Heshima kwenu wakuu.
Mataifa kadhaa duniani wamechagua baadhi wa wanyama kuwa nembo za nchi zao. Mfano Bald eagle(tai) ni nembo ya marikani. Tai ni ndege anayepaa katika anga za juu sana kuliko ndege wote. Akiwa huko jicho lake linaweza kuona mbali hata mzoga wa sungura uliopo ardhini. Waamerika wanadai kwao tai anawakilisha nguvu, uhuru, akili na ujasiri wa kuona mbali. View attachment 407474
Turudi hapa Tanzania. Mnyama wetu wa Taifa ni Twiga. (Giraffe). neno giraffe limetokana na neno la kiarabu (xirefa)lenye maana ya anayetembea kwa maringo.
View attachment 407475
Je kwa nini wazee wetu waliamua kumchagua twiga?
Je mchakato wa kuamua mnyama yupi atumike ulichukua miaka mingapi?
Je kulikuwa na wanyama wengine au ndege waliopendekezwa zaidi ya twiga?
Je watoto na wajukuu wetu wakitaka kujua habari kama hizi watazipata wapi? watazisoma wapi?
Nawasilisha.
Wenu katika ujenzi wa Tz ya viwanda viiiiingi.
Aisee bora simba ni mfalme wa nyika. Akiunguruma wengine kimyaaa.. sasa twiga yeye kutembea kwa maringo tuu... halafu hanaga haraka.LABDA WABADILI N'A WAWEKE MNYAMA SIMBA LABDA HAO WANAO KUJA KUTUPORA MALI WATAOGOPA.......
OVA
Inawezekana, maana twiga ni mpole na anashagaaga tuHuyo tigwa anawakilisha upole na uvumilivu walionao watanzania.
Huyo tigwa anawakilisha upole na uvumilivu walionao watanzania.
Tumdai nembo awe simba basi mkuuAisee bora simba ni mfalme wa nyika. Akiunguruma wengine kimyaaa.. sasa twiga yeye kutembea kwa maringo tuu... halafu hanaga haraka.
Ni sawa ila kwa sasa wanyama ambao wanatangazwa kwamba wameibwa sana ni faru, mbwa mwitu na duma. Hawa twiga wahejaa maporini balaaLabda wanaibwa sana, wanahisi miaka ijayo watapungua au kutoweka hivyo wanawachora ili kubaki nao kwenye kumbukumbu ya picha
Mkuu nembo yenyewe haita heshimiwa kabisaaamimi napendekeza panya awe nembo ya taifa