Kwanini tunaibeba DP World kiasi hiki?

Kwanini tunaibeba DP World kiasi hiki?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,099
Reaction score
828,943
Kama ni kafara la kukimbiza moto basi limetubamba kisawasawa...Na kama ni dozi ya upumbavu aliyetunywesha katu overdose kasoro wachache mno...!

Kwa makosa makubwa na ya wazi kiasi kile kwenye ule mkataba wa DPW na Tanzania kama sisi ndio tunataka kuwekeza kwao wallah nakwambieni ungechanwa mapema asubuhi tena kwa matusi na kejeli za kila aina!

Sisi sote tu mashuhuda namna tunavyotendewa nje ya nchi kwa makosa madogo mno tena sometimes kwenye nyaraka tuu ambayo yanaweza kurekebishwa hapo hapo

Mali zetu nyingi zilizokamatwa nje ya nchi si kwamba zote zilikamatwa kihalali, nyingine ni makosa madogo tu ya kisheria
Fidia tulizolipa na tunazoendelea kulipa nje ya nchi baada ya kushindwa kesi, nyingine zinatokana na kukosa uzalendo tu wa wanasheria wetu na wahusika wetu na kushindwa kupigania na kuonesha shida ilipo

Kipindi kile cha corona ni wangapi wamesahau namna mamlaka za Dubai zilivyowanyanyasa na kuwadhalilisha wabongo ambao nyaraka zao za chanjo zilikuwa na makosa madogo mnoo.. Kuna baadhi walirudishwa airport na kupoteza muda na nauli zao

Magereza za Dubai zina watanzania kibao kwa kesi mbalimbali ambazo nyingine ni za kubambikiwa, kushukiwa na nyingine makosa madogo mno... Sisemi kutenda kosa hata liwe dogo ni halali la hasha bali kuna baadhi ya makosa yanahitaji kuelimishwa tuu

Wakenya wanaweza kuwa mashuhuda wazuri kwa mabinti zao wanaokwenda arabuni kufanya kazi mbalimbali hasa za ndani, yale wanayofanyiwa kule hakuna mwafrika anaweza thubutu kumfanyia mgeni
Kwahiyo linapokuja swala la nchi yao.. Wenzetu hawana utani hawana huruma na hawana chembe ya utu wala ubinadamu.. Wananyoosha rula..!

Sisi huku bongo ndio kwanza tunawasaidia wageni
Kuvunja sheria mbalimbali
Kuwatetea wanapoharibu
Kuiba
Kukwepa kodi
Kuwatendea ndugu zetu mabaya nknk..
Kwao wao hawana huu upuuzi hata nukta.. Sana sana utashirikiana naye ila akikupa kisogo unadakwa.. Kakuchomam, na ndio atakuwa shahidi wa kukuangamiza ukipandishwa kizimbani

Sasa hili bango la watanzania wenzetu kuutetea mkataba mbovu mbovu mbovu kiasi kile huu uthubutu wanaupata wapi? Na mbaya zaidi wakiongoza na CCM wenyewe.. Hii ni aibu ni fedheha na ni laana kwa taifa hili.. Huku ni kudhalilishwa kulikovuka mipaka yote!

Hakuna anayekataa uwekezaji, kinachokataliwa na wananchi wazalendo ni mkataba mbovu, wenye makosa yasiyorekebishika na usio na maslahi yoyote kwa taifa.. Kwani kuna shida gani mamlaka zikitamka kuukataa na kuufuta?
Kwani kuna shida gani kuanza upya?
Kwani kuna shida gani kuwatafuta wawekezaji wengine?
Kwani ni lazima huyu dp na si mwingine yoyote? Kwanini?

Yanayofanyika sirini yakiwekwa bayana matokeo huwa hasi! Mambo haya yalianza 2022 kwa siri, taifa halikushirikishwa tangu mwanzo.. Kila kitu kingekuwa bayana tangu awali kwa uwazi na kwa uzalendo wa taifa.. Tusingefika leo hapa tulipo

Natambua wazi nguvu ya pesa ilivyoshawishi maamuzi yote mpaka sasa japo hili litakanushwa kwa viwango vyote, lakini mwenye macho haambiwi tazama!
Natambua ubinafsi wa viongozi wengi wa ccm wanaotegemea kujikomba na kujipendekeza dpw itakapoanza kazi ili wapate chochote na kuwatafutia vibarua ndugu, jamaa, marafiki na michepuko yao.. Hapa ndio ukomo wao wa kufikiri unapoishia..!

Huu unaotutikisa mpaka sasa ni mmoja tu kati ya ile 37 iliyosainiwa huko...

Good morning Tanganyika
014ab9329eb5b0ecf142dcdf7b743548.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna kitu tumelaaniwa wa Africa na hatuji kuendelea kamwe kama hatutoacha basi ni ubinafsi.Hata tuwe na elimu,teknolojia au rasilimali kiasi gani kama viongozi pamoja na ma elimu yao makubwa makubwa bila uzalendo hamna kitu Africa tutakua masikini hadi mwisho wa dunia.Watu wachache wanafanya maamuzi ya kijinga yanayogharimu vizazi kwa vizazi.Kwa nchi za wenzetu kwa mfano waarabu wala hawana elimu au tecnolojia za hivyo lakini uzalendo wa kusimamia rasilimali zao kila mtu anufaike na hata vizazi vijavyo imefanya waendelee sana.
 
