kwanini unapenda kumuhisi vibaya mwenzako?

Ngomo

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
200
95
kuna kitun kinacho nitatiza hasa katika mahusiano. utakuta kama mmekaa na mke wako au mme wako kwa muda mrefu bila kugombana wala kufumaniana , lazima ataanza mmoja kutafuta visa vya bila mpango eti anamhisis mwenzake anatoka nje. Njia ni kuhakikisha kama mwenzake ni mwaminifu. hii imekuwa kero kwa watu ambao ni waaminifu na wastaarabu . Nauliza kwanini umuhisis vibaya mwenzako?
 
Huwezi kuhisi mke/mume anatoka nje kama hakuna viashiria vinanyo onyesha hivyo. Ukiona mtu anamhisi mwenza wake anatoka nje bila kuwepo na viashiria ujue yeye ndiye anayetoka nje na anaogopa mwenzake asije fanya kama anavyofanya. Kumbuka suala ya kutoka nje ni hatari sana katika mahusiano, huwezi kumhisi mwenzio anatoka nje bila kuwa na uhakika vinginevyo utakaribisha mgogoro usio kuwa na maana. Hakuna mtu anayependa mgovi ndani ya ndoa kwa sababu migogoro ya ndoa ina mateso makubwa kwa wahusika hivyo siku zote wanandoa wangependa wasigombane maisha yote japo ni vigumu sana kuwa hivyo.
 
Ukiwa na INFERIORITY COMPLEX lazima utakuwa unamuhisi mwenzako vibaya au kama unafanya mabaya basi lazima utahisi kuwa na mwenzako anafanya mabaya kama yale unayofanya wewe
 
Ukiwa na INFERIORITY COMPLEX lazima utakuwa unamuhisi mwenzako vibaya au kama unafanya mabaya basi lazima utahisi kuwa na mwenzako anafanya mabaya kama yale unayofanya wewe

ninakubaliana na wewe asilimia mia m2 mzma na kwasababu hyo ndo unakuta ndoa nyng znakuwaga kwny migogoro ya namna hyo
 
Back
Top Bottom