Hofu ilikuwa kubwa nilipo mdogo,nikisikia jirani kafariki/mtu nnae mfaham,aisee nilikuwa naogopa kuingia ndani nikiwa peke yangu,yaan hata chumba nilikuwa nakiogopa,hata nikiingia kulala nilikua sipati usingizi niliouzoea,
waswahili wanasema kifo ukiskie kwa mwenzako,kikiwa kwako bwana weee heee.
Mzee alifariki nikiwa kijana,kwanza kuhs hof sikuwanayo kabisa,nilpo pokea taarifa nilikuwa kama zuzu,kulia silii kucheka sicheki,sina huzuni,sina furaha.baadae sasa..,,aisee kooni nilibanwa na uchngu,hta nikinywa maji hayapiti vyema,wala hayafuti maumivu kooni, ulichukua muda kutoweka,tumbo liliuma si la taifodi wala njaa,wala hamu ya kula sikupata.
Aisee kweli kufiwa usikie kwa mwenzako.Chaa ajabu hofu ya maiti wala sikua nayo,kama ambavyo zamani nilikuwa nikiogopa,
Kaburi nilisimamia mpaka likakamilika hata hamu ya kumbeba na kumpleka mazikon nilitaka nishiriki kubeba lkn nilishindwa kwa kufaham sitapata fursa kwa namna moja ama nyngne,
Yaani hapo sasa ndo nilijua umuhimu wa Baba.
Mpaka sasa hofu huwa sina,na usngzi nauchapa kama kawa hata kama nikiona maiti iliyokatika kichwa kule..utumbo palee,,ubongo kulee,walaaaaaa.