Kwanini umaskini na si Maisha ya kawaida

Kwanini umaskini na si Maisha ya kawaida

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,438
Reaction score
3,951
Wana jamnvi, ebu tukae tutafakari, Kwanini mtu awe maskini. Kinachoweza kumsaidia mtu kuwa na maisha yake ya kawaida ni uwezo wake wa kufanya kazi, Elimu hata ikiwa ndogo bado anakuwa na uwezo wa kutafuta. Je kuna kitu kingine kinacho muandama mwanadamu na kumkandamiza ili asiwe hata na maisha ya kawaida. Je kitu hicho kinacho muandama kinaweza kuondolewa ili kisiendelee kumdidimiza mwanadamu. Kwa sasa tunao matajiri ambao hata darasa la 7 hawakufika na tunao wasomi walio jitahidi kupata pesa kwa njia zao nao matajiri. Kunani?
 
Utajiri ni siri ya mtungi aijuae kata.

Mtaka cha uvunguni sharti ainame, mtu anataka utajiri ila hafanyi mambo ya kumfanya awe tajiri.

Haba na haba hujaza kibaba, watu wanataka utajiri wa haraka wa kafara,upako, na kubet wasijue polepole ndio mwendo na haraka haraka haina baraka.

Usione vyaelea vimeundwa. Pambana, kuwa na subira, work hard work smart, acha tamaa.
 
images (11).jpeg
 
Mfumo wa maisha uliopo una kitako, kwenye kitako kuna watu wengi sana ambao ni casual au regular people ambao ni working class.. juu mfumo huo ni mwembamba sana ndo mana una watu wachache kina bahresa na Dewji etcetera.

Kwa kadri gepu kati ya wajuu na wa chini inavyokuwa kubwa ndivyo hivyo hivyo hawa watu wa chini wanakumbana na shida ambaz hazina mfano, ngumu kumez na nyingi kwelikweli. Na hivyo hivyo wale wa juu hawajui kule chini shida nn mbona watu maskini kias kile.

Elimu, population control, misaada 'grants au donation, aid' ni baadhi ya variable za kupunguza hali mbaya iliyopo kule chini ya mfumo huo na sio tiba kamili. Kinachozungumzwa kuhus maskin kama sababu ni walau sifa chache miongoni mwa nyingi walizonazo wengi wa maskini. Hawana elimu, hawana mitaji, hawana exposure, wavivu na watu wasiopemda maendeleo y wenzao.

Tatizo la umaskini ni tatizo ngazi ya mfumo, lakini umaskin huo huo unatibiwa ngazi ya kikundi cha watu katika mfumo mzima au ngazi ya mtu mmoja mmoja. Hii ni habari mbaya zaidi
 
Umaskini ni mfumo wa gombea goli ulioletwa na binadamu ; binadamu halisi wamegawanyika katika kundi la mke na mume.

Leo hii tunagombea pesa hamna cha maana ,ndiyo mambo ya asili bado ni muhimu ...Ukizaa tu mtoto atakutana na tabu za dunia ,ukizaa chizi ndiyo tabu kabisa.
 
Pengine mifumo ya kibepari inatudidimiza au kutupa wakati mgumu kuwafikia walioajiriwa juu.... Labda mifumo ya kijamaa iliyoboreshwa inaweza kuwaweka watu wote kwenye mizani sawa..
 
Pengine mifumo ya kibepari inatudidimiza au kutupa wakati mgumu kuwafikia walioajiriwa juu.... Labda mifumo ya kijamaa iliyoboreshwa inaweza kuwaweka watu wote kwenye mizani sawa..
Uko sahihi ,umaskini ni mfumo tu basi .Ubeparini mbaya watu wanapambana wawe juu na Wengine wawe chini.

Ubepari hata leo unaona futari inayohusu mafukara wanapenda matajiri ...Kiufupi ubepari unatengeneza roho za ubinafsi.

Mtu anayenunua gari la Mil 200 unamkuta tiktok anasema usisaidie maskini ,yaani kutoka 10k hataki ili kusaidia wengine.
 
Pengine mifumo ya kibepari inatudidimiza au kutupa wakati mgumu kuwafikia walioajiriwa juu.... Labda mifumo ya kijamaa iliyoboreshwa inaweza kuwaweka watu wote kwenye mizani sawa..
Moja kati ya nguzo moja ya ujamaa kama unakumbuka aliousimamia Nyerere ni KuPUNGUZA UKUBWA WA GEPU LILILOPO KATI YA TAJIRI NA MASKINI. Gepu hili kwemye ubepari huwaga linatanuka kila kukicha mana vitu vinatoka kwa maskini kwemda kwa matajiri.

Hili gepu ni baya sana mana maskini kabisa atafanya kazi kwa ajili ya kula tu (kuchumia tumbo), na tajiri atafanya ukwasi na atajilimbikizia mali ajabu. Leo hii mtu anamiliki mali hata hazikumbuki kwa kichwa mpaka aandike mahali wakati wafanya kazi wake anawalipa hela ambazo hata kula mlo kamili tu mtihani
 
Utajiri ni siri ya mtungi aijuae kata.

Mtaka cha uvunguni sharti ainame, mtu anataka utajiri ila hafanyi mambo ya kumfanya awe tajiri.

Haba na haba hujaza kibaba, watu wanataka utajiri wa haraka wa kafara,upako, na kubet wasijue polepole ndio mwendo na haraka haraka haina baraka.

Usione vyaelea vimeundwa. Pambana, kuwa na subira, work hard work smart, acha tamaa.
Nonsense,
 
Wanataka Utajiri kama wa Chief Godlove.
Mwaka juzi tumeona kabisa anapiga picha gheto tena akiwa na kitanda kimoja na Mbao zenye rangi nyekundu za 10k.

Leo hii anaishi Kifahari , mpaka unajiuliza how is it possible...
 
Back
Top Bottom