Kwanini tanzania tunafanya vibaya kwenye biashara ya utalii ukilinganisha na kenya?

Dec 9, 2008
77
7
MIMI NI MDAU WA UTALII ILA KWA NINI TUNAFANYA VIBAYA KENYA WANAFANYA VIZURI HIYO SEKTA IMEAJIARI WATU WENGI NA KWETU PIA INGEPUNGUZA TATIZO LA AJIRA.:msela:
 
Hatujui kujitangaza vizuri nje ya nchi. Mfano: Hadi leo watu wengi nje ya nchi wanajua kuwa mlima Kilimanjaro na Serengeti viko Kenya
 
Tunachemsha kwenye utalii kwasababu:

1. Miundo mbinu mibovu, hotel chache na zingine ama mbovu au zina huduma mbaya,

2. Kujitangaza si sana, vivutio vinavyotangazwa sana sana mlima kilimanjaro,

zanzibar, ngorongoro, manyara na serengeti. Promotion ya vivutio vingine,

hakuna.


3.Vivutio vya sehemu nyingine, ndio kama hivyo, havifikiki, mtalii gani ataenda

Gombe kuangalia sokwe kama sio jangili?


4.Serikali haiwekezi vya kutosha kwenye sekta hii ya utalii, wanategemea tu mtu

aje apande mlima kilimanjaro halafu arudi zake kenya kabla ya kwenda ulaya. We

are hopeless.


Tumeshindwa kuendeleza natural sceneries zikavutia. Wangekuwa ni wazungu

wangeteneza sehemu kama matema beach, mbamba bay na itungi port (Ziwa

Nyasa) na kuwa sehemu za kutalii na kutanua; visiwa vya ukerewe, ukala, na

visiwa vingine ndani ya lake victoria, visiwa vya mafia, vyote pamoja na miji ya

pwani ingetengenezwa vizuri-weka hoteli safi, beach bomba, watalii wajimwage.

Ni lazima serikali iwekeze kwa nguvu kwenye miundombinu pamoja na matangazo.

Sorry nimeandika haraka haraka.
 
Matatizo ni kuwa watanzania hatuna utamaduni wa biashara. Katiba bado inatulazimisha tuwe wajamaa. Serikali imeacha kufanya baadhi ya biashara ili wafanye biashara kuwa huria. Wakenya ni wafanyabiashara tungu uhuru kwani ni mabepari. Wakenya walio wengi wameteswa sana na ubepari na hilo ni tatizo kubwa. Akili zao zimechangamka kwa matatizo na sasa wanaongoza kwa kuuza tanzanite na dhahabu nyingi kuliko sisi. Wanauza maua, matunda na mboga mboga toka tanzania. Waganda wanatuuzia kahawa yetu nje. Rwanda nayo imeanza kuuza nje tanzanite, dhahabu na bidhaa nyingine za tanzania kwa utaratibu mzuri sana. Rwanda kufungua kampuni ltd ni masaa 24. Tanzania siku 7 kama una bahati. Tujifunze biashara na tuamini sector binafsi na tuisaidie na tujisaidie tusome biashara na ujasiriamali. Watanzania hatujui biashara kwani siyo utamaduni wetu. Tunapenda kuvaa tai na kuteseka maofisini. Mind set problem.
 
Utalii bongo ghali sana ukilinganisha na kenya, Safari Kenya plus flight for a week unakuta labda dola 1200. Safari hiyo hiyo bongo unakuta ni mara mbili yake manake kutua KIA ni ghali sana. unaweza lipa zaidi ya dola 1400 usafiri na wakati ukishukia kenya dola 600 via JOMO kENYATTA.

Kwa nini nauli ya bongo iwe juu sana ukilinganisha na Kenya ilhali kijiografia hatupo mbali sana???
 
mimi nimekuwa mfuatiliaji mkubwa sana wa sekta ya utalii na maendeleo yake kwa ujumla ila nachotakawa kukwambia kuwa utalii wa nchi yetu una mapungufu makubwa sana na kama mambo Fulani Fulani hayatarekebishwa basi zitakuwa kelele siziso na mafanikio .

