Kwanini Unaamini Mungu yupo?

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Unajua wengi tumekua na kukuta utaratibu ambao umewekwa na walitutangulia.
Wengi tumedumisha imani ambazo tumezikuta mwenye jamii yetu.

Hivi ulishawahi jiuliza kwanini www ni dini hiyo unayoiamini?

Je unahisi km ungezaliwa dini nyingine ungebadili?

Je mpaka sasa unaamini dini yako ndio sahihi? Kwanini?

Je Kitu gani hasa kinakufanya uamini Mungu yupo?

Cc Kiranga, Al-Watan, Apollo, ONTARIO Jimena
 
Ukiangalia jinsi mambo yalivyo kwa undani,kuhusu miti,wadudu,wanyama,ndege,binadamu,bahari,anga,upepo,madini nk...utagundua kua Mungu hayupo kabisa

Kama Mungu yupo inabidi aseme yeye chanzo chake ni nini?

Mana mpaka leo...watu wa dini hawajui Mungu/Allah alitoka wapi,lakini pia wanasayansi nao hawajui chanzo cha sayari na nyota na viumbe vingine.

Kwa ufupi mpaka sasa hakuna taarifa sahihi kuhusu Mungu na Dunia
 
Unajua wengi tumekua na kukuta utaratibu ambao umewekwa na walitutangulia.
Wengi tumedumisha imani ambazo tumezikuta mwenye jamii yetu.

Hivi ulishawahi jiuliza kwanini www ni dini hiyo unayoiamini?

Je unahisi km ungezaliwa dini nyingine ungebadili?

Je mpaka sasa unaamini dini yako ndio sahihi? Kwanini?

Je Kitu gani hasa kinakufanya uamini Mungu yupo?

Cc Kiranga, Al-Watan, Apollo, ONTARIO @jimeena
Mungu yupo kwa ushahidi huu wakimazingira uwepo wa mbingu na ardhi, usiku na mchana, mke na mume, majini na nnchi kavu, wanyama na mimea, ndege na wadudu, wanaadam na majini. Ushahid Surat n'nabai (78:8) m/mungu anasema "na nimekuumbeni kwa jozi" hakika ni ushahidi tosha kuwa sote tumetoka kwa Allah.

Kuhusu yy kama tunataka kumjua zaid, Surat Al-iqlas sura ya 112 m/mungu anasema "yy ni wapekee, yy ndio mkusudiwa, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana mfanoe", kumbuka Qur'an an ni ujalizo wa Taurat, Zaburi na Injili vyote ni vitabu vya mungu vilivyo teremshwa kwa mitume wake Daud, Mussa, Issa, a.s na mtume Muhammad s.a.w iwe muongozo kwa wanaadam huwez letwa duniani bila muongozo, kama unapo nunua gari au chombo chochote cha electronic utapewa muongozo vip utumie so Allah ndio katuletea hii miongozo hata ukipinga mungu hayupo utashindwa pinga maut basi kubali mungu yupo na kuna maisha baada ya maut wabilah tawfiq m/mungu mjuzi zaid.
 
Kwanini unaamin uwepo wa upepo umeshawahi kuuona??
Kwanini unaamini uwepo wa kujaa na kupwaa kwa maji ya bahari
Kwnn unaamin kua ipo siku utafufuka na ulipwe kwa ulilolitenda duniani?? Nani atakuhukumu kama sio mungu??
 
!!!!!
hivi kwamfano binadamu akituma chombo anga za mbali sana hlf asiweke kitu chochote kitakachotambulisha kuwa hicho kifaa kimetengenezwa na binadamu kwa bahati nzuri au mbaya kifaa hicho kikashikwa na viumbe wengine huko anga za mbali je,hao viumbe watajua kuwa kifaa hicho kimetengenezwa na binadamu..?
Viumbe wengine!!!kina nani hao? Me najua dunia ndio sayari inayowezesha viumbe kuishi sababu kuna uhai. Hao viumbe wengine mi siwajui zaidi ya kusoma dhana za kufikirika, Hivyo swali lako ni imagination na unaweza kujijibu kwa kuimagine
 
Viumbe wengine!!!kina nani hao? Me najua dunia ndio sayari inayowezesha viumbe kuishi sababu kuna uhai. Hao viumbe wengine mi siwajui zaidi ya kusoma dhana za kufikirika, Hivyo swali lako ni imagination na unaweza kujijibu kwa kuimagine
unaelewa maana ya neno "kwamfano"...?
 
Naelewa maana yake. Mfano uliouyumia hauna uhalisia na maisha halisi, umeegemea kwenye fikra zako! Jaribu kuleta mfano mwingine wenye uhalisia mkuu
ha ha ha..
basi ngoja nilete swali moja kwa moja.. umesema Mungu yupo kwasababu wewe upo sasa nani anafanya Mungu na wewe kuwepo..? na kuwepo kwako kunadhihirisha vipi kuwa mungu yupo..?
na kuwepo kwako yeye anapata faida gani..?
 
Kwanza hakuna afanyae Mungu kuwepo, Mungu alikuepo, yupo na ataendelea kuwepo. Mungu ndio kanifanya mimi niwepo kupitia kuumbwa kwa Adam na Eva vikapita vizazi na vizazi mpaka mi nikazaliwa, Mungu alimuumba mwanadamu ili amtumkie na amuabudu na kuvitunza vitu vyote vya duniani ili kuutukuza utukufu wa Mungu.

Katika kumuuabudu na kumtumikia Mungu tunapata faida nyingi sana hata hazihesabiki , kuhusu Mungu kupata faida kwa kweli swali liko juu ya uwezo wangu, labda umuulize mwenyewe kupitia sala atakujibu
 
Back
Top Bottom