Kuna tetesi ccm wanahitaji pesa za uchaguzi mwakani hayati mkapa kwenye kitabu chake amekiri kuiba zaidi ya bil 300 kufanyia kampeni mwaka 2005 sasa imepita miaka 19 sasa pesa nyingi zinahitajika kufanyia kampeni mwakani

Chama kinachowaza kupata ushindi wa kishindo ni ngumu kuleta maendeleo matokeo yake ndio haya
 
Sio kila siku ni Jumamosi .. Hili this time litawaangamiza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saingine waliosaini hawakuelewa vizuri kingereza, wamesaini tu.
Kwani pana kiingereza kigumu basi hata sisi Kayumba tunakielewa sema walipewa Lupia hakuna mtu mwenye akili Timamu atakubali yale madudu aisee..ni vile wanaangalia leo kwa kupata wao sio Nchi inufaike kwa vizazi vijavyo ndio maana Nchi bado tunatafuta sare kwenye umasikini kwa sababu ya mikataba mingi ni kwa faida ya baadhi ya familia sio Watanzania wote.
 
Kama ni kafara la kukimbiza moto basi limetubamba kisawasawa...Na kama ni dozi ya upumbavu aliyetunywesha katu overdose kasoro wachache mno...!

Kwa makosa makubwa na ya wazi kiasi kile kwenye ule mkataba wa DPW na Tanzania kama sisi ndio tunataka kuwekeza kwao wallah nakwambieni ungechanwa mapema asubuhi tena kwa matusi na kejeli za kila aina!

Sisi sote tu mashuhuda namna tunavyotendewa nje ya nchi kwa makosa madogo mno tena sometimes kwenye nyaraka tuu ambayo yanaweza kurekebishwa hapo hapo

Mali zetu nyingi zilizokamatwa nje ya nchi si kwamba zote zilikamatwa kihalali, nyingine ni makosa madogo tu ya kisheria
Fidia tulizolipa na tunazoendelea kulipa nje ya nchi baada ya kushindwa kesi, nyingine zinatokana na kukosa uzalendo tu wa wanasheria wetu na wahusika wetu na kushindwa kupigania na kuonesha shida ilipo

Kipindi kile cha corona ni wangapi wamesahau namna mamlaka za Dubai zilivyowanyanyasa na kuwadhalilisha wabongo ambao nyaraka zao za chanjo zilikuwa na makosa madogo mnoo.. Kuna baadhi walirudishwa airport na kupoteza muda na nauli zao

Magereza za Dubai zina watanzania kibao kwa kesi mbalimbali ambazo nyingine ni za kubambikiwa, kushukiwa na nyingine makosa madogo mno... Sisemi kutenda kosa hata liwe dogo ni halali la hasha bali kuna baadhi ya makosa yanahitaji kuelimishwa tuu

Wakenya wanaweza kuwa mashuhuda wazuri kwa mabinti zao wanaokwenda arabuni kufanya kazi mbalimbali hasa za ndani, yale wanayofanyiwa kule hakuna mwafrika anaweza thubutu kumfanyia mgeni
Kwahiyo linapokuja swala la nchi yao.. Wenzetu hawana utani hawana huruma na hawana chembe ya utu wala ubinadamu.. Wananyoosha rula..!

Sisi huku bongo ndio kwanza tunawasaidia wageni
Kuvunja sheria mbalimbali
Kuwatetea wanapoharibu
Kuiba
Kukwepa kodi
Kuwatendea ndugu zetu mabaya nknk..
Kwao wao hawana huu upuuzi hata nukta.. Sana sana utashirikiana naye ila akikupa kisogo unadakwa.. Kakuchomam, na ndio atakuwa shahidi wa kukuangamiza ukipandishwa kizimbani

Sasa hili bango la watanzania wenzetu kuutetea mkataba mbovu mbovu mbovu kiasi kile huu uthubutu wanaupata wapi? Na mbaya zaidi wakiongoza na CCM wenyewe.. Hii ni aibu ni fedheha na ni laana kwa taifa hili.. Huku ni kudhalilishwa kulikovuka mipaka yote!

Hakuna anayekataa uwekezaji, kinachokataliwa na wananchi wazalendo ni mkataba mbovu, wenye makosa yasiyorekebishika na usio na maslahi yoyote kwa taifa.. Kwani kuna shida gani mamlaka zikitamka kuukataa na kuufuta?
Kwani kuna shida gani kuanza upya?
Kwani kuna shida gani kuwatafuta wawekezaji wengine?
Kwani ni lazima huyu dp na si mwingine yoyote? Kwanini?

Yanayofanyika sirini yakiwekwa bayana matokeo huwa hasi! Mambo haya yalianza 2022 kwa siri, taifa halikushirikishwa tangu mwanzo.. Kila kitu kingekuwa bayana tangu awali kwa uwazi na kwa uzalendo wa taifa.. Tusingefika leo hapa tulipo

Natambua wazi nguvu ya pesa ilivyoshawishi maamuzi yote mpaka sasa japo hili litakanushwa kwa viwango vyote, lakini mwenye macho haambiwi tazama!
Natambua ubinafsi wa viongozi wengi wa ccm wanaotegemea kujikomba na kujipendekeza dpw itakapoanza kazi ili wapate chochote na kuwatafutia vibarua ndugu, jamaa, marafiki na michepuko yao.. Hapa ndio ukomo wao wa kufikiri unapoishia..!

Huu unaotutikisa mpaka sasa ni mmoja tu kati ya ile 37 iliyosainiwa huko...

Good morning TanganyikaView attachment 2690651

Sent using Jamii Forums mobile app

Back
Top Bottom