Kwanza kabisa wadau wengi walio wekeza kwenye sekta hii wamekuwa na ndoto za kuwa mamilionea kwa muda mfupi na hatimaye utalii nchini umekuwa aghali kuliko nchi nyingi sana kitu kimoja lazima ukitambue kuwa mtu anapoamua kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine lengo lake sio siyo tu kuangalia simba au vivutio vingine bali ni kufanya mapumziko pia(relaxation) lakini kwa hali hii utalii hapa umeonekana kuwa ni kwa matajiri au watu wenye vipato vya hali ya juu kutoka ulaya na ndiyo maana utalii umekuwa wa msimu tu

Angali mifano hii Misri na Tunisia ukiondoa mapiramidi hakuna vivutio vingine zaidi ya bahari na jua ambalo wazungu wanapenda kujianika lakini takwimu zinaonyesha kuwa kwa nchi ya Urusi pekee ambayo uchumi wake si kama ujermani au nchi zingine za magharibi wanakwenda watalii 40000 kwa mwezi

Antaliya –Uturuki hakuna cha ziada zaidi ya bahari ya mediteranian lakini kwa msimu wa jua kuna watalii zaidi ya milioni tatu Je sisi ambao tunavivutio chungu mzima na bahari nzuri kabisa ambayo tunashindwa kuitunza ila hapa tatizo ni nini? Kwa mfano mimi na mke wangu tukiwa na dola za kimarekani 400 tunapata malazi kwenye hotel ya nyota 4 kwa siku tano huko Misri na kuna msimu hasa kwa kwa watalii kutoka nchi za ulaya unakuta hiyo dola 600 ina cover mpaka usafiri na wakati huo huo pato kubwa sana Misri linatokana na Utalii

Vivyo hivyo leo nikiwa na dola 900 inasaidia kwa usafiri na malazi ya siku saba hapo Uturuki ukiangalia nchini kwetu leo hii mimi na mke wangu tukitaka kwenda Serengeti tu kwa siku tano tunalipa kama dola za kimarekani 1800 per person per night maana yake nini yani kwa sisi watu wawili tunapashwa kulipa dola 3600 hapo hapo hatujatembelea vivutio vingine na ikiwa tumetoka mbali kama vile Finland basi nauli yetu ya ndege kwa wawili kwa KLM kama 3000USD na cha ajabu zaidi tunalipa dola 3600 wakati tunalala kitanda kimoja ambapo hata ukipiga hesabu sisi kwa siku kama tungekula hotel nyingine basi kwa chakula tungetumia dola 30 per day

Kwa ulaya hata kama mtu anapata mshahara mkubwa kuspend dola 7000 kwa siku tano ili kumuona tembo wakati siku hizi ulaya zoo zimejaa bwetele ambapo angeweza kumuona simba hizo ni pesa nyingi sana na ndiyo maana watalii wengi tunaowapata wengi ni matajiri ambao idadi yao si kubwa na wanakuja kwa msimu

Kuna kitu kinaitwa EURO TOUR nazani wengi wetu tumekisikia hii ni aina ya utalii kwa kutumia basi ambalo linazunguka miji mbalimbali ya ulaya kwa kawaida safari inaanzia Poland-ujerman-switzeland-france na miji mingine safari hiyo huwa inajuimusha kulala kwenye hotel nzuri pamoja na breakfast na dinner huwa ni ya siku kumi na moja na kwa ujumla ina cost dola 800 tu za kimarekani kwa hivyo watu wengi wa kawaida ulaya wangependa zaidi watumie dola 800 ili wapate pia relazatio ya hali ya juu kuliko kupoteza dola 70000

USHAURI WANGU
1)Kwanza kabisa wadau wa Utalii angalieni jinsi ya kupanga bei zenu nina aamini Tanzania kuna potential kubwa sana ya Utalii ambao tunaweza kuongeza kutoka Idadi ya 1.7 watalii wanaoingia kwa mwaka kufikia million 8 sioni tofauti kati yetu na Wamisri,Watunisia,waturuki bali ni maarifa tu au suitake kuniambia leo wamisri wanapata hasara wanapocharge dola 400 kwa siku tano kwa watu wawili

