Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,529
- 41,045
Nina hakika, kukifanyika sensa ya kupima ni taasisi gani ya serikali iliyo ya hovyo kuliko zote, Jeshi la Polisi litashika nafasi ya kwanza.
Siku za nyuma kulipokuwa kukitolewa mwenendo wa rushwa nchi, taasisi ambayo kila mwaka ilikuwa inaongoza kwa rushwa ni Jeshi la Polisi likifuatiwa na mahakama.
Jeshi letu la Polisi limejaa maharamia , badala ya kuwa kioo cha utiifu wa sheriana maadili, ndiyo linaongoza kwa kutenda mambo yaliyo kinyume cha sheria.
Badala ya kulinda raia, jeshi la polisi likilinganishwa majeshi yetu mengine yote, ndilo linaloongoza kwa kuua raia.
Watu waliopo ndani ya Jeshi la Polisi, wengi wao ni watu wa ajabu ajabu. Wengine wanafahamika jinsi waliyokuwa watu wema, waungwana, wenye maadili, lakini wakijiunga tu na Jeshi la Polisi, utashangaa.
Hawajui hata kuhoji, mara nyingi ni watu wa kufokafoka.
Hivi chuo cha Polisi huwa kinatoa mafunzo ya namna gani? Kwa nini watu wakienda hicho chuo, wakitoka wawe watu wa ajabu katika jamii?
Ili kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoendana na ustaarabu wa Dunia, ni vema Jeshi la Polisi likaundwa upya, hatua ya kwanza ni kuangalia mitaala ya chuo cha Polisi maana ukiangalia matendo ya Polisi wakitoka hicho chuo, ni kama wanaenda kufundishwa ugaidi wa kidola badala ya kuwawadimamizi wa sheria.
Lakini pia kufanyowe tathmini kuona kama ni halali watu wenye akili kidogo, walioshindwa kwenye masomo, ndio wanaostahili kuwa Polisi.
Kuna baadhi ya mambo wanayoyafanya, tunaweza kuwalaumu, kumbe yanachamgiwa na uwezo mdogo wa akili.
Sifa za mtu kuwa askari Polisi ziangaliwe upya. Tusiwe na hao polisi ambao hawajui hata mwongozo wao wa kazi (Police General Order - PGO).
Rais Samia anataka kuijenga Tanzania inayoendana na ustaarabu wa Dunia, lakini tatizo moja kubwa lipo kwa Jeshi la Polisi, ambalo kimsingi ni primitive,ni jeshi lisiloelewa hata thamani ya utu.