Kwanini TRA wasitengeneze Software au Application itakayofanya kazi ya EFD Machines?

Chief

Platinum Member
Jun 5, 2006
3,291
2,619
Hizi mashine za kutoa risiti za TRA ni ghali hasa kwa mtu anayeanza biashara na hana uhakika wa mzunguko wa fedha. Uchunguzi mfupi niliofanya ni kwamba Bei ya chini kabisa ni Sh. 580,000. Bei ya juu ni mpaka shs 2m.

Natoa pendekezo lifuatalo kwa TRA. Watengeneze application ambayo inaweza kutumika kwenye simu na computer. Mtu anayeanza biashara mpya, TRA wana activate TIN number ya mteja ambapo baada ya mteja ku download application, ana create profile yake eg jina la biadhara, mwaka wa fedha etc. Kurahisisha zaidi, una download na ku create profile yako, halafu app inaangalia kwenye database ya serikali ya TIN, business name, etc, na kufanya auto approval. Kesho tu unaanza biashara.

Akianza biashara, atakuwa ana print risiti kupitia application wakati tu akiwa online. Faida ni nyingi sana mfano unafuu wa gharama na urahisi wa system, software upgrading, reporting system, TRA wanaweza kuifunga remotely etc. Sasa hivi machine ikiharibika inabidi kutafuta fundi maalum kutengeneza, au ununue ingine kwa bei ghali.

Mfano wa system hii ni Kama hapa chini.
 
Hope next year TRA watakuwa na solution itakayokuwa bomba Kama mbdala wa EFD
Inakera sana ukitaka kununua EFD machine, eti uende duka maalumu. Hapo tayari umewwka mazingira ya kupigwa bei. Software una download popote ulipo. Huu mtindo wa sasa ni wa kizamani ukitilia maana teknology ya Sasa.
 
Idea Safi Sana. Naunga mkono hoja. Suala ni application, simu au computer na printer basi. Hata hivyo bado cost ipo ya kununua printer, lkn printer kwa vile zitakuwa zinauzwa madukani itakuwa bei rahisi.
 
Printer za hizi risiti bei ndogo mno hata shs 40,000 unapata. Simu tayari unayo na app inakuwa bure. Compliance itakuwa kubwa Sana.
 
TRA ata hizo EFD zao kuna muda wanahisi kama zinawadanganya.sembuse hiyo app yako uliyoishauri.TRA hawana imani hata chembe na wafanya biashara.
jambo la maana ni kuifumua hii taasisi ili isukwe upya.ije kihuduma zaidi na sio kitemitemi.
 
Ooooh, kwani siku hizi hakuna sheria ya kwamba mauzo yako yakiwa 14m kwa mwaka au zaidi ndipo unaoaswa kutumia hiyo mashine?
 
Ni kweli ila unajua gharama si machines, gharama ni mfumo wa usambazaji na management ya hizo machines na software

Simu inacontrol vipi reports ili iwe rahisi kufanya tax examination from submited financials?

Unajua huu mfumo wa sasa unawawezesha kucontrol through x report na z report sababu machine ni kwa ajili ya tra tu. Haiibiwi, huwezi instal game mtoto akachezea n. K

Idea ya Mfumo ni mzuri ila wanaitaji kutulia sana.
 
Ooooh, kwani siku hizi hakuna sheria ya kwamba mauzo yako yakiwa 14m kwa mwaka au zaidi ndipo unaoaswa kutumia hiyo mashine?
Kama gross margin yako ni 30%, hapo gross profit ni 4.2m kwa mwaka na hujaweka gharama zingine. Hiyo ni chini ya laki na sabini kwa mwezi. Ukiweka machine ya 590,000 inakuwa gharama sana.
 
Ni kweli ila unajua gharama si machines, gharama ni mfumo wa usambazaji na management ya hizo machines na software

Simu inacontrol vipi reports ili iwe rahisi kufanya tax examination from submited financials?

