Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anatumia muda mwingi kutafsiri Katiba na Sheria badala ya kutangaza sera?

Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu huleta Amani na Furaha

Kwa sababu katiba ndiyo msingi wa kila kitu, mtawala akikuta katiba inamuongoza katika haki basi watu watakuwa na furaha na hata wakilia watakuwa wanalia kwa machozi ya furaha.

Kama hujaelewa hilo la Uhuru na Haki basi jiongoze kwa kumsikiliza Bishop Mpemba

Source : Bishop Augustine Mpemba
 
Mwandishi wa makala sijui nijiweke kundi gani,mbona wengine Kila Mara wanasema wamejenga hiki na kike wakati ni kazi yao na kitu Cha kawaida kwa kuwa wananchi wanalipa Kodi,walitaka ajenge Nani wakati wao wanakusanya Kodi,Sasa hizo nazo ni sera?
Bora yeye anaetafsiri katiba anatufundisha na sisi wengine tusiojua
 
Nijuavyo mikutano ya kampeni ni kwa ajili ya kutangaza sera na ilani za vyama lakini nashangazwa na Tundu Lissu ambaye hutumia muda mwingi kutafsiri sheria na katiba ya nchi.

Mfano katika mkutano wa leo ametumia muda mwingi kuelezea utaratibu wa kumshtaki mtu na jinsi ya kumuita shaurini.
Akatolea mfano wa yeye kuitwa na NEC kienyeji.

Tundu Lissu elewa kwamba watanzania hawahitaji darasa la sheria bali uwaeleze utawafanyia nini wakikuchagua.

Maendeleo hayana vyama!
Haki za watu zimeelezwa katika sheria, mtu akijua haki zake basi hata kumwonea inakuwa ni ngumu. Kutokana na namna watu walivyobambikiwa kesi, basi faraja kubwa ya wananchi ni kutaka kujua wapambane vipi zamu yao yao ikifika ya kubambikiwa kesi, hata mipango ya uchumi ina base zake katika sheria.
 
Nijuavyo mikutano ya kampeni ni kwa ajili ya kutangaza sera na ilani za vyama lakini nashangazwa na Tundu Lissu ambaye hutumia muda mwingi kutafsiri sheria na katiba ya nchi.

Mfano katika mkutano wa leo ametumia muda mwingi kuelezea utaratibu wa kumshtaki mtu na jinsi ya kumuita shaurini.
Akatolea mfano wa yeye kuitwa na NEC kienyeji.

Tundu Lissu elewa kwamba watanzania hawahitaji darasa la sheria bali uwaeleze utawafanyia nini wakikuchagua.

Maendeleo hayana vyama!
Anagombea kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania
 
Leo akiwa Mkoa wa Kilimanjaro, Lissu kaahidi kuhakikisha anairejesha Tanzania enzi za ukoloni. Nimemsikia na kumona akiongea hayo mwenyewe kupitia televisheni ya ITV, muda mchache uliopita. Hivi maisha ya ukoloni yalikuwa bora kuliko yale baada ya uhuru?

Yaani Lissu kwa uongo hajambo, anaongeza kuwa Wakati wa ukoloni mamlaka yalikuwa kwa wananchi! Mambo ya ajabu sana haya...! Na mwenyekiti wake wa Chama anaogopa 'kumfunga' Lissu kengele.
Sielewi anatuchukuliake watanzania... hata kama ndo kutafuta kuungwa mkono na nchi zilizotutawala lakini sio kiivyo hii ni aibu watanzania hatupo hivi
 
Majukwaani wanadai maendeleo hayana vyama. Ila wenye kuleta hayo maendeleo kwa fedha ya walipa kodi uangalia kwanza ni wapi chama chao kinaongoza na huko kunakoongozwa na vyama vingine tofauti na wao ni kwa watoto wa kambo ambao hawalipi kodi!
 
Back
Top Bottom