikipiki zenye miguu minne n.k
3. Mto Pangani na Wami
Hii ni mito mikubwa inayopatikana Tanga inayomwaga maji yake ndani ya Bahari ya hindi.
4. Mapango ya Amboni (Amboni caves).
Mapango haya ni makubwa yenye uwazi mkubwa ndani yake unayoweza ukaingia ndani yake na kushuhudia mambo mbalimbali ikiwemo michoro ya kale iliyochorwa pembezoni mwa kuta za mapango hayo.
5. Milima ya Usambara
Hii ni miongoni mwa milima tofali inayopatikana ukanda wa Afrika mashariki hususani mkoa wa Tanga. Ni milima inayovutia wageni wengi kutokana na kuwa na mandhari mazuri yenye kuvutia. Ina eneo maalumu kwa ajili ya kutazama maeneo jirani (view point).
Unaweza ongeza na mengine unayoyafahamu.
Kwa huduma za Safari za kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania Wasiliana nami +255622174613.
Safari za Kiofisi, marafiki, familia, shule/vyuo, taasisi/kampuni n.k