Kwanini Mungu aliamua kutumia njia ya vitisho ili kujenga imani ya uwepo wake?

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,018
2,000
Kwa 100% binadamu wote wanaoamini kuwa Mungu yupo ni wale ambao nafsi zao zimejaa hofu na uwoga kutokana na vitisho mbalimbali ambavyo Mungu ameviweka juu yao.

Hata wewe unayesoma uzi huu muda huu unaamini Mungu yupo baada ya kuwa umetishwa sana na ukaingia hofu moyoni mwako na umeamua kuwa mnyonge tu na kuamini Mungu yupo baada ya kuogopa sana vitisho vyake.

Ukiachilia mbali vitu alivyoviumba,imetumika njia ya kutishana sana ili binadamu aamini uwepo wa Mungu kama ifuatavyo.

(i) VITISHO KATIKA KIFO.
Watu wengi sana wanaamini Mungu yupo baada ya kuingia hofu kwenye swala la kifo. Dini nyingi sana hasa uislam unawafundisha watu wake kuwa binadamu hupata maumivu makali sana tena sana kipindi anakata roho. Hasa mtu asiyemuamini Allah huteseka sana siku anakata roho. Baada ya vitisho hivi vya kifo,binadamu anajenga hofo moyoni na anaamua kuamini kuwa Mungu yupo ili ata akifa roho isitoke na maumivu makali. Je,wewe upo kwenye kundi hili?

(ii) VITISHO VYA JEHANAMU.
Binadamu baada ya kuambiwa kwenye vitabu vyake vya dini kuwa asipotenda mema siku ya mwisho Mungu atamchomwa moto basi jambo hili limewafanya watu wengi hata wewe mkuu waogope sana na waingie hofu moyoni ya kuchomwa moto na kuamua kuamini Mungu yupo kwasababu tu ya hofu ya moto wa jehanamu? Je, na wewe upo kwenye kundi hili?

(iii) VITISHO VYA KULAANIKA NA KUFIKWA NA MABAYA.
Kuna watu wengi sana hata humu JF wapo wanaamini Mungu yupo baada ya kuingia hofu kufikwa na mabaya ikiwepo magonjwa,vilema n.k. na wengine wameamua kuamini Mungu yupo baada ya kuogopa kulaaniwa na Mungu na kufikwa na mateso. Je,na wewe upo kwenye kundi hili?

(iv)VITISHO VYA SODOMA NA GOMORA.
Nyoyo za watu wengi sana zimeingia hofu kubwa sana juu ya Mungu baada ya kujua Mungu alisha wahi kuwachoma moto watu wa Sodoma na Gomora baada ya watu hawa kukiuka maagizo ya Mungu. Ili na wao wasichomwe moto kama ule wa Sodoma na Gomora watu wengi wameamua kuamini tu uwepo wa Mungu. Je na wewe upo kwenye kundi hili?

(v) VITISHO VYA GHARIKA LA NUHU.
Binadamu baada ya kusikia Mungu alishawahi kuuwa viumbe vingi kwa maji kwa kosa la kukiuka sheria za Mungu binadamu huyo ameamua kuingia hofu kubwa sana moyoni na kuamua tu kuamini kuwa Mungu yupo. Je na wewe upo kwenye kundi hili?

(vii) VITISHO VYA ADHABU YA KABURINI.
Dini zinawaambia watu wake kuwa ukifa ukiwa na dhambi basi ukiwa kaburini utapewa adhabu kali sana ikiwepo kupigwa na rungu kubwa sana utosini mpaka mbingu ya saba, kuumwa na nyoka mwenye sumu kali sana,kubanwa mbavu mpaka ukome. Haya yamewafanya watu wawe na hofu kubwa sana na hofu imewafanya waingie uwoga na kuamini tu Mungu yupo. Je na wewe upo kwenye kundi hili?

(viii) VITISHO VYA SIKU YA KIAMA.
Kuna dini zinaamini siku ya kiama jua litashusha chini watu wataungua sana, milima itavunjwa vunjwa na dunia itageuzwa chini juu na juu chini, wenye dhambi watafufuliwa wakiwa hawatamaniki na midomo yao imekuwa kama ya ngurue na kama ukiwa na dhambi siku ya kiama ukiwa na kiu ya maji basi unapewa usaha wa moto unaonuka sana ndio unywe n.k. Habari hizi zimejenga hofu kubwa sana kwa watu wengi na kuingia uwoga na kuamua tu kuamini kuwa Mungu yupo. Je na wewe upo kwenye kundi hili?

(ix) and the like.

MWISHO.
Hii inamaanisha binadamu mpaka atishwe sana na awe na hofu moyoni ndio aamini Mungu yupo tofauti na hapo hakuna mtu ambaye angeshughulika na mambo ya Mungu.
 

Ruge

JF-Expert Member
Aug 15, 2019
2,637
2,000
msingi wa dini ni uoga na sio imani
 

Attachments

  • FB_IMG_1593089368254.jpg
    File size
    35.4 KB
    Views
    0

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,068
2,000
Mkuu mimi ndio nimeuliza kabla hivyo kimantiki wewe ndio ulitakiwa ujibu swali then unauliza.

Jibu kwanza swali.
Mkuu mbona upo obsessed sana na Mungu?
Kwangu habari za Mungu ama Shetani ni imani kama nilivyozikuta. Kutaka maoni yangu binafsi ni kunirudisha nilikotoka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom