Kwanini tunaibeba DP World kiasi hiki?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo tumeshanasa kwenye dude linaloitwa makubaliano mkataba, liko kama sumaku.
 
Huu mkataba unavyotetewa kwa nguvu zote lazima Rupia imeshapenyezwa
Mwarabu anawauliza ccm mnatoa hamtoi
watu wanajua wanachofanya
Sidhani kama wanaosaini mikataba hawajui kuwa mikataba ni ya hovyo. Inawezekana hii mikataba ni deal kabisa..... wanasaini wakiwa wanajua kabisa huko mbele itavunjwa na wanakubaliana na mwekezaji mshiko wao kabisa mkataba utakapovunjwa na taifa kupigwa faini.

Haiingii akilini kwamba tangu miaka ya tisini serikali ile Ile ya chama kile kile iendelee kusaini madeal ya ajabu ajabu. Kwamba haijajifunza kitu tangu lile deal la kwanza la hovyo la air Tanzania kukaundwa air alliance? Mikataba ya migodini, gesi....this might be Front and back corruption
 
Lugha ya malikia Ile, shule zenyewe kayumba, mashungi mwenyewe alifeligi karisitigi.
 
Nguvu Ccm wanayoitumia kwenye hili jambo kuielimisha wananchi ingetumika na kwenye mingine ningewaona wana uchungu na hii nchi.

 

 

Kuna mambo muhimu sana watu hawajadili kwenye huu mkataba
Mfano;
1. Je mwekezaji atanufaishaje watanzania (Kodi kiasi gani na Ajira?)
2. Ni mtaji kiasi gani unahitajika ili tuweze kupata Kodi tajwa hapo juu
3. Kuna watanzania au shirika la kitanzania linaweza kufanya huo uwekezaji?
4. Je mwekezaji anapewa nini hasa kwenye bandari (kushusha mizigo? technologia? etc

Sijawahi kusikia Biashara yoyote Duniani inayojadiliwa bila kutumia nguvu kubwa kujua ni faida kiasi gani Nchi itapata halafu wakisha ona inalipa ndio wanaenda upande wa pili kuhakikisha mkataba unakaa vizuri.
(kwa mjadala unaoendelea, sioni faida tutakayopata ikijadiliwa kitu kinachonifanya nione kuwa, wanaoendesha huu mjadala sio wafanya biashara)

Ninachomaanisha ni kuwa; Kama Biashara inalipa; tutumie wataalam wetu kurekebisha mkataba ukae vizuri tupate mapato na naamini kabisa watu wengi wanalalamika kwa ushabiki na hata wakiulizwa wanacho lalamikia wala hawakijui....wanabakia tu bandari inauzwa.........ukiwauliza wamesoma wapi hawajui.....
 
Kwa Malumbano yanayoendelea naona kweli kuna ukwasi kwenye mkataba
Ila Mama aangalie ikiwezekana/ikimpendeza aseme sasa tunaanza upya maana wengi naona hawakatai uwekezaji bali muundo wa mkataba
 
Kuna watu ndani ya ccm wanatakiwa wahukumiwe kunyong'wa hadi kufa
mana ni zaidi ya majangili.
 
Sijawahi ona mkataba unaotetewa kama huu, sijui hawaoni kwamba jinsi wanavyokazana ndiyo nasi mashaka yanaongezeka!
Ni kama serikali inatubembeleza jamani kubalini jamani vinginevyo....
Sitaki kufikiria Samia ana wakati mgumu kiasi gani kwa sasa...sijui ni pori gani aliloingia huyu mama round hii...anyways muda utaongea
 
You right
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…