2)Pia jaribuni kupitia serikali kuweka vivutie vitakavyowafanya wawekezaji hasa wa hizi cheap airline kuja kuanza kuoperate Tanzania Leo hii kuna ndege nyingi sana Ulaya (cheapest airline) nyingi zinaishia Misri) na nyingine air arabia inaishia Kenya hizi ndege zitasaidia kwa kiwango cha asilimia 80 kuwaleta watalii kwa vipi?Leo hii ukitumia Air Arabia ktoka nchi nyingi za Ulaya hadi Kenya una save kama dola 1000 ambapo ungepanda KLM ,na kuna shirika moja la kihungary ambalo bei zake ni cheap hata siwahi kuona leo hii ukitumia hili shirika (vis airline) kutoka Warsaw hadi humburg)unaweza kulipa kama dola 12 tu hii ni ahisi sana Je tukiya comvice mashirika kama haya yakawa yanafanya safari zake atleast once a week si tutakuwa na watalii wengi .Maana yake lengo si kupata kupata watalii ambao ni wafanya biashara bali ni kpata watalii wengi zaidi hadi watu wa kawaida ambao ndiyo wengi sana
 
Nadhani Tanzania inafanya vizuri zaidi ya Kenya kwenye biashara ya utalii.

Kwa kifupi ni kuwa kwa mwaka Tanzania inaingiza mapato makubwa kupitia biashara ya utalii kuliko Kenya. Ingawaje Kenya inaingiza watalii wengi kuliko Tanzania. Hali hii inatokana na kuwa watalii wengi wanaokwenda Kenya ni wale wa bei nafuu wakati watalii wanaoingia Tanzania ni wale wenye uwezo wa kulipa gharama za juu.
 
Nadhani Tanzania inafanya vizuri zaidi ya Kenya kwenye biashara ya utalii.

Kwa kifupi ni kuwa kwa mwaka Tanzania inaingiza mapato makubwa kupitia biashara ya utalii kuliko Kenya. Ingawaje Kenya inaingiza watalii wengi kuliko Tanzania. Hali hii inatokana na kuwa watalii wengi wanaokwenda Kenya ni wale wa bei nafuu wakati watalii wanaoingia Tanzania ni wale wenye uwezo wa kulipa gharama za juu.

You must be dreaming, unafikiria kiCCM CCM !!!!
 
You must be dreaming, unafikiria kiCCM CCM !!!!

Lete fact acha uvivu wa kazi.., hebu tandika hapa chini jumla ya watalii walioingia Kenya na Tanzania mwaka jana au juzi na jumla ya mapato yalioingizwa na kila nchi....

kwa kuku saidia tu angalia hizi links hapa chini:

http://www.eturbonews.com/14251/top-slot-east-africas-tourism-tanzania-vs-kenya

hapa utaona paragrph moja inasema hivi

"While the tourists who visited Kenya spent an average $500 per trip, those visiting the neighbouring country spent about $1,600 for every trip."

Idadi na makadirio ya wanaokwenda Kenya:
http://africabusiness.com/2010/10/15/kenyan-tourism-figures-set-to-hit-1-2m-mark/

Mkadirio ya Tanzania haya hapa chini:
http://www.eturbonews.com/18070/tanzania-targets-17b-tourism-revenue

Kwa kifupi Watalii wanaokuja tanzania wanalipa zaidi ya mara mbili ya wale wa bei nafuu wanaokwenda Kenya.. Pia tazama idadi ya watalii wenyewe wanaokwenda kila nchi utaona tofauti ni ndogo sana...nafkiri sasa utakuwa umepata jibu ni nchi gani inayopata hela nyingi zaidi.

Inabidi uamke kutoka usingizini...
BTW: Hayo ya CCM umeyaleta wewe (kwanza hili sio jukwaa la siasa au uchaguzi...!) na unaonyesha ni jinsi gani usivyokuwa mfuatiliaji wa posts humu ndani....
 
Back
Top Bottom