Habari wana MMU
Natumaini mko wazima ila wachache wanaoumwa nami nawaombea kwa Mungu awaponye,
Leo nimekuja na hoja hii ya baadhi ya watu ambao wanakuwa katika hali fulani ya maisha yaani wanapitia kipindi kigumu mpaka inafikia hatua ya wao kujikattaa na kujiona kuwa hawafai lolote na si chochote wanabalki wanyonge wasio na mbele wala nyuma wanabaki mtazamo wa kuona kila kitu hawawezi kabisa. Kila walifanyalo wanaona hawawezi na wanaishia kushindwa kutimiza zile ndoto zao waliaojiwekea hata wengine wanakufa na maono na ndoto zao pasipo kutimiza. Wengine kutokana na kukataliwa na watu au wenzi wao wa maisha wameona hakuna haya ya kuishi na wanajifupisha maisha yao, wamesahau kuwa uhai Mungu amewapa ili wamtukuze na kumshukuru yeye. Wamesahau kuwa yuko ambaye anaweza yote na ndiye mtetezi wa maisha yao. hebu soma hapa Jeremia 29:11 inasema 'Maana nayajua mawazo ninayowazia ninyi, asema Bwana , Ni mawazo ya amani, wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu mwisho' Jeremiah 32:'Maana nayajua mawazo ninayowazia ninyi, asema Bwana , Ni mawazo ya amani, wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu mwisho' na soma hapa 'Jeremiah 32:27 inasema'Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili; Je kuna neno Je kuna neno gumu lolote nisiloliweza' Kwake Mungu hakuna neno au jambo lolote litakalomshinda yeye kwake yote yanawezekana kama umekataliwa na Mchumba, Baba/Mama au Mume wako au rafiki yako wa karibu yuko yeye ambaye ni rafiki wa kweli na wala si mdanganyifu kwani Binadamu atasema leo anakupenda na kesho amebadilika amekuwa mwingine kabisa mpaka inafikia unajisemea moyoni si huyu ndiye aliyeniambia kuwa ANANIPENDA NA NI RAFIKI YANGU iweje leo amenikataa. Hivyo ndivyo binadamu walivyo wachukulie hivyohivyo na jifunze kuwasemehe kwani ni kigeugeu kabisa mwangalie Mungu ndiye rafiki yako wa kweli soma hapa Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake, 14' Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo [Yesu] BASI ondoka na dhana ya kujikataa kutokujikulbali kwani unaye RAFIKI WA KWELI naye ni Mungu Baba