Unajua huu mfumo wa sasa unawawezesha kucontrol through x report na z report sababu machine ni kwa ajili ya tra tu. Haiibiwi, huwezi instal game mtoto akachezea n. K

Idea ya Mfumo ni mzuri ila wanaitaji kutulia sana.
Ugumu upo wapi hapo? Si unaweka password? Suala si simu bali application. Kwani Mbona banks wana apps zao una access account yako bila shida na kufanya miamala?

Naamini apps inakupa avenue kubwa zaidi ya hivi vimashini, mfano unaweza uka intergrate na VAT reporting na mteja aingize manunuzi yote yenye VAT aliyofanya na TIN zake. Report inakuwa rahisi na instantly utagundua fake recept hata kabla ya kufika TRA. Tuachane na huu ukiritimba wa vimashini.
 
Siku TRA wakiamua kwa dhati kuingia kwenye matumizi ya Teknolojia katika ulipaji kodi ndipo wataanza kuipata kodi yangu, wakiendelea kung'ang'ania matumizi ya hizo mashine kandamizi za EFD nitaendelea kuwa MKWEPA KODI milele.
Hivi wanashindwaje kutengeneza App watu tukajisajili na michakato mingine ikaendelea kama kawaida? Hizo mashine za EFD ni biashara ya nani? Puumbavu.
 
Ugumu upo wapi hapo? Si unaweka password? Mbona banks wana apps zao una access na account yako bila shida?
Yes ila bank ukifanya kosa ukaibiwa pesa yako hilo si jukumu lao ni lako.

Imagine mfumo wa android ni wa dunia nzima na control yake ni ndogo sana TZ. Sasa uutumie kukusanya mapato ya nchi yako halafu wanaijeria, waisrael, wahindi, waarabu woote hao wana utundu wa kucheza na android software.

Inawezekana sana, ila si jambo la kukurupuka. Inahitaji kutulia na uwe na It wenye akili sana.
 
Siku TRA wakiamua kwa dhati kuingia kwenye matumizi ya Teknolojia katika ulipaji kodi ndipo wataanza kuipata kodi yangu, wakiendelea kung'ang'ania matumizi ya hizo mashine kandamizi za EFD nitaendelea kuwa MKEPA KODI milele.
Hivi wanashindwaje kutengeneza App watu tukajisajili na michakato mingine ikaendelea kama kawaida? Hizo mashine za EFD ni biashara ya nani? Puumbavu.
Exactly!! Ndicho hicho ninachozungumza. Inakera Sana.
 
Yes ila bank ukifanya kosa ukaibiwa pesa yako hilo si jukumu lao ni lako.

Imagine mfumo wa android ni wa dunia nzima na control yake ni ndogo sana TZ. Sasa uutumie kukusanya mapato ya nchi yako halafu wanaijeria, waisrael, wahindi, waarabu woote hao wana utundu wa kucheza na android software.

Inawezekana sana, ila si jambo la kukurupuka. Inahitaji kutulia na uwe na It wenye akili sana.
Android ni mfumo tu wa simu, lakini muhimu ni servers ambazo zitakuwa zinatunza hizo data ambazo I bet sio Android.
 
Ugumu upo wapi hapo? Si unaweka password? Suala si simu bali application. Kwani Mbona banks wana apps zao una access account yako bila shida na kufanya miamala?

Naamini apps inakupa avenue kubwa zaidi ya hivi vimashini, mfano unaweza uka intergrate na VAT reporting na mteja aingize manunuzi yote yenye VAT aliyofanya na TIN zake. Report inakuwa rahisi na instantly utagundua fake recept hata kabla ya kufika TRA. Tuachane na huu ukiritimba wa vimashini.
Jinga hilo Mkuu, limekariri ama ni kati ya wanufaika wa hizo mashine za kinyonyaji.
 
Back
Top Bottom